MCL: Mkuu wa Mkoa adaiwa kumlawiti mwanafunzi wa SAUT

MCL: Mkuu wa Mkoa adaiwa kumlawiti mwanafunzi wa SAUT

Yes mkuuu na labda nikujuzee wahusika wakuu hapa n wafamyabiashara

Rc ukienda todauti na wafanyabiashara wa eneo lile nakwambia watakushawishi ujae ukijaa wanakusukumua tairi la moto

Kunanduguyangu aliteuliwa akawa mtulivu kweli sijui ikawaje akaanza kuonekana kukaripia wafanyabiashara eneo lileunajua wanaume kama auko kwenye pombe uzinzi kama sio uzinzi ufiraji

Wakamtwika zigo mojaaa lam
aanaa naloo la chuoo akàlewaa demu anachat na wakuu akamrekodi akiwa na boxer nk ndugu magu hata akutaka saliamtume sijui uchunguzi akahojiwa na wazee wakazi hizi picha zako nk akakiri mzigo ukatoa panapotakiwaa

Sema n vyema pia ukishajua level yako jihadhari nahayamamboo

2.tafuta Lodge ambazo unajua mnaweza kusitiriana
3.usimwamini mtu wengi wakiteuliwa wanajisahau wanajua wakosafe na wale waliowakuta kumbe wanawalia tymng wakiaribu wanarekodi imeisha hio

4.kama uliyazoea sana uźinzi pombe unapunguza kidogo

5.kama unauwezo pangisha kabisa sehemu inageti ukiwa na manziii unaenda zakoo husika unatoaa ganzi unarudiihme safe

6 bar sioo sehemu nzurii sana ya kujichanganya niliwahi ona dc wa tarime enzi zamagu alikuwa anamikwara kwa mademu mwisho wa siku akiwa bar akanza kutembea na bastola last jamaa wkamrekodi magu akumuacha tena kandikwa live gazetin katoka sababu ya pombe ...akilewa anakwambia n rais wa tarime hakuna wakumgusa mara nikimtaka yoyote namchukua mweeee alipoitws kuhojiwa akakana akaonyeshwa kalewa na bastola mezan akakiri ikaisha

Vijana wengi wakiteuliwa wanahisi ndio sehemu ya kumaliza starehe zaooo za maisha wamesahau hata Yesu alikuwa na yuda pemben

Aldbestyusufffuuueeee kidumewambegu
Mambo ambayo nimejifunza kwa muda mrefu (uzoefu wangu)ni:-
1. Ukipata au ukiwa ni mkubwa mahali pako pa kazi; jiongeze mara dufu kwa kuchukua tahadhari kubwa ukijua kwamba hiyo nafasi uliyopata, wapo wengi waliitamani na wanaitamani na pengine walikuwa wanaifukuzia. Jihadhari.
2. Usiku una mambo mengi mno i.e. wakati wa giza una mambo mengi sana. e.g. Nimehudhuria kesi nyingi mahakamani na amini usiamini, 95% ya mashauri yaliyokuwa yameletwa mahakamani ni mambo au ni matukio yaliyohusu mambo yaliyotendwa usiku. e.g. Kipigo na kujeruhi, Kufumania na kujeruhi kwa silaha(Kukata mapanga), Kubaka na kulawiti, wizi, n.k.
3. Matumizi ya pombe (Unywaji)yaliyopitiliza(Ulevi)ni kitu kinachochangia kwa kiasi kikubwa mno mtu kutenda jambo ambalo ni aibu kubwa na pengine ingekuwa kama sio kulewa pombe, kamwe asingelifanya tukio hilo e.g. Kutorosha mke/mme i.e. kuvunja ndoa ya mtu au kukamatwa Ugoni n.k.
Mwisho ni kwamba ukichanganya vyote kwa pamoja na katika eneo moja;
Giza/Usiku + Madaraka + Pombe/Ulevi+ Tamaa za mwili zisizodhibitiwa (Ashki = Genye) Utapata maangamizo au wanaita anguko kuu na usipokufa au kufungwa jela bahati yako ila hutakosa kupata majeraha/Madhara ya kimwili, kiuchumi na kiroho.
 
humu wengi tunamuhukumu jamaa hata bila ya ushahidi

nacho ona ni roho mbaya za kitanzania tu kufurahia mwenzako kupata shida

humu kama ingekuwa ni haki 90% tulistahili kuwa jera
Watanzania wengi hatuna kitu. Kwahiyo tukiona aliye nacho kapata shida tunajipa furaha "hewa" ( yaani furaha ambayo haituondolei shida zetu)
 
Mwanza/Dar. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linaendelea na uchunguzi juu ya tukio la kigogo mmoja wa juu ngazi ya mkoa wa kanda ya ziwa, kutuhumiwa kumlawiti mwanafunzi wa chuo kikuu jijini Mwanza ndani ya gari.

