Mchungaji Mashimo, amuomba Rais Samia awalipie deni la Milioni 20, Simba na Yanga ili washinde CAF

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mchungaji Komando Mashimo amemuomba Rais Samia awalipie deni Simba na Yanga ili waweze kushinda katika michuano ya CAF. Mashimo amesema mwaka 2022 Mungu alitenda kwa ajili ya simba na yanga lakini hawakumtolea mungu walichoahidi ambacho ni kiasi cha Tsh milioni 20.

Amesema sadaka hiyo itatumika kufuta makosa ambayo Simba na Yanga wameyafanya mbele ya Mungu. Ambapo wasipotoa sadaka hiyo hawataweza kushinda kwenye michuano ya CAF mbali na fedha ambazo Rais ameahidi kwa kila goli katika michuano hiyo.

Mchungaji Mashimo amekuwa ni mtu wa kuziombea timu kushinda na kuwadai washabiki sadaka. Mwaka 2022 aliziombea Simba ikashinda moja ya mechi zake na pia aliiombea Yanga ikashinda mechi, lakini hakupewa sadaka kwa ushindi huo.

Ieleweke kwamba timu hizo hazikuwa na makubaliano ya kumpa Mashimo chochote.

Your browser is not able to display this video.
 
Pumbafu sana
 
🤣🤣🤣🤣🤣 bila m.20 ya Mashimo ata mkazike watu uwanjani amshindi mechi🤣🤣🤣🤣 duuh!!!!
 
Huyu ndio mdhamini wa yule dada aliyekamatwa kwa kusambaza video chafu ?
 
Kwa hiyo hapo ameona shimo?
 
Daudi ana matatizo ya akili sana.
Sie tunamjua tangu akiwa askari wa Jiji (City) anadhulumu machinga anasali kanisa la TAG Ubungo Msewe.
Huyu hayuko sawa kiakili mpuuzeni.
Tunaweza kuweka mengi juu yake atakosa waumini.
Ameshasumbua sana watu kesi za uonevu akiwa polisi jamii (mgambo) kila juma na kesi pale kituo cha Mbezi Luisi Polisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…