Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Ningependa Tundu Lissu ashinde Uenyekiti CHADEMA kwa faida ya demokrasia ya Tanzania na hata kwa CCM yenyewe

Pre GE2025 Mchungaji Msigwa: Ningependa Tundu Lissu ashinde Uenyekiti CHADEMA kwa faida ya demokrasia ya Tanzania na hata kwa CCM yenyewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mchungaji Msigwa ameeleza wazi kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu katika kinyang’anyiro cha Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Akizungumza kuhusu mwelekeo wa uchaguzi huo, amesema:

"Mimi nam-support Tundu Lissu, ningependa ashinde, lakini ni matatizo yao hayo. Mimi, yeyote atakayeshinda yaani sisi (CCM) tunataka chama kile tukishinde. Yeyote atakayeshinda bado tutakabiliana naye, awe Lissu, awe Mbowe, au mtu mwingine kutoka Burundi, Rwanda. Lakini kwa kuwa mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi, nitakabiliana na yeyote. Hata hivyo, kwa faida ya demokrasia ya Tanzania na hata kwa faida ya CCM yenyewe, anayepaswa kuwa Mwenyekiti pale ni Lissu."
Soma, Pia: Tundu Lissu: Mchungaji Peter Msigwa ni rafiki yangu, lakini nitamkabili Kisiasa
 
Mchungaji Msigwa ameweka wazi msimamo wake kwa Tundu Lissu kuelekea Uchaguzi wa ndani wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA) ambapo amesema "Ningependa Tundu Lissu ashinde"
Masikini huyu yuko huko kama mateka moyo wake wote bado uko Chadema na kwa vile mgomvi wake alikuwa Mbowe na anaona kuna kila dalili Mbowe kupigwa chini anatamani sana kurudi ila anaogopa tu kutekwa .
 

Attachments

  • 5852875-b2d46096282c702ae9acbe27b26cfaa2.mp4
    1.3 MB
  • 5798904-1fa5b9f4fe7a36a353fd0342c9e2b57.mp4
    2.9 MB
Masikini huyu yuko huko kama mateka moyo wake wote bado uko Chadema na kwa vile mgomvi wake alikuwa Mbowe na anaona kuna kila dalili Mbowe kupigwa chini anatamani sana kurudi ila anaogopa tu kutekwa .
Arudi tena? Halafu atasemaje
 
Mwashambwa ni CHADEMA???Choice Variable ni Chadema???
Shida yenu mnapenda majibu mepesi kwa maswali magumu.Tangu lini mfuasi wa dhati wa Chadema atakubali ushauri wa hao wawili kuhusu nani anastahili kupigiwa kura?

Wao kwa kumpigia debe Mbowe wanajenga hisia kuwa Mbowe ni kibaraka wa CCM hivyo kuwafanya watu wampigie kura Lissu.

Msigwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu kila mtu anajua anavyomchukia Mbowe.

Bahati mbaya wako watakaoingia mkenge na kumpigia kura Lissu ambae CCM wanamtaka. Lengo lao ni Lissu ashinde halafu Mbowe asuse. Ikitokea hivyo CDM itakuwa ICU by the time Uchaguzi Mkuu unafanyika.

Amandla...
 
Back
Top Bottom