Uwesutanzania
JF-Expert Member
- Feb 9, 2019
- 1,380
- 1,686
Mda ambao mtoto anautumia kuwa shule ni mda mwingi mno.
Namaanisha ni ile anaenda shule saa 11 asubuhi alafu anarudi saa 11 jioni, kuanzia Jumatatu mpaka ijumaa,.
Hii inapelekea mtoto kukosa malezi bora ya mzazi na kutengeneza jamii isio na maadili mema.
Au kama ni ngumu kupunguza mda wa mtoto kuwa shule basi msogeze mda wa kuwapokea hawa watoto.
Yaani muanze kupokea watoto wenye umri wa miaka 12 na zaidi au hata 14. Hii itasaidia kupokea watoto ambao tayari wana malezi bora kutoka kwa wazazi wao familia na jamii kwa ujumla.
Nimesema haya yote ni baada ya kuwa na mitaala mibovu katika shule zetu za msingi na kuwa na waalimu wasio na weredi katika kumjengea mtoto kesho yake iliyo njema katika jamii na maisha yake kiujumla.
Siku izi kumekuwa na vijana wenye maadili mabovu na wasio na matendo mema bila ya kujua nini mzizi wa haya yote,.
Ndugu yangu msomaji mwaribifu mkubwa wa kizazi chako ni shule na waalimu.
Hivyo ili kuokoa kizazi chako jitahidi sana uwe unatumia mda mwingi kuwa kalibu na watoto wako ni si kuipa majukumu shule.
Cha kushangaza zaidi wazazi wengi mmekuwa mnaanza kupeleka watoto katika shule za awali wakiwa wadogo sana miaka 3,4,5 nk hii sio sawa.
Huku ni kumuaribu mtoto kizungu wanachojifunza na masomo wanayofundishwa hayana maana yeyote katika maisha yao na familia zao za baadae.
Ni mimi wako UWESUTANZANIA.

Daaaah, mwanangu umefikili kimjini sana. Alafu mimi nipo zangu kijijini huku. Tunaamka asubuhi mimi na mke wangu tunaenda shamba kila siku bila ya watoto wetu kwa kigezo cha shule,. Afu inakuwa wakija hawajui jembe, afu wanarudi mtaani elimu imeshawatupa.
Mazazi menyewe matakataka haya yana malezi gani?
Nchi zilizofanikiwa ktk elimu,muda wa masomo ni mdogo sana.Kwa mfano Finland watoto wanaanza shule kuanzia umri wa miaka 7 na masomo yanakuwa masaa machache kwa siku.Walimu wa kwanza ni wazazi au walezi nyumbani na watoto lazima wapitie utoto wao wakiwa nyumbani.Tunaomba Mhe Rais alione hili na afanye mabadiliko ktk elimu na historia itamkumbuka kwa hili.