Mchungaji Msigwa umetukosea heshima wanandugu kwa kushindwa kutambua mchango wa fedha za familia

Mchungaji Msigwa umetukosea heshima wanandugu kwa kushindwa kutambua mchango wa fedha za familia

Hizi movie hizi kweli ni za ajabu mpaka zinanifanya kufikiri mara nyingi sana.Inawezekanaje mtoe hukumu ya kumfunga Msigwa na wenzake, mkasimama kidete kwa hali na mali mpaka hukumu ikapita kama mlivyotaka mkahakikisha wamepelekwa Segerea.

Ghafla tu mkamtoa yule Msukuma.Mliposikia karibu Watanzania wengi wamechanga fedha za kuwatoa za kutosha na nyie mkaanza mchezo wa kuigiza,tena wa kitoto kwelikweli.

Unifunge halafu ujifanye mwema kuja kunitoa,ni kitu gani hicho wala sikuelewi.Mnachanganyikiwa mpaka mnafanya vitu vya ajabu.

Eti familia ya Kina Msigwa imechanga 2m peke yake.

Hivi kwa nini mnadharau watu hivi. kina Msigwa ni wa 2m.Halafu bila kuwa na aibu eti nayo Ikulu ni mmoja wa Familia.Hapa tunajiuliza,waliochanga 2m wamehifadhi majina yao aliyekuja na vioja kwa nguvu kubwa amechorwa kila mahali.Uongo mwingine haujifichi.Haya Kina Msigwa wamesema familia haijachanga 2m.huyo amepata wapi hiyo figure.Kama sio kudhalilisha watu.

Huyu hapa kajipachika jina tu la Msigwa kumbe hata hajulikani.Hawa ni walewale wamezoelekaga.Ukija kimbelembele yupo,kinyumanyuma pia yupo basi tena.

Wenye misimamo yao wapo.Kina Mch.Peter na sio wewe bendera fuata upepo.Hata wewe usipokuwepo Mch.Mambo yake yanenda tu.Kwanza nina hakika wewe hukuchanga chochote unapiga kelele tu hapa.
Aliyekulisha sumu ndiye aje akunyweshe maziwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulimuona siku Magu alipotembelea Iringa alivyokuwa anamsifia?

Ni haki yake kumsifia, maana hiki ni kipindi cha mavuno ya hela za Mabwege wanaolazimisha kupendwa
 
Ni haki yake kumsifia, maana hiki ni kipindi cha mavuno ya hela za Mabwege wanaolazimisha kupendwa
Kuna siku utaaibika sana kama mlivyoaabika kwa Lowassa, Mashinji, na Sumaye na ni mwaka huu huu!!
 
Tukiachana na maswali ya kupuuzwa ya mtoa Mada yasiyo na tija kwa taifa...
Serikali ituambie kwanini pesa za serikali zinatumika kwenye masuala ya kumtoa mwanafamilia jela?
Tumeona magari ya serikali yenye mafuta ya kodi zetu yanatumika kwenda segerea kwa msigwa,hii ni kwasababu gani??
Je,hii siyo kesi ya kutumia ofisi vibaya kwa kujinufaisha binafsi?
Je, hii sio rushwa kutaka kumpata Msigwa aingie chama chao?
Je huu sio uhujumu uchumi?
Huu sio ubinafsi mkubwa ukizingatia wapo watanzania wameteseka na kuomba msaada bila mafanikio?
Je, Haikuwa vema pesa hizi angesaidiwaga Tundu Lissu kuokoa maisha yake yalipokua yanakatishwa kinyama?
THIS IS A BIG SHAME...KARMA WILL TAKE ITS COURSE... YOU CAN CHEAT PEOPLE BUT YOU CANT CHEAT GOD...SAIDIA WENYE UHITAJI ZAIDI!!!
 
