Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
Nimemsikiliza kwa makini ndugu yangu PETER MSIGWA kwenye hotuba yake na vyombo vya habari ambapo yeye na viongozi wengine wa Chadema waliokuwa gerezani wameachiwa huru baada ya kulipa faini.
Kilichonishangaza ni MSIGWA kushindwa kutambua mchango wetu wa kifedha uliokuwa unaratibiwa na kaka yake, BERNET MSIGWA ambapo kwa ndugu wa huku Iringa tulifanikiwa kukusanya jumla ya milioni 2 na baadae alikwenda kuomba msaada kwa mwanafamilia mwenzetu Mhe. Rais JOHN MAGUFULI ambaye alijitolea sh. milioni 38.
MSIGWA kwa kutanguliza maslahi ya Chadema umeikana michango yetu wanandugu, eti kwa sababu wakati kaka yake BERNET anashughulika kukutoa gerezani aliambatana na POLEPOLE ambaye kutokana na Mhe. Rais kutingwa na Majukumu alimuagiza ashirikiane nae.
Ndugu yetu PETER kumbuka kuna maisha baada ya Siasa, kuna muda utastaafu Siasa, utapata misiba(japo siombei hilo)na hata kufariki dunia, sisi ndugu zako ndio tutakaowajibika kukusitiri na kusaidia familia utakayoiacha Chadema hawata kuwa na wewe tena.
Ni raia yangu utajitokeza kwa wanandugu kuomba msamaha juu ya jambo hilo, ikumbukwe kwa mila na desturi zetu za kihehe mafadhaiko uliyosababisha kwetu yanaweza kukusababishia laana ya kushindwa ubunge kwenye uchaguzi na kufukuzwa uanachama na Chadema.
Ndimi ndugu yako,
Luvanda Ngurusavangi Msigwa
Igumbilo, Iringa.
Acha kutumiwa na CCM, nawe elewa mambo ya Familia hayamalizwi kwenye JF. Namba yake ya simu unayo kwanini uandike hapa , hata kama limekukera.
Hata mimi leo nimekwazana na ndugu yangu, nimempigia simu na tumeyamaliza bila wewe kujua.
Msigwa kakubali kuwa kuna mahusiano ya kindugu na Magufuli, lakini mambo ya kifamilia anapenda yaishie katika Familia.
Hivyo msubiri huko Iringa au mfuate Dar mkamaliziane.
Angalizo: Usirudi tena hapa JF kwa swala la Kifamilia. Jifunze kitu katika hili.