Mchungaji Samweli Karao apiga Marufuku Kampeni za Siasa Msiba wa aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Arumeru

Mchungaji Samweli Karao apiga Marufuku Kampeni za Siasa Msiba wa aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Arumeru

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966


Mchungaji Samweli Karao wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), anayeongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Arumeru, Albert Elias Mollel, amewaonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kutumia msiba huo kwa malengo ya kisiasa. Akihubiri mbele ya viongozi mbalimbali na mamia ya waombolezaji waliokusanyika nyumbani kwa Albert eneo la Ngaramtoni, jijini Arusha, Mchungaji Karao amesema: “Niwatahadharishe, hii ni ibada takatifu ya Mungu, si mahali pa kampeni au kauli za kisiasa. Nisisikie suala kama hilo lililoandikwa kwenye tisheti. Hapa ni mahali pa ibada ya kumlaza mpendwa wetu, si siasa.”

Amesisitiza kuwa yeye ni mchungaji wa watu wote, bila kujali itikadi zao za kisiasa “Hata kile chama kinachokula ubwabwa ni chama changu, kwa sababu mimi ni mchungaji wa kila mmoja”. Ibada hiyo ya mazishi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali akiwamo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara, John Heche.
 
Back
Top Bottom