Uchunguzi umebaini jina la usajili wa namba ya simu iliyotajwa na mwanafunzi huyo, linafanana na la mmoja wa wakuu wa mikoa nchini.

Mbali na usajili huo ambao hufanywa kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa kuonyesha jina linalofanana na la mteule huyo, lakini jina hilohilo pia ndilo linaonekana katika tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa huo na akaunti ya Instagram.

Lakini jina hilo pia limetokea katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mwaka 2022 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ingawa jina linaloonekana kwenye usajili wa simu na lile linaloonekana katika akaunti ya mkuu wa mkoa huyo kwenye mtandao wa Instagram, linatofautiana kwa jina la katikati.

Tukio hilo linalodaiwa kutokea Juni 2, 2024 katika eneo la maegesho la moja ya baa mashuhuri jijini Mwanza, tayari limeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii hususan X (zamani Twitter) ingawa aliyetoa taarifa hiyo, hakumtaja mhusika kwa jina.

Uchunguzi wa gazeti hili kutoka vyanzo mbalimbali jijini Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam, vimedokeza uchunguzi wa suala hilo unafanywa kwa usiri mkubwa, kwani mtuhumiwa ni mtu mzito serikalini ambaye mpaka jana jioni alikuwa hajatiwa mbaroni.

Kulingana na taarifa kutoka vyanzo hivyo, tayari polisi walichukua sampuli kwa ajili ya kupima vinasaba (DNA) kutoka katika nguo alizokuwa amevaa mwanafunzi huyo kama zitaoana na mtuhumiwa na kuzituma kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Taarifa zimeeleza tukio hilo linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza na tayari taarifa za awali zimetumwa kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan Kingai ambaye alipotafutwa hakupatikana.

Gazeti hili limemtafuta mmoja wa maofisa Ofisi ya Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema:“Taarifa za tukio hilo aulizwe Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.”

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Wilbrod Mtafungwa alipotafutwa amesema: “Nipo msibani kwa sasa hivi.’’ (ilikua saa 10 jioni)

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya alipotafutwa ikiwa ni saa 12:40 jioni kuhusu suala hilo, hakukubali wala kukanusha juu ya uwepo wa tukio hilo zaidi amesema: “Yapo mambo anayoongea kamanda kama kamanda.”

Alipoulizwa na gazeti hili kuwa yeye ndiye ameachiwa ofisi, Kamanda Msuya alisisitiza atafutwe kamanda Mutafungwa kwani ndiye hutoa taarifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda alipotafutwa kuzungumzia suala hilo kutokana na yeye kuwa mwenyekiti wa usalama mkoani humo amesema: “Mimi sijaletewa kwenye dawati langu hilo tukio la mwanafunzi na huyo mwanafunzi hajaniletea hilo suala labda niwasiliane na polisi.”



Hivi ndivyo uhusiano ulivyoanza
Uchunguzi wa gazeti hili kwa kuegemea vyanzo mbalimbali jijini Mwanza, Dar es Salaam na Dodoma, zinaeleza mtuhumiwa huyo alianza uhusiano na mwanafunzi huyo mwenye miaka 21 Januari 2024 jijini Mwanza.

Siku hiyo walikutana katika tafrija ya siku ya kuzaliwa ambayo mtuhumiwa anatajwa ndiye alikuwa mgeni rasmi na hapo ndipo walipobadilishana simu na kuanzisha uhusiano na kuendelea kuwasiliana kwa simu mara kwa mara.
“Unajua huyu bosi ili kumu win (kumpata) huyu dada alianza kumtumia fedha za matumizi ya hapa na pale. Sasa ile mwezi Februari 2024 kama utakumbuka kulikuwa na ziara ya Rais hapa Mwanza,” kimesema chanzo chetu.

