Mchungaji wa Kanisa anaposimama katika madhabahu ya Mungu YAHWEH Kanisani ameitwa kuhubiri Neno la Mungu tu. Anapoingia kufundisha falsafa zake hata kama zinampendeza sana Mwanadamu, Mchungaji huyo anakuwa amejiodoa kiwa mtumishi wa Kristo: "Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine... Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe...Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo"
(Wagalatia 1:6;8;10).