Jamani huku tunakoelekea ni pabaya mno, kweli nyakati tulizopo ni za mwisho , nimesikitishwa na kitendo cha gwajima kugeuza kanisa kama kijiwe cha kurushiana maneno na watu wa mataifa, akae ajue kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu(kama anavyojiita) na makonda ni wa mataifa tu kama watu wengine, kitendo cha kumchafua kwa maneno ya kashfa sio tu anajishushia heshima Bali ni analichafua kanisa ,kama mtumishi wa Mungu hakupaswa kufanya vile, Mara mia angetumia sheria zaidi kuliko anachokifanya, gwajima hana hekima za kimungu, nina mashaka na cheo chake.
Huwezi kutumia madhabahu ya Mungu kutoa maneno machafu kwa watu wa kimataifa,akumbuke watu wamefuata Neno la Mungu,Neno la uzima ili wapone kiroho,unapitumia kanisa kuhubiri habari za mtu tena kiongozi wako kwa maneno machafu,hii dhambi itamtafuna gwajima na ni zaidi ya laana katika kanisa lake.
Gwajima anahitaji maombi,gwajima anaitaji hekima ya ki mungu zaidi ili apone,nawaonea sana huruma waumini wa gwajima wanaonekana kuwa vipofu,hawaoni wala kuambiwa kitu.Mungu amsaidie sana gwajima.