Mchungaji Gwajima ni nani? Tukianzia hapa Tutajua namna ya Kudeal na watu aina yake

Mchungaji Gwajima ni nani? Tukianzia hapa Tutajua namna ya Kudeal na watu aina yake

Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais...

Huyu nihttps://youtu.be/BuwarpFj8E8

Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?.
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".

Mchungaji Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?.
Hii ni thread ya swali kumhusu Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, Mchungaji, Dr. Josephat Gwajima, Jee ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.

Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada, tena mahubiri juu ya chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.

Ni nabii wa uongo kwa sababu anahubiri uongo.
Uongo wa Gwajima ni Kumiliki Vyeti vya Daudi Albert Bashite na Paul Christian Makonda Mezani Kwake!.
Ila pia Mchungaji Gwajima amedai, anavyo vyeti vyote ofisini kwake tangu cha Daudi Albert Bashite alichopata Divisheni 0, hadi cheti cha Paul Christian alichounganishiwa na Christina!, na kudai kuwa ana mshitaki Makonda kwa Ndalichako na kwa Magufuli, na asipochukuliwa hatua zozote, yeye atashangaa sana na atavitoa vyeti hivyo hadharani, umma uvione. Jee hii inaweza kuwa kweli?, huu sio uongo mwingine wa mchana kweupe?!. Hili la Mchugaji Gwajima kudai anavyo vyeti vya Daudi Bashite na Paul Christian, kwa maoni yangu, huu ni uongo!, kwa sababu nijuavyo mimi, mtu ulikuwa ukipata Div. 0 hupewi cheti chochote na NECTA zaidi ya Leaving Certificate, Leaving huwa haionyeshi umepata nini, sasa hicho cheti cha Daudi Bashite alichonacho Mchungaji Gwajima, kinachoonyesha Daudi Bashite alizungusha, Gwajima amekitoa wapi?. Kwa vile Daudi Bashite alifeli darasa la saba Nyanza, hawezi tena huyo huyo Daudi Bashite akajiunga na Shule ya Sekondari ya Pamba ambayo ni ya serekali, bali Daudi Bashite baada ya kufeli darasa la 7, hapo ndio mwisho rasmi wa jina la Daudi Albert Bashite, hivyo mtu aliyejiunga na shule ya sekondari ya Pamba, sio Daudi Bashite, bali alitumia jina la mwanafunzi mwingine aliyefaulu, hivyo Mchungaji Gwajima, hawezi kuwa na vyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha kuwa alizungusha. Kwa kifupi, hakuna Daudi Bashite yoyote aliyesoma sekondari, Daudi Bashite original, aliishia darasa la saba!, hivyo kama Mchungaji Gwajima, anadai, anavyo vyeti vya Daudi Bashite, vinavyoonyesha alipata Div 0, huu utakuwa ni uongo!, ila mtanisamehe sana, sisi wengine tuu miongoni mwa wale wenye imani haba kamaTomaso, hatuamini mpaka tuone!. Kwa hapa naendelea kumwita Mchungaji Gwajima ni muongo hadi pale atakapo vitoa vyeti vya Daudi Bashite hadharani tuvione ndipo nitaamini!.

Jee Maneno na Matendo ya Mchungaji Gwajima ni Kama Yesu, ni ya KiMungu?.
Swali ni jee huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Mchungaji Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Jee huyu Mchungaji Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?. Mchungaji Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Jee huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Jee kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?.
Mchungaji Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Mchungaji Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.

Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma unga kwa Mchungaji hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Paskali
 
Hahahaa kwa wasiomjua gwajima wataisoma namba, jamaa hatishiki na hana kizibiti mwendo wa ulimi. Bashite kalikoroga wacha alinywe, alitegemea gwajima aende mahakamani ili serikali ya asiyejaribiwa imtume mwanasheria mkuu imtetee. Sasa waende mahakamani wao waone jinsi bashite na genge lake watakavyoaibishwa
 
Mchungaji gani anatembea na wake za watu na kuaribu ndoa? arafu eti wafuasi wake wanaenda kufunga pingu za maisha kwake,tafakalini!
Kua utayaona! Ukifuatilia maisha ya viongozi wa dini, hutakaa umwamini Mungu. Tunajua mengi.
 
1. Ni msukuma anayetumia uchawi wa gamboshi kuwalagai wafuasi wake

2. Ni mtu aliyejitangazia uchungaki, uaskofu mwenyewe bila kuwekewa mikono na mtu yeyote

3. Ni mtu anayejiita ' DOCTOR" lakini haijulikani alisoma lini na wapi hiyo PHD hewa na kama vyuo alivyosoma( if any ) vinatambuliwa na TCU

