Mchungaji maarufu barani Afrika, Bushiri atoroka nchini Afrika Kusini baada ya kuachiwa kwa dhamana

Mchungaji maarufu barani Afrika, Bushiri atoroka nchini Afrika Kusini baada ya kuachiwa kwa dhamana

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Mchungaji maarufu barani Afrika, Bushiri ametoroka nchini Afrika kusini baada ya kuachiwa kwa dhamana mapema mwezi huu kwa kushtakiwa kwa utapeli na utakatishaji fedha.

Mchungaji Bushiri, ambaye amesema kuwa anataka kusafisha jina lake, amerejea katika nchi yake, Malawi, akiwa na mke wake Mary na kusema kuwa kulikuwa na majaribio kadhaa ya kutishia maisha yake na mamlaka ya Afrika Kusini haikutoa ulinzi wowote kwake.

Kupitia mitandao ya kijamii mchungaji Bushiri amesema kukwepa dhamana ni njia ya busara ya kulinda maisha yake huku kukiwa kuna maswali ni namna gani mchungaji huyo ameweza kutoroka Afrika Kusini na kurudi kwao na kama mataifa hayo mawili yatashirikiana kumkamata na kumrejesha Afrika Kusini asikilize kesi yake.
Aidha yapo madai kuwa Bushiri alitoroka na ndege ya rais wa Malawi, Lazarus Chikwera, lakini ofisi ya Rais wa Malawi ulikanusha madai hayo lakini Waziri wa Mambo ya Nje nchini Malawi, Eisenhower Mkaka atahusishwa katika suala hilo.

Naye Waziri wa sheria wa Afrika Kusini, Ronald Lamola ameweka wazi kuwa serikali nchini humo haitasita kufuatilia suala hilo.

Bushiri nyuma yake kuna watu wanamtumia kama mtambo wa kutakatisha fedha.
 
Dah! Kama ni kweli hii kitu itakuwa ni pigo sana kwa kanisa.
 
Lissu alikimbia kesi 5 kisutu + jaribio la kuuliwa na mashine za mauaji za Jiwe
Lissu ana haki ya kuondoka nchini. Kama ameshambuliwa na wasiojulikana na bado hakuna uchunguzi wowote. Na baada ya uchaguzi tu, akaondolewa ulinzi afanyeje?

Kesi zinazomkabilili ni za uchochezi na ziko sita Kisutu
 
Bushiri is no more than a FRAUDSTER money LAUNDERER....

He has been using people's insanity to become a MILLIONARE...

How come sane minds believe that the DEAD could be RISEN?!!! 😂😂😂

He is in BAIL yet he traveled back to his home country....let Malawi authority EXTRADITE him back so as he can face LEGAL CHARGES....

WAAFRIKA TUAMKE NA HAWA WACHUMIA TUMBO!!!

MAENDELEO HAYANA VYAMA
 
Dah,kama ni kweli hii kitu itakuwa ni pigo sana kanisa...
Ni kweli. Rumors are alitoroka na msafara wa Rais wa Malawi. Hapo ni kwamba alitembeza mkwanja mnene kwa watu wengi.

Inashangaza sana huyu self-procraimed ‘prophet’ kukimbia kesi. Hawa ndio wale kutwa kucha wanawashauri waumini wao kununua the so called mafuta ya upako, maji ya upako, leso za upako etc ili washinde kesi ilhali wao wanahire best lawyers kwenye kesi na ikibidi wanakimbia kama hivi
 
😂😂😂

"Mafuta" kwa waumini tu....
 
huku kukiwa kuna maswali ....kama mataifa hayo mawili yatashirikiana kumkamata na kumrejesha Afrika Kusini asikilize kesi yake
Kama kuna maswali basi tafuta majibu uweke kwenye taarifa yako kama je, Malawi na SAfrika wana extradition treaty. Ripoti yeyote duniani ya suala la mtuhumiwa aliyetoroka nchi lazima igusie suala hilo.
 
😂😂😂

"Mafuta" kwa waumini tu....
Kweli kabisa, uliona wapi mchungaji akitaka kujenga kanisa au kuliboresha akiyumia mafuta ya upako tu ? Angalia hata wakitaka kununua magari kama watafanya maombi peke yake ,ni lzima waumini wachange kumnunulia tu.
 
😂😂
Kuna siku nilimuambia mtu mmoja kuwa kama Mwenyezi Mungu Angewapa nguvu zaidi ya walizonazo "hawa watu wa imani zote" basi wangezuia TAFITI NA SAYANSI kiasi kwamba tusingekuwa na INTERNET wala NDEGE duniani....

Wangesema ni haramu...tutumie tu "MAFUTA" ili tupate mavuno mashambani mwetu ,tule na TUSUBIRI kwenda MBINGUNI....😂😂😂
 
Bushiri msanii sana, hana tofauti na Gwajima. ukichanganya na ufala wa waafrika basi inakuwa burudani sana. Gwajima eti alifufua mtu!? Bushiri nae eti kaweka vikaratasi moto ukawaka?!.

Afrika bado tuko wajinga kama wanyama tu.
 
Mtumishi aheshimu mamlaka na arudi akajitetee mahakamani maana kukimbia ni kulitelekeza kanisa na waumini wake.
 
Ni kweli. Rumors are alitoroka na msafara wa Rais wa Malawi. Hapo ni kwamba alitembeza mkwanja mnene kwa watu wengi.

Inashangaza sana huyu self-procraimed ‘prophet’ kukimbia kesi. Hawa ndio wale kutwa kucha wanawashauri waumini wao kununua the so called mafuta ya upako, maji ya upako, leso za upako etc ili washinde kesi ilhali wao wanahire best lawyers kwenye kesi na ikibidi wanakimbia kama hivi
Mkuu umesahau kuwa mchungaji akitaka kujenga utaskia sadaka kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mchungaji, akitaka gari utasikia sadaka kwa ajili ya gari la mchungaji. Ila utaskiamchungaji aiwambia waumini, waje awaombee wale wanaotaka kununua magari mwaka huu au wanaotaka kujenga mwaka huu.

Akili yetu tunaijua wenyewe.
 
Back
Top Bottom