Mchuuzi ( Boniface Kariuki) aliyepigwa risasi na polisi katika maandamano Nairobi athibitishwa kufariki

Wa Nuni

Senior Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
104
Reaction score
209
Boniface Kariuki, mchuuzi aliyepigwa risasi wakati wa maandamano wiki mbili zilizopita jijini Nairobi, amefariki dunia. Msemaji wa familia, Emily Wanjira, amesema Kariuki alithibitishwa kuwa amefariki saa tisa na robo jana alasiri

Taarifa za awali kutoka kwa Familia ilisema madaktari wamewataarifu kuwa ubongo wa kijana wao Boniface Kariuki, umekufa

Familia ya Kariuki sasa inataka polisi waliompiga risasi mpendwa wao kuwajibishwa kisheria.

Familia ya Kariuki ilidai polisi waliompiga risasi mpendwa wao kuwajibishwa kisheria
Kulingana na msemaji wa familia Emily Wanjira, madaktari katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta waliwaambia kwamba viungo vya mchuuzi huyo vingali vinafanya kazi licha ya ubongo wake kufa.
Kariuki yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili kuondoa risasi iliyokuwa imekwama katika kichwa chake, akichunguzwa kwa ukaribu na madaktari
Kwa sasa familia ya Kariuki inataka maofisa waliompiga risasi mpendwa wao kuwajibishiwa.
Tayari mashirika ya kiraia na wanaharakati wanashinikiza kufanyika kwa mageuzi ya dharura kwenye idara ya polisi
 
Jeshi la polisi africa mashariki linapswa kufanyiwa marekebisho makubwa kuendana na wakati
 
Hao MAMMBWA si wamekamatwa..? Walishakamatwa
 
Boniface Kariuki, mchuuzi aliyepigwa risasi wakati wa maandamano wiki mbili zilizopita jijini Nairobi, amefariki dunia. Msemaji wa familia, Emily Wanjira, amesema Kariuki alithibitishwa kuwa amefariki saa tisa na robo jana alasiri

Taarifa za awali kutoka kwa Familia ilisema madaktari wamewataarifu kuwa ubongo wa kijana wao Boniface Kariuki, umekufa

Familia ya Kariuki sasa inataka polisi waliompiga risasi mpendwa wao kuwajibishwa kisheria.

Familia ya Kariuki ilidai polisi waliompiga risasi mpendwa wao kuwajibishwa kisheria
Kulingana na msemaji wa familia Emily Wanjira, madaktari katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta waliwaambia kwamba viungo vya mchuuzi huyo vingali vinafanya kazi licha ya ubongo wake kufa.
Kariuki yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili kuondoa risasi iliyokuwa imekwama katika kichwa chake, akichunguzwa kwa ukaribu na madaktari
Kwa sasa familia ya Kariuki inataka maofisa waliompiga risasi mpendwa wao kuwajibishiwa.
Tayari mashirika ya kiraia na wanaharakati wanashinikiza kufanyika kwa mageuzi ya dharura kwenye idara ya polisi
Simuonea huruma marehemu na siionei huruma familia.
 
Hakuna atakayesalia chini ya jua,tunatofautiana vifo tu.Apumzike kwa amani Boniface Kariuki.
 
Hv nchi ya kidemokrasia yenye katiba nzuri na polisi waelewa inaua watu tena?
 
Back
Top Bottom