Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo. Adai yeye ni zaidi ya Rais

Gwajima haweza kumsamehe Makonda mpaka atakapovunja madhabahu ya machungu na hasira kwenye moyo wake. Ni aibu sana kwa mtu anayejiita mtumishi wa Mungu kuwa na roho ya kisasi namna hiyo. Angejifunza kwa baba Askofu Pengo alivyojibu baada ya yeye Gwajima kimtukana.

Gwajima amethibitisha jinsi alivyo na madhabahu hayo ya machungu na hasira. Hii ni sehemu ya mafundisho kanisani kwake hapo mwaka 2012. Mchungaji anayehuduma kanisani kwake alifundisha neno nzuri sana kuhusu kusamehe. Nafikiri mafundisho haya hayakumsaidia kabisa Gwajima.

https://www.google.com/url?sa=t&sou...ggcMAA&usg=AFQjCNHaqYL0dLJXGBlIha4p6DvyEVHXyA
 
Nukuu ya Mtumishi Gwajima aliposema atafanya nini baada ya kuchafuliwa na issue ya drugs

"Wajinga hulipa kisasi
Wenye akili huachia
Walio na Mungu husamehe,
Mimi nina Mungu kwahiyo nasamehe"

Kinachoendelea kanisani kwa Gwajima haki hakisi hata nukta moja ya alichokisema

Watumishi kwa mujibu wa bibilia wanatufunza tusamehe saba mara sabini,
Sala ya Bwana inasema Mungu atusamehe kama tunavyo wasamehe waliotukosea

Gwajima aliwahi kumporomoshea matusi mazito askofu Pengo, lakini Pengo alijibu namsamehe na nitamuombea kwa Mungu

Katika ukristo vita yetu si ya kimwili bali kiroho, Gwajima anapigana vita ya kimwili sasa, goti pekee lilitosha kumuachia Mungu afanye mustakabali kwa alichofanya makonda kwa mtumishi

Gwajima amesamehe nini sasa? Kauli kali za kidunia dhidi ya mtu aliye mkosea hazi akisi maneno yake kama mtumishi, Mungu wetu hadhiakiwi wala hapiganiwi kwa nguvu na fitina za kidunia
Ni kupitia maombi, kuongea na Mungu direct na kumuachia Mungu kutenda kwa kadiri imfaayo

Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema Hii haina uhusiano wowote na kumtetea Makonda dhidi ya kashfa ya kutumia vyeti vya kugushi.
Kama raia mwema naunga mkono Makonda athibitishe elimu yake na ikiwa amefoji sheria ichukue mkondo wake kama kawaida
Gwajima amesha samehe ila anachokifanya nikujisafisha kwa waamini wake lkn pia anamueleza MUNGU wake kwann bwana mwanao naumizwa kwa maneno ya uongo ,kwann bwana sasa katika kuyasema hayo MUNGU anayajibu hapohapo.kwa hiyo watu na jamaa yenu mvumilie to.
 
Kwa kusoma vitabu vyote vya Mungu kuanzia injili kuna sehemu Yesu aliingia mahekaluni akavunja vunja mali za wayahudi tena akiwa na jazba, Zaburi ya Daudi inakuambia kua Daudi hakua wa michezo! Aliwatandika kweli wapinzani wake kina Goliat, Musa alipambana na jabali La mtu Firaun mpaka tone la mwisho.Mtume Muhammad S.A.W alipigana vita vya uhud huku akiongoza msafara tena akiwa mkali kweli kupambana na maadui zake. Leo upole na uoga wa watumishi wetu hawa uko kwenye vitabu gani?

Hivyo kua na Watumishi wa Mungu wapo wapo tu wanatukanwa wameufyata,Wanaonewa wameufyata hakuna kitu Kama hicho.Hakuna kitabu kinachosema unapoonewa ukae kimya Mungu atakulipa, Hakuna! You should show reactions!

Ndio maana hata kwa kutazama sinema zilizochezwa kuigiza maisha ya Yesu utaona hakuna sehemu alipokua akicheka Cheka hovyo, hakuna sehemu alipokua akimuonea mtu haya,alimwambia Petro kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu! Ni kwa sababu alikua anajua tabia ya Petro.

