Pre GE2025 Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426



View: https://www.youtube.com/live/-6K3ZpUpoB8


Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Peter Msigwa amesema kwamba Ushindi wa Sugu ulijaa makando kando na Mchezo Mchafu (Hakufafanua)

Ametangaza kukata rufaa kwenye Kamati Kuu ya Chama chake kupinga ushindi huo wa Sugu, bado haijajulikana kama Kamati Kuu ikiridhishwa na Madai yake nini kitatokea, Sugu atanyang'anywa Ushindi na kupewa Msigwa au Uchaguzi utarudiwa

Binafsi nampongeza Mchungaji huyu kwa uamuzi wake huu, maana hii ndio njia Sahihi iliyowekwa na Chama chake ya kudai haki.

Pia soma
- Kuelekea 2025 - Kumekucha: Mchungaji Msigwa amkataa John Mrema kuwa Msimamizi wa Uchaguzi Kanda ya Nyasa

- Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa

- Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa: Sikuingia CHADEMA kutafuta Vyeo bali Kuwatumikia Wananchi, nitaendelea kukitumikia chama Katika Jimbo lolote mtakalonihitaji!

- Mchungaji Msigwa asema Mliodhani nahama Chadema Mnajidanganya
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Peter Msigwa amesema kwamba Ushindi wa Sugu ulijaa makando kando na Mchezo Mchafu (Hakufafanua)

Ametangaza kukata rufaa kwenye Kamati Kuu ya Chama chake.

Binafsi nampongeza Mchungaji huyu kwa uamuzi wake huu, maana hii ndio njia Sahihi iliyowekwa na Chama chake ya kudai haki.
Hiki chama si demokrasia na maendeleo?
 
Namuona Mchungaji Msigwa nje ya CHADEMA. Hizo rufaa ni mwanzo wa safari yake kutoka CHADEMA. Kote atasema hajatendewa haki. Usiku ule na hotuba ile aliyoitoa, alisifiwa kwa political maturity aliyoionyesha. Nini tena kimempata? Anatafuta sababu na cha kusema akijiondoa CHADEMA..
 
Ulitegemea aeleweke?Wote hao vigeugeu na wanabadili rangi kama kinyonga.

Walimuita Marehemu Lowassa fisadi Papa wakapiga about turn na kumfanya mgombea Urais wa Ukawa.

Hao wakokuambia leo ni Jumatatu hakikisha kwa kuangalia kalenda.
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Peter Msigwa amesema kwamba Ushindi wa Sugu ulijaa makando kando na Mchezo Mchafu (Hakufafanua)
...
Ni AIBU kubwa kwa CHADEMA kumchagua Sugu badala ya Peter Msigwa. Hata mukiniambia kuwa Sugu alikuwa na fedha chafu na kagawa kwa wajumbe, fedha unapokea lakini kura unapiga kwa kutumia akili yako.

Naiombea hiyo rufaa ipite ili IWASAFISHE CHADEMA.

Unamuachaje mtu kama Msigwa ana madini, amenyooka, hanunuliki na ana VISION na kwenda kumpa kura mvuta bangi, mtu wa matusi, mvaa mlegezo??

Mimi SIYO CHADEMA ila you people ARE NOT SERIOUS!!

Kwa taarifa yenu, mukirudia makosa haya kwenye Ubunge wa Mbeya Mjini mkamismamisha SUGU 2025, JIMBO MNALIPOTEZA.

TULIA hakubaliki Mbeya ukiacha maeneo ya Uyole, Itezi, Igawilo na Iduda anakogawa hela na T-shirt. Lakini zile kata asilia za Mbeya Mjini yaani kuanzia Mwakibete hadi Iyunga, Sisimba, Mwansekwa Tulia Ackson si lolote.

Tafuteni mtu anayeuzika ila siyo SUGU
 
Maskini Msigwa akikata rufaa kupinga tajiri Sugu hawezi fanikiwa angekaa kimya tu

Chadema Toka kuanzisha kwake lilikuwa chama Cha wenye Pesa sio malofa Msigwa ashukuru kuwa alipenya

Lakini Chadema Toka kuaasisiwa kiliasisiwa na Matajiri Watupu na wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje

Lofa Msigwa aridhike tu na alichopata miaka hiyo

Chadema ni capitalist party sio socialist party chama Cha malofa na wanyonge

Ni vizuri na Lisu alijue Hilo ndio maana hakuna maskini awe Lisu au yeyote aweza kuwa mwenyekiti wa Chadema taifa
 
Ni AIBU kubwa kwa CHADEMA kumchagua Sugu badala ya Peter Msigwa. Hata mukiniambia kuwa Sugu alikuwa na fedha chafu na kagawa kwa wajumbe, fedha unapokea lakini kura unapiga kwa kutumia akili yako...
Uongozi ni kama mbio za kupokezana vijiti, yule Sugu unayemzungumzia wewe si huyu wa leo, hata hivyo hatuwezi kuzuia Msigwa kukata rufaa kwenye Chama maana huko ndiko katiba inaelekeza.

Hata hivyo napinga dharau zako kwa Sugu kwa vile hazina tija, Hospitali nyingi za Mbeya zilifanyiwa marekebisho kwa ushawishi wa Sugu kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Ulisubisya, yaani Sugu kamkalisha Mpoki chini na kumueleza umuhimu wa kuboresha Hospitali ya Rufaa na Ile ya Meta (Martenity Hospital) zinazohudumia Mkoa wa Mbeya na Mpoki akafanya mchakato, sasa hata akivaa mlegezo lakini akatufanyia haya shida iko wapi?
 
Kabla kusikiliza hiyo rufaa kamati ya nidhamu ya Chadema imuite na imhoji mchungaji Msigwa Kwa Nini aliita vyombo vya habari kusema atakata rufaa?

Kwani taratibu kichama si angeweza kata rufaa moja Kwa moja bila kuita vyombo vya habari

Kwani ndivyo katiba ya Chadema ndivyo inavyosema kuwa mtu akitaka kukata rufaa ndani ya chama lazima apitie kwanza kwenye vyombo vya habari Kwa kuitisha press conference?
 
Namuona Mchungaji Msigwa nje ya CHADEMA. Hizo rufaa ni mwanzo wa safari yake kutoka CHADEMA. Kote atasema hajatendewa haki. Usiku ule na hotuba ile aliyoitoa, alisifiwa kwa political maturity aliyoionyesha. Nini tena kimempata? Anatafuta sababu na cha kusema akijiondoa CHADEMA..
Kuna Siri kubwa inaendelea Kati ya mchungaji Msigwa, Tundu Lisu na Lema 🐼
 
Back
Top Bottom