Mchungaji Kimaro: Matajiri ndio Walimzika Yesu, akina Petro na wenzake waliokula bure miaka 3 walimkimbia!

Lete andiko!
 

Ashaanza kulewa sifa, mapinduzi makubwa katika kitabu cha matendo na uzihirisho wa roho Mtakatifu walifanya matajiri? Shida ni jina Kimaro.
 
Iñjili ya huyu jamaa aisee...
Halafu eti ni rahisi ngamia 🐫 kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa mbingu
Ufalme wa mbingu ni stori za kusadika,,,na ndio hizo zinawapumbaza watu waendelee kuishi kizembe huku hao wanao yahubiri hayo wakiendelea kula mema ya dunia hii,,Ishi sasa kadri uwezavyo,,, Habari za kusadikika utakutana nazo huko huko,,,(mbere kwa mbere)in Magu's Voisi!!
 
Ndio haao waliosemwa kuuona ufalme wa Mungu ni Bora ngamia apenye Tundu la sindano?

Ndio hao walimtetea Kimaro baada ya uonevu wa Malasusa, wakaweka mabango mitaani. Ana Kila sababu ya kusema hivyo
 
Ndio haao waliosemwa kuuona ufalme wa Mungu ni Bora ngamia apenye Tundu la sindano?

Ndio hao walimtetea Kimaro baada ya uonevu wa Malasusa, wakaweka mabango mitaani. Ana Kila sababu ya kusema hivyo
Huyu jamaa hafai,sisi padri katuambia aliyepeleka habari za kufufuka Yesu aliyekuwa anajulikana Kama kahaba,Maria Magdalena ndio alikuwa wa kwanza kusambaza habari za ufufuko wa Yesu,so hata nasi tusijione wanyonge pamoja na madhaifu yetu tukitubu tunaanza upya na kuwa wasambazaji injili waziri🙏wajumbe wa Mungu,yeye kimaro anawasujudu matajiri na kuwadharau watunza makaburi🤔kila mmoja ana nafasi yake,moyo wake umejaa tamaa ya mali na amepotoka.
 
Unaweza kututhibitishia kuwa hizo ni habari za kusadikika? Nifafanulie hilo ili niijue kweli
 
Ndio maana sisali tena. Pale.

Jamaa anapotosha mandiiko.

Petro ndio msiingi wa kanisa. Na hakua tajiri.

Hiyo ya Arimathaya ni sadaka kama nyingine tu.

Hapo kijito washarika wana pesa na wanamhudumia hivyo lazima awapaishe.
 
Yusuf alikua mwanafunz wa YESU kwa siri!! Mambo haya watu wanayachukulia kirahis san, kama ni msomaji na muelewa wa Bible imeweka wazi pia ukiangalia kuanzia YESU kukamatwa kwake, kusulubiwa, kufa na kufufuka kila tukio lilikua na muhusika au wahusika. Mengine yalitokea ili maandiko yatimie, je bila yuda kumsaliti maandiko yangetimiaje? Je bila petro kumkana maandiko yangetimiaje? Baada ya Kristo kufa petro aliamua kurudi kupiga kaz yake ya uvuvi na jamaa zake, but ili ujue walio wake ni wake alivyofufuka alimrudia petro na kumpa majukumu ya kulisha kondoo wake... Kuanzia pale ilianza kupigwa injili ya kufa mtu hata sasa!!!
 
Nadhani Mch. Kimaro anaendelea kukosa umakini. Sijui sababu ni nini Mungu wangu. Mtumishi aliyeonekana kusimamia neno nakuwa hivi. Bwana Yesu lisema kuwa kuwa tajiri kunakuingiza katika risk kubwa sana (hataari) ya kutokuingia Mbinguni. Yesu alikosea? Pia kulinusuru kanisa wakati wa uhitaji ndio kuingia Mbinguni? Kama mtu hana nia ya kwenda Mbinguni hapo ni sawa. Toa pesa nyingi sana kusaidia watumishi, jenga majengo ya makanisa , n.k. tutakusifu sana naa itaisia hapo. Je ni kwamba mtu aliyeiba akawa tajiri akatoa sadaka kanisani sifa ya wizi inaondoka? Mwanasiasa mmoja hapa TZ aliwahi kuwashangaa wezi wanaojaribu kumhonga Mungu kwa kutoa sadaka pesa waliyochuma kwa wizi, rushwa na ufisadi. Kumbe wanatiwa moyo na mahubiri kama haya. Kweli Mch. Kimaro umeniangusha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…