Mdahalo: Kipi Ni Sumu Ya Muungano - Je, Ni Kwa Kuikataa Tanganyika au Ni Kwa Kuikubali Tanganyika?

Mdahalo: Kipi Ni Sumu Ya Muungano - Je, Ni Kwa Kuikataa Tanganyika au Ni Kwa Kuikubali Tanganyika?

Kama haulengi kuongelea faida za Muungano huu uzi una faida gani? Waste of time and energy.

Sijaiona hiyo faida ulioongelea na wala Kobelo aliyoiongelea, kama iko iwekeni tena hapa tujadili faida za Muungano kama mmeshindwa, kwaheri na siku nyingine usinialike kwenye nyuzi ya Muungano kama haziongelewi faida zake.
Faida za kiuchumi na kijamii.
kijamii kama vile kuwepo kwa watanganyika kama watumwa na wakazi wa visiwa hivyo, na kuwepo kwa wazanzibari kama wakazi wa Tanganyika kabla na baada ya 1964.

Kiuchumi, kama vile Zanzibar kupatiwa fungu la fedha kutoka Tanganyika ili kuendesha serikali yake. Fedha zilizotokana na maliasili za Tanganyika. Kutumia umeme kutoka Tanganyika bila kulipa hata thumni ... etc.
 
Naona hiyo "kwenda zako" ni hasira za kukwambia sina haja ya kujadili jambo lisiloongelea faida ya Muungano
. Utakasirika sana. Jadili na Kobelo. Bye.

Sina hasira yoyote na wewe faizafoxy, hapo nilikuwa nina maana ya "tenda wema uende zako" hapa nikiwa na maana kwamba katika nyakati hizi, hakuna kilicho chema kwa mtanganyika kama kuelewa na kudai haki ya utambulisho wake ndani ya muungano, na tukimaliza jukumu hili ipasavyo, hakika sote tutakwenda zetu (baada ya kumaliza muda wetu duniani), na kuachia watoto na wajukuu na hata vitukuu vyetu nchi bora badala ya bora nchini kama ilivyo sasa; Kama matumizi ya maneno hayo yamekuudhi, niwie radhi;

Hakuna mada hapo. Nyerere kisha aga dunia na hakuna chenya maana alichokiacha duniani zaidi ya wanawe.

Sasa kuhusu hoja kwamba hauoni cha kujadili katika uzi huu kwani Nyerere hayupo nasi tena, kama kweli unaona hiyo ni hoja ya maana, hakuna mtu anayeweza kukulazimisha uendelee kuwepo katika mjadala huu kwani ni haki yako kuwa na mtazamo huo; Vinginevyo kwa mtu yeyote ambae ameingia katika mjadala huu akiwa na uchungu wa kweli juu ya Tanganyika, asingesema maneno hayo, hasa iwapo anaelewa ukweli wa mambo kwamba ingawa mwalimu hayupo nasi tena, msimamo wa Mwalimu kuhusiana na muungano wa serikali mbili, msimamo ambao unaikataa serikali ya Tanganyika, ndio msimamo huo huo ambao kuna dalili zote kwamba CCM pia ndio inaingia nao kama msimamo rasmi wa chama cha mapinduzi kuhusiana na mfumo wa muungano katika muktadha wa katiba mpya - sera ya serikali mbili ndani ya muungano;

Ni matumaini yangu tu kuwa hata huko ulipo, unapigania utambulisho wa utanganyika wako, hata kama mada kama hizi unaziona hazina maana; Asante kwa ushiriki wako;
 
Mkuu Mchambuzi, kuna hoja nakubaliana nawe na zipo ambazo ziziafiki kama nitakavyo eleza.
Serikali 3: Nakubaliana na ujenzi wa hoja yako kuhusu uwepo wa serikali 3 kwa miaka 50.
Uwepo wake haupo wazi na imepelekea sehemu moja kujitambua na kuhisi ni sehemu muhimu ya muungano kuliko nyingine na hapa ni znz

Ni kweli kuwa uwepo wa serikali 3 utapunguza gharama kuliko ilivyo sasa. Kila serikali itakuwa na mipango yake kulingana na uchumi wake tofauti na sasa ambapo serikali moja(SMZ) ina uhuru zaidi na zile mbili zinabanwa kwa gharama ya nyingine ambazo ni Tanganyika na muungano.