Kama kweli mlikiwa na nia njema mlitakiwa kupeleka huo mchango wenu Chadema na sio Lumumba. Acha kuchefua watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie wanafamilia wanafiki sana. Chama kilitoa utaratibu was kuchangia kwa kutoa account ya benki na nr ya M-Pesa. Ikawaje nyie mkaja na utaratibu tofauti? Mmeniudhi sana. Halafu iweje muende gerezani kumtoa mkiwa mmeongozana na yule vuvuzela Polepole ambaye si mwanafamilia? Ovyo kabisa!
 
Huwezi kuwa ndugu wa Msigwa na ukawa unatamani mabaya yamfike ndugu yako ili ukate kiu uliyonayo ikiwemo kufiwa.

Akifiwa Msigwa tafsiri yake ni kuwa umefiwa pia.
Je, unamjua atakayekufa ni nani kwako?

Acha hizo, siasa na familia ni mambo tofauti sana.

We all live once & die once.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msigwa kajisahau tu msameheni,mtakua nae bega kwa bega baada ya october 2020,akishaukosa ubunge
 
Nimemsikiliza kwa makini ndugu yangu PETER MSIGWA kwenye hotuba yake na vyombo vya habari ambapo yeye na viongozi wengine wa Chadema waliokuwa gerezani wameachiwa huru baada ya kulipa faini.

Kilichonishangaza ni MSIGWA kushindwa kutambua mchango wetu wa kifedha uliokuwa unaratibiwa na kaka yake, BERNET MSIGWA ambapo kwa ndugu wa huku Iringa tulifanikiwa kukusanya jumla ya milioni 2 na baadae alikwenda kuomba msaada kwa mwanafamilia mwenzetu Mhe. Rais JOHN MAGUFULI ambaye alijitolea sh. milioni 38.

MSIGWA kwa kutanguliza maslahi ya Chadema umeikana michango yetu wanandugu, eti kwa sababu wakati kaka yake BERNET anashughulika kukutoa gerezani aliambatana na POLEPOLE ambaye kutokana na Mhe. Rais kutingwa na Majukumu alimuagiza ashirikiane nae.

Ndugu yetu PETER kumbuka kuna maisha baada ya Siasa, kuna muda utastaafu Siasa, utapata misiba(japo siombei hilo)na hata kufariki dunia, sisi ndugu zako ndio tutakaowajibika kukusitiri na kusaidia familia utakayoiacha Chadema hawata kuwa na wewe tena.

Ni raia yangu utajitokeza kwa wanandugu kuomba msamaha juu ya jambo hilo, ikumbukwe kwa mila na desturi zetu za kihehe mafadhaiko uliyosababisha kwetu yanaweza kukusababishia laana ya kushindwa ubunge kwenye uchaguzi na kufukuzwa uanachama na Chadema.

Ndimi ndugu yako,
Luvanda Ngurusavangi Msigwa
Igumbilo, Iringa.

Familia mngeshirikiana na chama CHAKE ambacho kilishaweka utaratibu wa KUWATOA Viongozi wake,

Wakawaingia WENYE ROHO mbaya za uchonganishi na UCHOCHEZI kuwa ndugu yenu / yetu hawezi saidiwa na CHADEMA.

MLIPOONA MMEPATA MILIONI MBILI TU, MLIWASILIANA NA CHADEMA?

HATA MLIPOMWAMBIA MAGUFULI NA KUTOA HIZO PESA, MNGEWASILIANA NA CHAMA CHAKE NA KUWASILISHA MICHANGO YA FAMILIA KWA CHAMA CHAKE.

KUTOFAUTIANA VYAMA HAKUVUNJI UNDUGU,

KAMA MTAMTENGA AKISTAAFU SIASA MTAMWONEA.

AU MLIPEWA SHARTI KUWA HIYO PESA WASIIONE WA CHADEMA?

KAMA NI HIVYO, MNGEMWULIZA KWANZA MIPANGO ILIYOPO, MNGEELEKEZWA CHA KUFANYA.
 
Back
Top Bottom