Mchungaji Emmanuel Rajabu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato atupa jiwe gizani

Kitabu cha Ufunuo tu ni mafumbo ya kutosha , manabii wengi tu waliwasilisha ujumbe wao kwa lugha mficho na walieleweka
Hata Yesu aliongea kwa mafumbo sana tu kasome Biblia upya
Nitajie nabii gani kwenye biblia aliwahi kumtamkia mafumbo mfalme. Iwe ni Daniel, Eliya Mtishbi, Elisha n.k
 
Eliya Mtishbi alikuwa muwazi kwa mfalme hadi akatishiwa maisha yake. Yohana Mbatizaji aliuwawa kwa kusema ukweli, Daniel hakuwahi kumficha Nebukadreza licha ya misimamo mikali ya Nebukadreza.

Mtumishi wa Mungu unapokuwa na uhakika na ujumbe wako juu ya uovu wa kiongozi wa nchi, ni lazima uuseme kwa uwazi, hakuna mtumishi wa Mungu aliyebeba roho ya uoga.

Ni heri na yeye angekaa kimya tu kama hawezi kuweka wazi kuliko kuongea kwa mafumbo mafumbo.
 
Nafkiri na yeye asingeongea kwa mafumbo. Hakuna nabii wala mtumishi wa Mungu ktk Biblia aliwahi kuwa mtu wa mafumbo.


Biblia ya wapi unayoiongelea wewe. Kama ni mkatoliki unatakiwa uende japo kwenye mafunzo yale ya awali katekisimu.

Tangu kale, hata Madiha Kristo, aliwafundisha watu kwa mithali na mifano, hadi mitume wake mara kadhaa walimwuliza kupata ufafanuzi. Naye akiwajibu aliwaambia kuwa anafanya hivyo ili wale wa shetani, wasikie lakini wasielewe, watazame lakini wasione.

Hakuna kitabu katika biblia kilichoandikwa kwa mafumbo mengi kama kitabu cha ufunuo.
 
Tunazungumzia habari ya nabii kuzungumzia ujumbe wa kitaifa na sio mafundisho ya makuzi ya kiroho.
 
Viongozi wetu wamekosa vision wanatumia dini kuwa ajenda zao bila kujua madhara yake mbeleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…