milele amina
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 6,045
- 8,080
Huko CCM siku zako zinahesabika!
Hujaielewa CCM vizuri
Hujaielewa CCM vizuri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
huyu ccm haitakiwi kumwamini.labda wampe ubaloziMchungaji Msigwa ameeleza wazi kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu katika kinyang’anyiro cha Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Akizungumza kuhusu mwelekeo wa uchaguzi huo, amesema:
"Mimi nam-support Tundu Lissu, ningependa ashinde, lakini ni matatizo yao hayo. Mimi, yeyote atakayeshinda yaani sisi (CCM) tunataka chama kile tukishinde. Yeyote atakayeshinda bado tutakabiliana naye, awe Lissu, awe Mbowe, au mtu mwingine kutoka Burundi, Rwanda. Lakini kwa kuwa mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi, nitakabiliana na yeyote. Hata hivyo, kwa faida ya demokrasia ya Tanzania na hata kwa faida ya CCM yenyewe, anayepaswa kuwa Mwenyekiti pale ni Lissu."
Soma, Pia: Tundu Lissu: Mchungaji Peter Msigwa ni rafiki yangu, lakini nitamkabili Kisiasa
Huo ni mkakati wa TISS kumweka Mbowe CHADEMA ifeNa ndiyo maana CCM wamewekeza nguvu kubwa ya fedha na manpower ili hilo litokee,masikini Mbowe anafikiri anapendwa sana na Samia kumbe anakaangwa kwa mafuta yake mwenyewe. Samia anajua Chadema ikisambaratika huko CCM hawana cha kumtishia tena .
MamaSamiah,Tlahtlah ni CHADEMA?Shida yenu mnapenda majibu mepesi kwa maswali magumu.Tangu lini mfuasi wa dhati wa Chadema atakubali ushauri wa hao wawili kuhusu nani anastahili kupigiwa kura?
Wao kwa kumpigia debe Mbowe wanajenga hisia kuwa Mbowe ni kibaraka wa CCM hivyo kuwafanya watu wampigie kura Lissu.
Msigwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu kila mtu anajua anavyomchukia Mbowe.
Bahati mbaya wako watakaoingia mkenge na kumpigia kura Lissu ambae CCM wanamtaka. Lengo lao ni Lissu ashinde halafu Mbowe asuse. Ikitokea hivyo CDM itakuwa ICU by the time Uchaguzi Mkuu unafanyika.
Amandla...
Na darasa lake la saba awe balozihuyu ccm haitakiwi kumwamini.labda wampe ubalozi
Katika Mambo ya Walawi 11:7-8 na Kumbukumbu la Torati 14:8, Mungu aliwaambia Waisraeli kuwa nguruwe ni najisi kwa sababu hula nyama lakini hawatafuni cud (chakula mara ya pili). Hivyo, Waisraeli walikatazwa kula nyama ya nguruwe au kugusa mizoga yake. Hili lilikuwa sehemu ya sheria ya Musa, ambayo iliwaongoza Waisraeli jinsi ya kuishi kwa usafi wa mwili na kiroho.Angalia hii nguruwe ya kijani nayo
Hajasema kwa upande wa CCM anapenda nani awe makamu mwenyekiti?Mchungaji Msigwa ameeleza wazi kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu katika kinyang’anyiro cha Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Akizungumza kuhusu mwelekeo wa uchaguzi huo, amesema:
"Mimi nam-support Tundu Lissu, ningependa ashinde, lakini ni matatizo yao hayo. Mimi, yeyote atakayeshinda yaani sisi (CCM) tunataka chama kile tukishinde. Yeyote atakayeshinda bado tutakabiliana naye, awe Lissu, awe Mbowe, au mtu mwingine kutoka Burundi, Rwanda. Lakini kwa kuwa mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi, nitakabiliana na yeyote. Hata hivyo, kwa faida ya demokrasia ya Tanzania na hata kwa faida ya CCM yenyewe, anayepaswa kuwa Mwenyekiti pale ni Lissu."
Soma, Pia: Tundu Lissu: Mchungaji Peter Msigwa ni rafiki yangu, lakini nitamkabili Kisiasa
Sio Mbowe tena ?...CCM inataka Lissu ashinde.
Amandla...
Ndio maana nasema mnapenda majibu mepesi kwa maswali magumu. Unadhani watu watampigia kura Mbowe katika uchaguzi wa CHADEMA kwa sababu hao wanampigia debe? Au ndio wataona ni uthibitisho kuwa Mbowe ni mamluki wa CCM na hivyo watampigia kura Lissu?MamaSamiah,Tlahtlah ni CHADEMA?
Hata siku moja Mkuu. Lissu akiwa Mwenyekiti CCM watakuwa na kazi rahisi. Kama atatekeleza anayosema, atasusa chaguzi na hivyo kuwapa CCM na vyama vingine ushindi wa kirahisi. Atakataa majadiliano wakati vyama vingine vitaendelea nayo na hivyo kuifanya CHADEMA ionekane un reasonable hasa kwa taasisi na nchi za nje zenye interest na utulivu nchini. Aidha, Lissu ataitisha maandamano kitu ambacho serikali ina uzoefu mkubwa wa kuyanyima pumzi. Wazuie wakubwa kutoka nyumbani kwao, tangaza kuwa jeshi linafanya usafi siku hiyo, Tanpol itangaze kuwa ni haramu na wasilaumiwe kwa yatakayowapata watakaoandama. Maandamano yasipofanikiwa mara kadhaa CDM watabaki kulaumiana tu na kutafuta wachawi.Sio Mbowe tena ?...
Tuondolee upuuzi wako wa kiccm hapaKatika Mambo ya Walawi 11:7-8 na Kumbukumbu la Torati 14:8, Mungu aliwaambia Waisraeli kuwa nguruwe ni najisi kwa sababu hula nyama lakini hawatafuni cud (chakula mara ya pili). Hivyo, Waisraeli walikatazwa kula nyama ya nguruwe au kugusa mizoga yake. Hili lilikuwa sehemu ya sheria ya Musa, ambayo iliwaongoza Waisraeli jinsi ya kuishi kwa usafi wa mwili na kiroho.
Anaogopa kutekwa na kulawitiwa.Jamaa anatamani kurudi lakini anaogopa kusema.
Mchungaji anakiri, anataman kuona Siku Moja Brain ya LISSU inatumika Kwa faida ya Taifa.
Anakiri LISSU ni mwenye Akili kubwa, Msomi,mwenye maarifa mengi mno, ana Uelewa mpana wa mambo mengi.
Anakiri, LISSU ni Moja ya watu wachache Wanaozaliwa na kipawa hiko.
View: https://youtu.be/fBHarISl_Fk?si=yeDFOWKsk48pl5xd
Hahaha 😆kwa faida ya demokrasia ya Tanzania na hata kwa faida ya CCM yenyewe, anayepaswa kuwa Mwenyekiti pale ni Lissu