Pre GE2025 Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa atangaza kukata rufaa kupinga Ushindi wa Joseph Mbilinyi (Sugu) Kanda ya Nyasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kabla kusikiliza hiyo rufaa kamati ya nidhamu ya Chadema imuite na imhoji mchungaji Msigwa Kwa Nini aliita vyombo vya habari kusema atakata rufaa?
si sheria za chama zina mruhusu kukata rufaa. Tunaimba sana kuhusu demokaria, ila mchakato wake ukianza kelele lazima ziwe nyingi
 
Sidhani kama Chadema inaweza kuwaacha domant watu kama Msigwa watapewa post za teuzi, ninachokiona kuna watu wanaamini wao ndio wanastahili.

Itapendeza pia mtu kama Sugu aambiwe afanye kazi za chama alizoomba swala la ubunge wagombee watu wengine yeye asimamie mchakato wa kupata wagombea ubunge.
Chadema Wana Nafasi 4 tu za Uteuzi

Katibu mkuu, Naibu KM ( Tanganyika), Naibu KM( Zanzibar) na kile Cheo cha Jon Mrema
 
Hatutaki Hustler wa kushinda vijiweni na masela. Tunataka mbunge anayeweza kuleta maendeleo.

Leteni hata yule Mwakajoka basi
Sugu hatakiwi kutogombea ubunge kwa sababu ya chuki zako kwake, bali hapaswi kugombea ubunge maana yeye ndio kiongozi wa kanda na anapaswa kuhakikisha chama kinafanya vizuri kanda hiyo.

Hatutaki watu wenye kuhodhi madaraka watu wenye uwezo wa kibunge wapo yeye akae pembeni na Msigwa asubiri kutupa karata yake kwenye ubunge.
 
Matatizo mengine CHADEMA huwa mnajitafutia wenyewe tu, mlitakiwa muwe na wenyeviti wa chama mkoa halafu uwenyekiti wa kanda unakuwa unapokezanwa kwa hao wenyeviti kwa mkoa labda kwa miaka miwili miwili.
 
Sugu hatakiwi kutogombea ubunge kwa sababu ya chuki zako kwake, bali hapaswi kugombea ubunge maana yeye ndio kiongozi wa kanda na anapaswa kuhakikisha chama kinafanya vizuri kanda hiyo.

Hatutaki watu wenye kuhodhi madaraka watu wenye uwezo wa kibunge wapo yeye akae pembeni na Msigwa asubiri kutupa karata yake kwenye ubunge.
Kwa sasa Mchungaji Msigwa atapata ugumu kugombea ubunge Iringa kwa sababu ya Vita baridi Kati yake na Mwenyekiti wa Mkoa Bilionea Mungai

Ni Mungai Ndiye kasababisha Sugu ashinde Kanda
 
Namuona Mchungaji Msigwa nje ya CHADEMA. Hizo rufaa ni mwanzo wa safari yake kutoka CHADEMA. Kote atasema hajatendewa haki. Usiku ule na hotuba ile aliyoitoa, alisifiwa kwa political maturity aliyoionyesha. Nini tena kimempata? Anatafuta sababu na cha kusema akijiondoa CHADEMA..
Anajiondoa, sababu ndio hii kishapata.
 
Uhuru wa kuongea kwa Chadema ni jambo la kwanza, hakuna anayezuiliwa kuongea atakacho na hasa kwenye masuala ya Haki na Demokrasia
Katiba ya Chadema inatakiwa kuzingatiwa kama hamjui kuendesha chama mkodi watu kutoka CCM wawasaidie uchaguzi ndani ya Chadema ni suala la kikatiba kukata rufaa sio kitu Cha kwenda kwenye vyombo vya habari
 
Kwa sasa Mchungaji Msigwa atapata ugumu kugombea ubunge Iringa kwa sababu ya Vita baridi Kati yake na Mwenyekiti wa Mkoa Bilionea Mungai

Ni Mungai Ndiye kasababisha Sugu ashinde Kanda
Mungai usimsingizie hayo mambo yako, kwenye Kanda Mungai alipiga kura moja tu ambayo ni yake.
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Peter Msigwa amesema kwamba Ushindi wa Sugu ulijaa makando kando na Mchezo Mchafu (Hakufafanua)

Ametangaza kukata rufaa kwenye Kamati Kuu ya Chama chake kupinga ushindi huo wa Sugu, bado haijajulikana kama Kamati Kuu ikiridhishwa na Madai yake nini kitatokea, Sugu atanyang'anywa Ushindi na kupewa Msigwa au Uchaguzi utarudiwa

Binafsi nampongeza Mchungaji huyu kwa uamuzi wake huu, maana hii ndio njia Sahihi iliyowekwa na Chama chake ya kudai haki.

Pia soma

Vitu vingine haviingii akilini kwenye uchaguzi Kuna kushinda na kushindwa mchungaji msigwa Hana budi kupumzika
 
Back
Top Bottom