Nadhani hata Mungu anawapenda sana wapambanaji wake wasiokua wanafki, wasiokua watu wa "ndio mzee" Sidhani kama mtumishi wa Mungu ukasimama kuusema ukweli na ukawa mkali Mungu akakuchukia.

Sheikh Ponda na Gwajima aina ya watumishi wa Mungu waliothubutu. Wako tofauti sana na wengine.
 
Hoja yangu ni nikuu ya Gwajima mara tu baada ya kutoka sentro

Vyeti tupo watu wengi sana tutahoji maana haya ni ya kaisari mkuu
Wenzio wamefungwa ufahamu na "pepo vyeti". Yaani huwezi kujadili hoja tofauti hata kama ni constructive.
 
Kwa kusoma vitabu vyote vya Mungu kuanzia injili kuna sehemu Yesu aliingia mahekaluni akavunja vunja mali za wayahudi tena akiwa na jazba, Zaburi ya Daudi inakuambia kua Daudi hakua wa michezo! Aliwatandika kweli wapinzani wake kina Goliat, Musa alipambana na jabali La mtu Firaun mpaka tone la mwisho.Mtume Muhammad S.A.W alipigana vita vya uhud huku akiongoza msafara tena akiwa mkali kweli kupambana na maadui zake. Leo upole na uoga wa watumishi wetu hawa uko kwenye vitabu gani?

Hivyo kua na Watumishi wa Mungu wapo wapo tu wanatukanwa wameufyata,Wanaonewa wameufyata hakuna kitu Kama hicho.Hakuna kitabu kinachosema unapoonewa ukae kimya Mungu atakulipa, Hakuna! You should show reactions!

Ndio maana hata kwa kutazama sinema zilizochezwa kuigiza maisha ya Yesu utaona hakuna sehemu alipokua akicheka Cheka hovyo, hakuna sehemu alipokua akimuonea mtu haya,alimwambia Petro kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu! Ni kwa sababu alikua anajua tabia ya Petro.

Nadhani hata Mungu anawapenda sana wapambanaji wake wasiokua wanafki, wasiokua watu wa "ndio mzee" Sidhani kama mtumishi wa Mungu ukasimama kuusema ukweli na ukawa mkali Mungu akakuchukia.

Sheikh Ponda na Gwajima aina ya watumishi wa Mungu waliothubutu. Wako tofauti sana na wengine.
Acha kumfananisha Shekhe Ponda na Watuhumiwa wa madawa ya kulevya...
 
Kama mlitegemea msamaha basi mmeingia choo kilichojaa manyigu poleni, gwajima piga kazi oparesheni kushikisha adabu lazima iendelee tu hamna namna
Pepo limemdhalilisha kwa kugoma. Aibu yenu msiojua mnachokishabikia
 
Tofauti yao ipo juu ya yule wanayemuamini Ni ambayo mmoja ( unique), hakuzaa wala kuzaliwa,wala hana hata mmoja anayefanana naye.
 
Shehe ponda hakuwai kusema kuwa anafufua watu. Usimfananishe na matapeli
 
we jamaa muongo sana wewe tatizo unaangalia muvi unaconclude eti vitabu vyoooote hakuna kitabu chochote. nakupa kazi ndogo tu nitajie vitabu vya mungu ulivyowahi kusoma hata vitano tu japo kuna malaki ya vitabu kama so mamilioni. Acha kupotosha. Antibashite movement
 
sheikh ponda blue blue hakuna kupepesa macho........alimshambulia JK japo alikuwa wa dini yake hakuwa mnafk kwa kwel
 
Ninakubaliana na hoja hii kwa kuwa moja kati ya kazi za dini ni pamoja na kukemea maovu. Dini ambayo watumishi wanataka sadaka tu haitufai hata kidogo. Hata Yesu alikuwa akikemea watawala waovu na ndiyo kilichopelekea kifo chake. So dini ambayo husoma biblia au Kurwani na kupokea sadaka pekee haijitoshelezi.
 
Kitu pekee nnachopenda kwa Gwajima ni namna anavyojiamini. Jamaa anaongea kwa fact na sio mnafki wa kupendelea mtu flani. He is Unique.
 
Back
Top Bottom