mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Sasa we kiongozi unakwenda the cask bar 😄Mambo ambayo nimejifunza kwa muda mrefu (uzoefu wangu)ni:-
1. Ukipata au ukiwa ni mkubwa mahali pako pa kazi; jiongeze mara dufu kwa kuchukua tahadhari kubwa ukijua kwamba hiyo nafasi uliyopata, wapo wengi waliitamani na wanaitamani na pengine walikuwa wanaifukuzia. Jihadhari.
2. Usiku una mambo mengi mno i.e. wakati wa giza una mambo mengi sana. e.g. Nimehudhuria kesi nyingi mahakamani na amini usiamini, 95% ya mashauri yaliyokuwa yameletwa mahakamani ni mambo au ni matukio yaliyohusu mambo yaliyotendwa usiku. e.g. Kipigo na kujeruhi, Kufumania na kujeruhi kwa silaha(Kukata mapanga), Kubaka na kulawiti, wizi, n.k.
3. Matumizi ya pombe (Unywaji)yaliyopitiliza(Ulevi)ni kitu kinachochangia kwa kiasi kikubwa mno mtu kutenda jambo ambalo ni aibu kubwa na pengine ingekuwa kama sio kulewa pombe, kamwe asingelifanya tukio hilo e.g. Kutorosha mke/mme i.e. kuvunja ndoa ya mtu au kukamatwa Ugoni n.k.
Mwisho ni kwamba ukichanganya vyote kwa pamoja na katika eneo moja;
Giza/Usiku + Madaraka + Pombe/Ulevi+ Tamaa za mwili zisizodhibitiwa (Ashki = Genye) Utapata maangamizo au wanaita anguko kuu na usipokufa au kufungwa jela bahati yako ila hutakosa kupata majeraha/Madhara ya kimwili, kiuchumi na kiroho.
Ova