Mda wa mtoto kuwa shule upunguzwe

Mda wa mtoto kuwa shule upunguzwe

Shule Gani inapokea watoto saa 11 alfajiri?

Kama muda huo ndo muda anaotoka nyumbani kwako hizo ni chanagamoto zako wewe tafuta shule karibu na maeneo unayoishi

Haya ni matatizo ya nani wazazi au shule ?

Sasa unawapeleka kufanya nini kama hakuna faida
Unajua kengele ya kwanza ya shule za msingi inagongwa saa ngapi?
 
Hoja yako ni ya msingi saana naona wadau wanakupuuza,
kuna jirani anawapitisha shule asubuhi anawapitia jiooon akirud kutoka job
 
Afu mzazi anakuja kuwa wa kwanza kutoa machozi akiona picha za utupu za mwanae mtandaoni.
Hajui mfumo wake ndio ulimuaribu.

Mtoto anatoka fomfo anatafuta camera au simu kubwa anaanza tumia makalio yake kutengeneza KONTEKTI.
Tanzania na mifumo yetu ya elimu tubadilike sana
 
Jamaa kaleta mada halafu anaijibu yeye mwenyewe! Ujinga huu!
Hawa ni watu ambao huwa hawana fikra pana. Hapa JF naamini mtu kuanzisha mada ni kutaka kujifunza kutoka kwa ambao wana mawazo tofauti nawe au wenye added advantage kwa maoni yako
 
Mda ambao mtoto anautumia kuwa shule ni mda mwingi mno.

Namaanisha ni ile anaenda shule saa 11 asubuhi alafu anarudi saa 11 jioni, kuanzia Jumatatu mpaka ijumaa,.

Hii inapelekea mtoto kukosa malezi bora ya mzazi na kutengeneza jamii isio na maadili mema.

Au kama ni ngumu kupunguza mda wa mtoto kuwa shule basi msogeze mda wa kuwapokea hawa watoto.

Yaani muanze kupokea watoto wenye umri wa miaka 12 na zaidi au hata 14. Hii itasaidia kupokea watoto ambao tayari wana malezi bora kutoka kwa wazazi wao familia na jamii kwa ujumla.

Nimesema haya yote ni baada ya kuwa na mitaala mibovu katika shule zetu za msingi na kuwa na waalimu wasio na weredi katika kumjengea mtoto kesho yake iliyo njema katika jamii na maisha yake kiujumla.

Siku izi kumekuwa na vijana wenye maadili mabovu na wasio na matendo mema bila ya kujua nini mzizi wa haya yote,.

Ndugu yangu msomaji mwaribifu mkubwa wa kizazi chako ni shule na waalimu.

Hivyo ili kuokoa kizazi chako jitahidi sana uwe unatumia mda mwingi kuwa kalibu na watoto wako ni si kuipa majukumu shule.

Cha kushangaza zaidi wazazi wengi mmekuwa mnaanza kupeleka watoto katika shule za awali wakiwa wadogo sana miaka 3,4,5 nk hii sio sawa.

Huku ni kumuaribu mtoto kizungu wanachojifunza na masomo wanayofundishwa hayana maana yeyote katika maisha yao na familia zao za baadae.

Ni mimi wako UWESUTANZANIA.

Zamani kidogo mwanafunzi wazembe au wasioelewa kwa haraka/kawaida kama wenzao ndio walikua wanapitiliza saa nane mpaka saa 11 wakiita remedial classes kuwasaidia wanafunzi waweze kwenda sawa na wenzao.

Naona wakanogewa, umekua utaratibu wa kawaida sasa, uwe unaelewa au huelewi wote saa 11.

Sababu nyingi saivi ni za kibiashara tu wala sio kitaaluma kutokana na ushindani uliopo.

Changamoto kubwa nikiachana na uliyotoa mtoa mada, Watoto hawa hawana elimu wala maarifa mengine mbali na inayotolewa shuleni. Hata kazi ndogo ndogo za nyumbani hawawezi kufanya. Na hata wakati wa likizo utakuta wanaanzishiwa tuition 😂😂
 
Utaratibu wa shule za msingi za umma, zinapokea wanafunzi saa ngapi na wanatoka muda gani?

Nakumbuka zamani, unaingia saa moja kamili saa nne unatoka; wengine wanaingia saa nne wanatoka saa saba au nane.

Huu utaratibu wa kwenda shuleni usiku, ameuleta nani? Na una tija gani katika uvumbuzi wa viwanda?​
 
Mda ambao mtoto anautumia kuwa shule ni mda mwingi mno.

Namaanisha ni ile anaenda shule saa 11 asubuhi alafu anarudi saa 11 jioni, kuanzia Jumatatu mpaka ijumaa,.

Hii inapelekea mtoto kukosa malezi bora ya mzazi na kutengeneza jamii isio na maadili mema.

Au kama ni ngumu kupunguza mda wa mtoto kuwa shule basi msogeze mda wa kuwapokea hawa watoto.

Yaani muanze kupokea watoto wenye umri wa miaka 12 na zaidi au hata 14. Hii itasaidia kupokea watoto ambao tayari wana malezi bora kutoka kwa wazazi wao familia na jamii kwa ujumla.

Nimesema haya yote ni baada ya kuwa na mitaala mibovu katika shule zetu za msingi na kuwa na waalimu wasio na weredi katika kumjengea mtoto kesho yake iliyo njema katika jamii na maisha yake kiujumla.

Siku izi kumekuwa na vijana wenye maadili mabovu na wasio na matendo mema bila ya kujua nini mzizi wa haya yote,.

Ndugu yangu msomaji mwaribifu mkubwa wa kizazi chako ni shule na waalimu.

Hivyo ili kuokoa kizazi chako jitahidi sana uwe unatumia mda mwingi kuwa kalibu na watoto wako ni si kuipa majukumu shule.

Cha kushangaza zaidi wazazi wengi mmekuwa mnaanza kupeleka watoto katika shule za awali wakiwa wadogo sana miaka 3,4,5 nk hii sio sawa.

Huku ni kumuaribu mtoto kizungu wanachojifunza na masomo wanayofundishwa hayana maana yeyote katika maisha yao na familia zao za baadae.

Ni mimi wako UWESUTANZANIA.
Nakumbuka enzi hizo soma popatlal secondary school tulikua tu naanza classes 8am na kumaliza 12:40pm kila siku na shule Ilikua inafanya vizuri Zaid ya waliokua wanashinda shule
 
Zamani kidogo mwanafunzi wazembe au wasioelewa kwa haraka/kawaida kama wenzao ndio walikua wanapitiliza saa nane mpaka saa 11 wakiita remedial classes kuwasaidia wanafunzi waweze kwenda sawa na wenzao.

Naona wakanogewa, umekua utaratibu wa kawaida sasa, uwe unaelewa au huelewi wote saa 11.

Sababu nyingi saivi ni za kibiashara tu wala sio kitaaluma kutokana na ushindani uliopo.

Changamoto kubwa nikiachana na uliyotoa mtoa mada, Watoto hawa hawana elimu wala maarifa mengine mbali na inayotolewa shuleni. Hata kazi ndogo ndogo za nyumbani hawawezi kufanya. Na hata wakati wa likizo utakuta wanaanzishiwa tuition 😂😂
Kabisa mkuu
 
  • Thanks
Reactions: I M
Yote haya yamesababishwa na mfumo wa elimu mbovu nchini ambayo imepelekea wengi kupeleka vishule vya english medium ambayo hulazimishwa kuwaamusha usiku kutokana na umbali.Tungekuwa na mfumo mazuri wa elimu kama ulivyo wa Rwanda,Kenya,Burundi,Uganda au Malawi kusingekuwa na watu wanahangaika na hivi vi English medium.
 
Mbona bado wanakaa mda mdogo sana tena mda huo hata nyumbani wazazi huwa hawapo
Saa 1-9 masaa yaliyobaki wanakuwa nyumbani
Sababu za maadili kuporomoka ziko mtaani zaidi kuliko shule
 
Back
Top Bottom