Chanzo hicho kimedai siku hiyo kigogo huyo alikutana na dada huyo katika moja ya hoteli jijini Mwanza, ambapo katika hali ya kustaajabisha, alimuomba wafanye mapenzi kinyume cha maumbile, ombi ambalo dada huyo alilikataa.

Kigogo huyo inadaiwa aliendelea kumshawishi akubali kufanya naye mapenzi kinyume cha maumbile kwa ahadi kuwa angempa maisha mazuri na kumuahidi angekuwa anampa kiasi kisichopungua Sh500,000 kila mwezi.

Tukio lenyewe lilivyokuwa
Chanzo kimoja kutoka ofisi ya kigogo huyo, kimedai siku ya tukio, mtuhumiwa alitumia kila mbinu kumshawishi mwanafunzi huyo wakutane jijini Mwanza, ambapo walikutana katika baa hiyo mashuhuri na kupata vinywaji.

“Sasa baada ya muda huyu jamaa akamuambia wakazungumze kwenye gari maana kuna mambo ya muhimu anataka kumweleza. Huko sasa jamaa ndio akashinikiza wafanye kinyume cha maumbile,” kimedokeza chanzo hicho.

Chanzo kingine kutoka moja ya ofisi nyeti za Serikali jijini Dodoma, kimedai baada ya kwenda kwenye gari lililokuwa limeegeshwa eneo la maegesho ya klabu hiyo, ndipo kigogo huyo alipotimiza haja zake.

“Tunavyoambiwa sio kwamba huyo mwanafunzi aliridhia, hapana. Huyu jamaa alimtisha sana na kwa vile huyu dada alikuwa anamjua kama mheshimiwa, alijua ni watu wanatembea na silaha na walinzi hivyo akafanya aliyoyafanya”.

“Inaonekana huyu ni mchezo wake baada ya kumshawishi sana huyu dada wa watu akamgomea. Ndio naona akaja na hiyo plan B (mpango wa pili) wa kumwita kwenye gari akamvua nguo kwa nguvu na kumlawiti,” kimesema chanzo kingine.

Chanzo kingine kilidai kigogo huyo na gari alilolitumia vilinaswa na kamera za usalama zilizofungwa katika klabu hiyo tangu gari hiyo inaingia, kuegeshwa na kutoka usiku wa saa sita na namba za usajili zilisomeka vizuri.

Kamera zinaonesha ilipofika saa 2:48 usiku, binti huyo alionekana akiingia katika gari hilo na saa 3:21 usiku, takribani dakika 30 kupita, mlalamikaji alionekana akitoka kwenye gari.

Saa 6:24 usiku, zinaonesha gari hilo lilionekana katika geti la kutokea likiwa eneo la mwanga mkali uliowezesha kulitambua usajili wake. Dereva wa gari hilo alikuwa amevalia kofia aina ya kapelo akitoka kwenye gari hilo kwa ajili ya kulipia ushuru wa maegesho.

Taarifa zinadai, Juni 3 mwaka huu, siku moja tangu alipofanyiwa ukatili huo, binti huyo alikwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi-dawati la jinsia na watoto, jijini Mwanza. Alisikilizwa kisha kupelekwa moja ya hospitali kubwa jijini hapo kwa uchunguzi.

Katika uchunguzi huo uliofanywa na daktari (jina tunalihifadhi), alibaini mwanafunzi huyo wa mwaka wa kwanza aliingiliwa kinyume na maumbile.
Taarifa zinadai Jeshi la Polisi limetuma barua Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza ili kupata usajili wa namba za gari hilo aina ya Toyota Crown nyeupe.

Aidha, tararibu za kupeleka simu ya mlalamikaji na vipande vya picha zilizopigwa na kamera za usalama zinaandaliwa kwa ajili ya kupelekwa kwenye maabara ya uchunguzi wa kisayansi.

Mwananchi

====




Pia, soma=> Mkuu wa Mkoa Simiyu atenguliwa, Kenan Kihongosi achukua nafasi hiyo
Duuu Mzee mzima anatatua marinda ya kitoto ya 2023 duuu tuwe na huruma tusitumie fedha zetu kuhariba maisha wa watoto
 
Back
Top Bottom