Mchungaji Msigwa umetukosea heshima wanandugu kwa kushindwa kutambua mchango wa fedha za familia

Mchungaji Msigwa umetukosea heshima wanandugu kwa kushindwa kutambua mchango wa fedha za familia

Nimemsikiliza kwa makini ndugu yangu PETER MSIGWA kwenye hotuba yake na vyombo vya habari ambapo yeye na viongozi wengine wa Chadema waliokuwa gerezani wameachiwa huru baada ya kulipa faini.

Kilichonishangaza ni MSIGWA kushindwa kutambua mchango wetu wa kifedha uliokuwa unaratibiwa na kaka yake, BERNET MSIGWA ambapo kwa ndugu wa huku Iringa tulifanikiwa kukusanya jumla ya milioni 2 na baadae alikwenda kuomba msaada kwa mwanafamilia mwenzetu Mhe. Rais JOHN MAGUFULI ambaye alijitolea sh. milioni 38.

MSIGWA kwa kutanguliza maslahi ya Chadema umeikana michango yetu wanandugu, eti kwa sababu wakati kaka yake BERNET anashughulika kukutoa gerezani aliambatana na POLEPOLE ambaye kutokana na Mhe. Rais kutingwa na Majukumu alimuagiza ashirikiane nae.

Ndugu yetu PETER kumbuka kuna maisha baada ya Siasa, kuna muda utastaafu Siasa, utapata misiba(japo siombei hilo)na hata kufariki dunia, sisi ndugu zako ndio tutakaowajibika kukusitiri na kusaidia familia utakayoiacha Chadema hawata kuwa na wewe tena.

Ni raia yangu utajitokeza kwa wanandugu kuomba msamaha juu ya jambo hilo, ikumbukwe kwa mila na desturi zetu za kihehe mafadhaiko uliyosababisha kwetu yanaweza kukusababishia laana ya kushindwa ubunge kwenye uchaguzi na kufukuzwa uanachama na Chadema.

Ndimi ndugu yako,
Luvanda Ngurusavangi Msigwa
Igumbilo, Iringa.
Ndugu zake ni Wacongo sio sehemu ya Watanzania?
Mambo ya familia yatazungumzwa faragha Kwenye familia.
 
mimi naona kama shukrani alitakiwa aitoe kwenye familia na sio public, sasa mambo yenu ya kifamilia huku jf unayaleta ya nini? kwani wakati mnakaa kikao cha kumchangia mlikuja huku jf?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kuona Wahehe wanafiki kiasi hiki.
Wakati "mwanafamilia" mwenzenu anampeleka Mhe. Peter Msigwa mahabusu 'bila kosa' na kumpitisha Kisutu wakati anampeleka jela, Wanafamilia mlikuwa mmeziba masikio na kufumba macho?
Masononeko na mateso ya watoto wa Msigwa, na mama yao hamkuyaona?
Masononeko yenu yamejitokeza tu, baada ya Watanzania kumtoa jela?
Luvanda Ngurusavangi Msigwa, unajua kuwa kulipa faini maana yake ni kwamba Mhe. Peter Msigwa ametumikia kifungo?
Unajua kuwa kumbukumbu za kifungo ni doa chafu katika maisha yake?
Je, wanafamilia mnaandaa utaratibu gani kufuta hilo doa chafu?
Luvanda, wanafamilia mmejipangaje kuhakikisha kuwa mwamafamilia mwenzenu Mhe. Peter Msigwa anaendelea kupata haki yake ya kuongea na Watanzania waliompigia kura kuwa Mbunge ambazo zimenyakuliwa a "mwanafamilia mwenzenu aliyechangia milioni 38"?
Kinyume cha hapo, wewe Luvanga Ngurusavangi Msigwa utakuwa ni mshiriki wa utesaji wa Mhe. Peter Msigwa.
Mkuu umeongea sahihi, hata mimi nilishangaa saana kusikia eti mtu aliyewatengenezea kesi Msigwa na wenzake ghfla anageuka na kuwa ndigu wa familia ya Msigwa !!, hao wanaojita wanafamilia walisindwa nini kumuomba huyo Meko alekeze ile kesi ya kubambikiwa iondolewe mahakamani kama ili vyofanyika kwa yule askari aliyeua !!
 
Mkuu umeongea sahihi, hata mimi nilishangaa saana kusikia eti mtu aliyewatengenezea kesi Msigwa na wenzake ghfla anageuka na kuwa ndigu wa familia ya Msigwa !!, hao wanaojita wanafamilia walisindwa nini kumuomba huyo Meko alekeze ile kesi ya kubambikiwa iondolewe mahakamani kama ili vyofanyika kwa yule askari aliyeua !!
Umenena vema.
Askari aliyeua, tena kwa risasi, alifutiwa kesi na "mwanafamilia aliyechangia milioni 38" lakini akaamua kumpeleka jela 'mwanafamilia Mbunge Msigwa' kwa kusababisha kifo hicho, wakati hakuwa na bunduki wala kisu mfukoni.
 
Hawa ndugu zake wakati msigwa anahangaika na iyo kesi walimpa msaada gani? Je kunamchango wowote walimchangia kulipa mwanasheria? Au walisubir afungwe ndyo wamsaidie? Alafa kwanini alyewafunda ndye katoa 95% yamchango wote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom