Mchungaji Mtikila asema CHADEMA wanahusika na kifo cha Chacha Wangwe; kumfikisha Lowassa Mahakamani

Mchungaji Mtikila asema CHADEMA wanahusika na kifo cha Chacha Wangwe; kumfikisha Lowassa Mahakamani

Umslopagazi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2013
Posts
1,675
Reaction score
903


Swali: Kwa mfano, amesema elimu itakuwa ni ya bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu. Lakini pia amesema anauchukia sana umasikini na amechukua makundi ambayo yamebeba idadi kubwa ya Watanzania: Mama n’tilie, dereva bodaboda na vijana wasiao na ajira. Tuliona juzi akishiriki katika usafiri wa umma – Daladala. Kwahiyo, huenda haya ndiyo mambo ambayo watu yanawatesa sana na ndiyo maana wanataka wampe heshima ya kumuingiza pale Magogoni ili awe Rais wa JMT. Lakini hofu ipo wapi, ni kwa watawala wanaogopa anaweza kuibua yale maovu yaliopo katika mfumo kwsababu alikuwepo katika mfumo wa CCM ama jamii imechukia CCM kwamba ni wakati sasa wa mabadiliko?

Mtikila: Naelewa maovu ya Edward Lowassa toka akiwa Waziri kwenye ofisi ya Waziri Mkuu. Mambo yale yote ya kutisha ambayo kweli angekuwa ameyafanya China, angekuwa hayupo duniani. Angenyongwa hadharani kwa machafu aliyoyafanya.

Huyu ni muongo. Edward Lowassa ni muongo. Alikuwepo humo na wala hajaacha mambo ya CCM. Kilichomuondoa CCM ni urais, lakini chama anachokipenda yeye ni CCM ambayo ndiyo roho yake yeye.

Swali: Labda alichukizwa na mchakato [wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM] ulivyokwenda?

Mtikila; Ndiyo huo mchakato. Lakini matatizo ya nchi hii hayajaletwa na mchakato huo wa CCM, yameletwa na itikadi yenyewe. Toka miaka 54 ambapo tumetawaliwa na hawa jamaa. Inatakiwa mabadiliko kabisa, lakini siyo mnachukua mtu yuleyule aliyekuwa injinia mnamleta huku.

Swali: John Magufuli wanasema katika maamuzi yake mengi anatumia jazba. Lakini anasimamia sera zilezile za bure kuanzia chekechea mpaka Kidato cha Nne. Wakosoaaaji wanasema yeye amejikita katika masuala ya viwanda na barabara tu na mambo mengine ya msingi anayasahau. Je, upande wa CCM unaongeleaje mchakato wao wa kuelekea Magogoni?

Mtikila: Huwa naishiwa nguvu kuzungumza mambo ya CCM kwasababu ndio wanaowajibika tangu tarehe 9 Desemba 1961 nchi yetu ilipokuwa paradiso mpaka walipotufikisha.

Sijamaliza kuhusu huyu wanayemwita Bw. Edward Lowassa kwsababu nakumbuka huyu Bwana, achilia mbali wizi wake mwingi, ninajua kabisa mtu mmoja, jirani yangu, sasa marehemu, Meja Generali Herman Lupogo, vile vizazi vya waadilifu Wajamaa wa kweli. Alikuwa Mwenyekiti TACAIDS…

…alilalamika kwenye kikao: “Mimi nimeambiwa nitoe milioni 150 na Bwana Mkubwa, anazitaka Waziri Mkuu. Hizi pesa za watu, za kusaidia watu wapo hoi bin taabani – wanaishi kwa matumani. Sasa anataka mimi nimpe, siwezi”

Baadaye akasema: “Aling’ang’ana nikasema kwa Rais; Rais hanisaidii. Kwahiyo mimi naacha, kuliko nitende dhambi nisikubaliwe mbinguni – naacha” Akajitoa uenyekiti.

Alivyotoka tu hapo, aliyembadili ni mwanamke mmoja. Alilazimika, alitoa milioni 150. Anataka kujilia kwasababu ya cheo. Sasa, mtu wa jinsi hii mkiona watu mnamshabikia, ni tatizo. Hilo ni tatizo la nchi kubwa sana. Na watu wenyewe wana matatizo, ule utaahira nusu.
 
Last edited by a moderator:
Akiongea startv tuongee asubuhi leo, anasema aliitwa apewe tsh. Mil 100 na kwamba alipangiwa kuuawa. Amemtaja muuaji wa Chacha wangwe. Dah katonesha pabaya kweli.
 
Taarifa yako haijitoshelezi mkuu, unakimbilia wapi, hebu tupe habari iliyokamilika kidogo.kamtaja nani muuaji?
amezungumzia kifo cha chacha wangwe wakiwa wanazungumzia nini?
 
Ameeleza namna gari ya CHADEMA iliyokuwa imembeba Chacha Wangwe ilivyopaki ghafla na kupigwa kichwani.

source, startv
 
taarifa yako haijitoshelezi mkuu, unakimbilia wapi, hebu tupe habari iliyokamilika kidogo
kamataja nani muuaji?
amezungumzia kifo cha chacha wangwe wakiwa wanazungumzia nini?

Mambo mengine tunaweka pending makusudi ohooo cyberlaw kaka.... Ila anaendelea kufunguka yote ya Cdm, Ukawa, Lowassa....yupo Star tv....
 
Hivi Mtikila ni Mchungaji wa Kanisa lipi? Natamani siku moja nihudhurie.
 
hivi makamu mwenyekiti wa chama chake ni nani na katibu mkuu wake ni nani?
 
Mchungaji Mtikila amezidi kusisitiza kuwa wahusika wakuu wa kifo cha Chacha Wangwe ni viongozi wa chadema, ushahidi anao na muda wowote ushahidi huo ukihitajika ataufikisha mahakamani.
 
Mtikila jina lake lilikatwa kwenye wagombea urais so hana hela ya mboga lazima atumike
 
Hata wanyama wanaweza kuwa na busara katika maamuzi ila Mtikila anashangaa wanaomshabikia Edward Lowassa ambaye ni mwizi na kwa uchafu alioufanya nchi hii kama ingalikua ni China angeshanyongwa muda mrefu sana,Awataka watanzania waache ushabiki.

Anaenda mbali zaidi alipozungumzia afya ya Edward Lowassa na kusema maradhi alionayo yanaathiri kichwani.

Kuhusu taarifa za tafiti zilizofanywa na TWAWEZA Mtikila anamshukuru Mungu kwani wanaomuunga mkono Edward Lowassa fisadi ni wachache.

Anaendambali kwakusema watu wanaomshabikia Edward Lowassa wanautahaira nusu(epedomia) anasisitiza Watanzania tuwe makini na huyu fisadi.

Anasema ukiachilia mbali matatizo yao ni afadhali ya Magufuli awe raisi wa nchi.

Mfano anatoa mfano wa afya zao Edward Lowassa ni mgonjwa na hatuwezi geuza Ikulu kua ICU ya wagonjwa.Na anasema mficha maradhi mauti humuumbua na anasisitiza Edward Lowassa angejikita kwenye afya yake kwanza.

Anakumbusha wizi wa Edward Lowassa ambao alituongopea akaahidi kwenda kutununulia mvua na kutumia pesa nying na hatimae mvua yakununua ikawa ni uongo mtupu.
 
Duh sijui nani ktk serikali hii iliyopo asingeitwa Marehemu..so and so
 
Sisi tunamtaka ivo alivyo, ili tuandike historia, kwani mpaka Ulaya wafanye ndo tuige?!
 
Back
Top Bottom