4. Ni mropokaji anayesema anatumia watu " MAKOMBORA" wakati hiyo sio sifa ya ukristo

5. Anamiliki helcopter mbili na mali za thamani kubwa lakini kanisa kaezeka kwa mabanzi na mabati ya ......?


hihihihi hahahaha yani nacheka balaa
 
Hata alivyomtesa Mbasha kwa my wife wake Florah
1.png

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
1.Gwajima ni Mchungaji wa Kondoo wa mungu....
2.Ana Vyeti vya Daudi... (sio Daudi wa Goliath....namzingumzia wa Kolomije-Misungwi)
3.Yeye akiongea na watoto wake..... viongozi hukimbilia makanisa mengine kulia.
4.Ana Helkopta
5.Anategemea kununua ndege
Hiyo namba 5. Anategemea kununua ndege kwa biashara gani?[emoji23] ndege wanamchangia maskini na matajiri wanaosali kwake, yeye anakula bata waumini wanaishi kwa Shida tena wanabudu wakiwa juani, binadamu bhana
Gwajima kwa hulka yake hawezi kua mtumishi wa Mungu ( ni mtazamo wangu na Mungu anisamehe kwa kutenda kosa la kumhukumu mtu)
 
gwajima ni yule alienda koromije na chopa eti makonda akaona wivu...
gwajima na makonda wamezaliwa kijiji kimoja ila walikuwa hawajuani
 
Kabla sija comment kuhusu Gwajima naomba vyeti vya bashite viwekwe hadharani
 
Askofu na Mchungaji Gwajima amekuwa moja ya watu maarufu na gumzo kubwa sana nchini. aina hii ya watu wapo duniani kote kwa Dini au Imani zote. Mtu wa namna hii unapoanza naye vita unapaswa kwanza kujichunguza. kuchukua muda mrefu kujichunguza wewe kwanza kabla hujaanza kumchunguza yeye na kuangalia udhaifu wake.

Tumemuona mara kadhaa Gwajima akisimama kuzungumza anachoamini pasipo kuuma uma maneno. Tumwona akimsema Laiyekuwa Rais wa Awamu iliyopita, tulimwona akisema Serikali iyopita kwa Ujasiri na kupelekea kupata matatizo kadhaa. Hakuishia hapo tu. aliwasema hata Viongozi wengine ambao aliamini walikengeuka kwa sababu moja au nyingine pasipo hofu kuwa nao wana jamii kubwa na yenye nguvu nyuma yao. Miaka ya nyuma alikuwepo Mchungaji Mtikila. huyu alikuwa na Roho hii pia miaka hiyo. alizungumza alichoamini pasipo kujali jamii kubwa inayomzunguka ina aamini nini.

Kuna haja ya Kujua Mchungaji Gwajima ni nani? ametokea wapi, ameishi katika mazingira gani, anaamini nini, ana elimu gani na kwa nini anajiamini.

tukifaham historia ya gwajima tutajiuliza ni kwa nini alitajwa kwenye uhusika wa kuuza au kujihusisha na madawa ya kulevya? alijiamini nini kusema kuwa akipimwa hata akikutwa ana kemikali za sigara/tumbaku au pombe iitwe ni madawa ya kulevya? wakati wa kupimwa walikuwepo akina nani?

habari zote kuwahusu viongozi mbalimbali au data zao na ujasili alio nao anaupata wapi? watu wa namna hii huongea yale ambayo wengine hawawezi kuongea. huamini kuwa wao ni chachu katika jamii fulani kwa maana ya kuwa wana mchango mkubwa sana. Ukienda kanisani kwa Gwajiama ana waumini wasomi, wasio na elimu dunia kubwa, walio na elimu dunia kubwa,matajiri na maskini. ukiacha waumini wa kanisani kwake. kuna ambao si waumini wa imani yake ila ni watu wanaoamini msimamo wake. na msimamo wa gwajima ni msimamo wa nyundo. hii ni karba au hulka ya watu ambao wao huamini katika kugonga kila amabcho kitakuwa kimewekwa chini yao. gwajima ni nyundo.

Gwajima huwezi ku dela naye kwa vitisho. unahitaji ku deal naye kwa hekima sana na maarifa. unapomtisha yeye huongeza mapambano. huyu ni aina ya watu ambao unaweza ukadhani ni wadogo sana lakini wana ushawishi fulan katika jamii. penda usipende wapo watu wa namna hii.

ni mzinzi mmoja hivi, kakamata akili na mnymbu wengi
 
Mchungaji gani anatembea na wake za watu na kuaribu ndoa? arafu eti wafuasi wake wanaenda kufunga pingu za maisha kwake,tafakalini!
Wewe ndio ulikuwa unashika dudu la Gwajima kulichomeka kwa mke wa mtu? Au upo single ulitaka akukongoli wewe?
 
Hiyo namba 5. Anategemea kununua ndege kwa biashara gani?[emoji23] ndege wanamchangia maskini na matajiri wanaosali kwake, yeye anakula bata waumini wanaishi kwa Shida tena wanabudu wakiwa juani, binadamu bhana
Gwajima kwa hulka yake hawezi kua mtumishi wa Mungu ( ni mtazamo wangu na Mungu anisamehe kwa kutenda kosa la kumhukumu mtu)
Mtumishi wa mungu atakula madhabahuni kwake....imeandikwa.
Ila akila Gwajima mnachukia??
Sasa kwa taarifa yako...watumishi wa mungu hapa duniani wanamiliki mindege ya kifahari...Gwajima kachelewa tu...
Tumuombee
 
Mchungaji gani anatembea na wake za watu na kuaribu ndoa? arafu eti wafuasi wake wanaenda kufunga pingu za maisha kwake,tafakalini!
Usituhamishe kwenye hoja ubuyu huo ulishapita tangu enzi za akina mbasha.....

Mwambie Bashite aweke Vyeti mezani kwanza
 
Back
Top Bottom