Baraza la Vyombo vya Habari Kenya (MCK) limetaka hatua za haraka kuchukuliwa dhidi ya watu wanaoshambulia na kutishia waandishi wa habari nchini. MCK imesema jumla ya waandishi 18 na madereva wawili kutoka vyombo mbalimbali vya habari wameshambuliwa na kujeruhiwa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Miongoni mwa matukio ya hivi karibuni ni mashambulizi yaliyotokea wakati wa mkutano wa Linda Mwananchi mjini Homa Bay, ambapo waandishi kadhaa walijeruhiwa, vifaa vyao kuharibiwa au kuibwa, huku gari la chombo kimoja cha habari likichomwa moto.
MCK imeitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP), Inspekta Jenerali wa Polisi na IPOA kuhakikisha kesi hizo zinachunguzwa na wahusika wanafikishwa mbele ya sheria. Baraza hilo limesema kutokuwepo kwa hatua dhidi ya wahalifu kunazidi kuwapa ujasiri wa kuendelea na vitendo vyao.
MCK imeonya kuwa hali hiyo ni tishio kubwa kwa uhuru wa vyombo vya habari, upatikanaji wa taarifa na demokrasia, hasa Kenya inapokaribia Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Kwa nini waandishi wanaofanya kazi yao ya kuwafahamisha wananchi wanaendelea kuwa walengwa wa mashambulizi?