shida inakuja pale, ameshaitwa sana na vikao vya maboss wake kurekebisha baadhi ya mienendo yake, yeye amekaidi mbele zao kwamba hawezi kupangiwa (kwa fununu za ndani), anajiona yeye ni maarufu sana pale kijitonyama kiasi kwamba hawana uwezo kumtoa kwasababu ameshajenga mizizi ya kutosha na waumini watamtetea, ndio maana amenyamaza kimyaaa hataki kuwanyamazisha hao waumini wake. dawa yake Malasusa anatakiwa aidha afunge kanisa kwa muda kupisha upepo kupita, halafu awaambie tu waumini kwamba anayetaka kuja kusali aje, asiyetaka byebye. kwasababu kanisa lile sio la mtu, ni la kkkt, hata kama wanajiona wamechanga pesa san akujenga, haimaanishi kwamba wanalimiliki, na walioko mle haimaanishi kwamba watakaa mle milele wanaweza kuhama wapendavyo, hivyo anayetaka aendelee kusali, asiyetaka amfuate kimaro.
ila kosa kubwa wataweka precedent mbaya ni kuonekana wameshindwa mbele ya kimaro kwa kumrudisha, kwasababu atatokea tena mchungaji sehemu nyingine atafuata tabia anazofanya kimaro za kujiona maarufu na hawezi kuhamishwa pale (wakati waanzilishi wa kanisa la pale walishahamaga hata yeye alitokea kariakoo kkkt, alilikuta tu pale). kila mchungaji atakuwa anafanya tu hivyo na kubishana na wakubwa zake akijua waumini watamtetea. ikiwezekana hata kumfukuza wafukuze tu.