Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais...
Huyu nihttps://youtu.be/BuwarpFj8E8
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.
Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.
Ni nabii wa uongo kwa sababu anahubiri uongo.
Uongo wa Gwajima ni Kumiliki Vyeti vya Daudi Albert Bashite na Paul Christian Makonda Mezani Kwake!.
Ila pia Mchungaji Gwajima amedai, anavyo vyeti vyote ofisini kwake tangu cha Daudi Albert Bashite alichopata Divisheni 0, hadi cheti cha Paul Christian alichounganishiwa na Christina!, na kudai kuwa ana mshitaki Makonda kwa Ndalichako na kwa Magufuli, na asipochukuliwa hatua zozote, yeye atashangaa sana na atavitoa vyeti hivyo hadharani, umma uvione. Jee hii inaweza kuwa kweli?, huu sio uongo mwingine wa mchana kweupe?!. Hili la Mchugaji Gwajima kudai anavyo vyeti vya Daudi Bashite na Paul Christian, kwa maoni yangu, huu ni uongo!, kwa sababu nijuavyo mimi, mtu ulikuwa ukipata Div. 0 hupewi cheti chochote na NECTA zaidi ya Leaving Certificate, Leaving huwa haionyeshi umepata nini, sasa hicho cheti cha Daudi Bashite alichonacho Mchungaji Gwajima, kinachoonyesha Daudi Bashite alizungusha, Gwajima amekitoa wapi?. Kwa vile Daudi Bashite alifeli darasa la saba Nyanza, hawezi tena huyo huyo Daudi Bashite akajiunga na Shule ya Sekondari ya Pamba ambayo ni ya serekali, bali Daudi Bashite baada ya kufeli darasa la 7, hapo ndio mwisho rasmi wa jina la Daudi Albert Bashite, hivyo mtu aliyejiunga na shule ya sekondari ya Pamba, sio Daudi Bashite, bali alitumia jina la mwanafunzi mwingine aliyefaulu, hivyo Mchungaji Gwajima, hawezi kuwa na vyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha kuwa alizungusha. Kwa kifupi, hakuna Daudi Bashite yoyote aliyesoma sekondari, Daudi Bashite original, aliishia darasa la saba!, hivyo kama Mchungaji Gwajima, anadai, anavyo vyeti vya Daudi Bashite, vinavyoonyesha alipata Div 0, huu utakuwa ni uongo!, ila mtanisamehe sana, sisi wengine tuu miongoni mwa wale wenye imani haba kamaTomaso, hatuamini mpaka tuone!. Kwa hapa naendelea kumwita Mchungaji Gwajima ni muongo hadi pale atakapo vitoa vyeti vya Daudi Bashite hadharani tuvione ndipo nitaamini!.
Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.
Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Paskali