Mchungaji Kimaro: Afrika itakuwa ya kwanza kupona Corona itafuatiwa na Asia na wa mwisho watakuwa Israel (Wazungu)

Mchungaji Kimaro: Afrika itakuwa ya kwanza kupona Corona itafuatiwa na Asia na wa mwisho watakuwa Israel (Wazungu)

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mchungaji wa KKKT Kijitonyama Dr Kimaro amesema kwa mujibu wa maandiko ya Biblia Mungu alishaitangazia uponyaji wa kwanza Afrika yanapotokea maradhi ya kiulimwengu kama Corona.

Hivyo kwa mujibu wa Biblia Afrika itapona ya kwanza, itafuatiwa na Asia na mwisho watakuwa Israel kwa maana ya wazungu wa Ulaya na Marekani amesema mchungaji.

Mchungaji Kimaro amefanya maombi maalumu ya kuliepusha taifa kutoka janga la Corona na ameahidi Tanzania itakuwa kimbilio la dunia nzima kwani hata sayansi inaitambua Tanzania kama ni nchi na ardhi aliyoishi binadamu wa kwanza katika uso wa dunia.

Source: Upendo TV

Nawatakia Dominica yenye baraka!
 
Binadamu wa kwanza si Adam huyo mchungaji nani alimpotosha ya kwamba mwanadamu wa kwanza aliishi Tanzania??


Nawe nani kakupotosha kwamba binadamu (mtu) wa kwanza kuwepo duniani ni Adamu???
 
2685904_82995883-F775-47B2-BF36-898BFF6BEB65.jpeg
 
Hii ndio bongo yenye uongo mwingi na unafiki uliopitiliza
 
Mchungaji wa KKKT Kijitonyama Dr Kimaro amesema kwa mujibu wa maandiko ya Biblia Mungu alishaitangazia uponyaji wa kwanza Afrika yanapotokea maradhi ya kiulimwengu kama Corona...
Usiwe kigeu geu.
Kuna post umesema Waafrika hawafi kwa corona ambayo ni mafua tu.
Sasa nini kimekugeuza kuamini kuwa Kimaro anatabiri ukweli?
 
Back
Top Bottom