Naona baadhi wanapata shida sana kumuelewa Msigwa, binafsi namuona kapevuka sana kwenye ulingo wa siasa za kiushandani sio ndani ya Chadema alipo, bali kwenye siasa za Tanzania kiujumla.
Mara kadhaa Msigwa amekuwa akihusishwa na kutaka kwenda CCM, ukitazama wanaomhusisha na hizo tuhuma wengi ni walaini kwenye siasa za kiushandani, wanaoogopa malumbano ndani ya taasisi hata kama mwisho wa siku ndio yanazidi kuijenga taasisi husika.
Mfano, Msigwa kusema hakuridhishwa na namna mshindi alivyopatikana kwenye uchaguzi wa kanda ya Nyasa hivi karibuni hivyo kuamua kukata rufaa, ajabu wengi wanaona hiyo ni njia yake ya kuelekea CCM, hawaoni kama hiyo ni njia yake ya kudai haki yake anayoona amedhulumiwa kwenye ule uchaguzi!.
Ajabu zaidi wengine akiwemo MMM kuonekana kushangazwa na namna baadhi ya viongozi/wafuasi wa CCM wanavyoshangilia na kuonekana wapo upande wa Msigwa kwenye hiyo issue, kwao wanamuona Msigwa kama ana wafuasi ndani ya CCM.
Hawakumbuki CCM ni mshindani wao na lazima wakiona kuna dalili ya mgogoro ndani ya Chadema, waitumie nafasi kuukuza kwa kuchukua upande mmoja wa aliye kwenye huo mgogoro, hawa wanadhani kuna siku CCM itasema mazuri ya Chadema, hawajiulizi mbona CCM hawaripoti anayosema Msigwa akiwa na Lissu kwenye mkutano wao huko Singida?
Kwa akili zao mbovu wao ndio wanaamua kuukuza zaidi mgogoro na kuipa ushindi CCM kwa kuanza kumpiga kwa mawe mwanachama mwenzao ndani ya Chadema, hawa simply hawajioni kama wameshaingia kwenye mtego wa CCM.
Licha ya kuwa kwao kwenye siasa za upinzani kwa muda mrefu, bado ni wachanga kwenye siasa za ushindani, siasa za nguvu ya hoja, wao wanataka mkiwa chama kimoja basi mfanane kila msimamo na kila jambo, tena kila wakati, kama maembe juu ya mti, Msigwa is above them all.
Wanataka kama Msigwa anaona amedhulumiwa haki yake anyamaze kimya, huo kwao ndio utii kwa chama na sio ujinga, hawa hawataki aitishe press conference, hiyo kwao ni dalili ya kuondoka Chadema kwa Msigwa na wala sio haki yake ya uhuru wa kutoa maoni yake kikatiba, wako negative tu ajabu wanajiita wana demokrasia!.
Iko siku watamuelewa Msigwa tu.