Uwepo wa serikali tatu, kila mshirika atakuwa na nafasi sawa bila kuwajibika kwa mwingine ikiwa ni fursa nzuri sana ya self governance. Kwa hesabu, uwazi wa kila serikali utakuwa ni challenge ya self governance nakupunguza gharama tofauti na sasa ambapo serikali ya Tanzania haiwezi kujiendesha bila kufikiria SMZ ambayo ni huru.

Pili, umeuliza swali kama matatizo haya yanatokana na nini. Jibu langu ni kuwa matatizo yanatokana na wanasiasa. Ni wanasiasa wasioweza au wasiotaka kueleza muungano na faida au hasara zake kwa uwazi. Wanajenga hoja nyepesi za hisia zaidi ya uhalisia. Mfano, pamoja na mahausiano ya kidugu na fursa za muungano yupo mwasiasa anayeona tatizo ni ajira za ubalozi baasi.
Wanasiasa hao kwa kiu ya madarka wanashindwa kuueleza muungano kwa uhalisia wa ubaya au uzuri wake huku wakiongozwa na tamaa zaidi badala ya masilahi ya wananchi.

Tatu, Umeuliza je, uwepo wa Tanganyika ni pale tu znz inapokuwa na madai? Jibu langu ni kuwa hiyo ni sehemu inayoochochea na si dhana nzima. Muungano ni kama ndoa, kwamba kila mmoja anapoteza au anatoa kwa ajili yake. Kwa muda mrefu Tanganyika imesimama katika hilo na tukubaliane imetoa zaidi ya inachopaswa

Watanganyika wameamini uwepo wa muungano lakini kwa kuzingatia kuwa mshiriki wa 'ndoa' amekuwa na madai zaidi badala ya kutoa ndipo wameeamka. Mfano, madai ya utaifa wa znz imewafanya Watanganyika wajihisi hawana mshiriki na hivyo kuanza kudai utaifa wao katika familia.

Kilichochagiza zaidi ni uwepo na kujitambua kwa kizazi kipya cha Tanganyika, na pili ni kutokana na 'narcissism' ya upande wa pili. Mzanzibar anapojitambua kama mzanzibar na si Mtanzania hilo linaleta swali Mtanzania ni nani kama tulikubaliana kuwa tutakuwa Watanzania.

Mzanzibar anajitambulisha kama Mtanzania pale anapohitaji fursa za Tanzania basi. Kwa msingi huo Mtanganyika hana utambulisho wake na wala utambulisho wake haukubaliki Zanzibar na kujihisi yatima.
Ni kutokana na uyatima huo nguvu ya kudai Tanganyika inazidi hasa kwa kuzingatia amejitoa zaidi.
Ninauhakika nitasomeka kama 'biased' lakini naamini hicho ndicho chanzo na nasimama na hilo.

Jp Omuga amesema Zanzibar ilikuwa huru kabla na hoja kwamba katika serikali 3 haitajiweza ni hafifu.
Ninadhani Jp Omuga hajaliangalia suala hili kiuchumi zaidi. Zanzibar itakuwepo hata muungano ukivunjika leo. Hiyo ni tofauti na uwepo wa serikali ya shirikisho ambapo udhaifu wa znz utakuwa wazi.

Madai ya Omuga ni usawa katika muungano, hilo ni kweli lakini usawa huo lazima uwe na mipaka.
Mathalani, huwezi kuongelea usawa katika fursa na kuacha gharama.
Mfano, tukikubaliana usawa huo katika kila jambo basi twende mbele hadi gharama.

Uwepo wa serikali ya shirikisho ni mzigo kwa znz kutokana na saizi ya uchumi wake.
Nimewahi kutolea mfano kuwa gharama za serikali ya shirikisho zikiwa trilioni moja tubasi 2/3ya uchumi wa znz utakwenda huko. Hapo ndipo ukweli kuwa znz haitamudu unapokuwa wazi.

Serikali 2 haiwezekani tena kwa kuingatia kuwa miaka 50 hakuna suluhu hatutegemei muujiza mwingine.
Uwepo wa serikali 3 unaweza kuwa na suluhu, lakini pia lazima suluhu hiyo itanguliwe na nia, sababu za kiuchumi na kijamii zaidi kuliko siasa. Ni lazima washirika waelewe kuwa na ulazima wa kutoa ili muuungano uwepo.

Nia ya muungano itajengwa kwanza kwa kura za maoni. Kura ya maoni itandoa 'narcissism' na kupelekea kukubali kutoa kwa ajili ya muungano.

Kwa hali ilivyo hakuna silver bullet ya tatizo la muungano kama wanavyosema akina Nape.
Ni lazima kwanza Tanganyika iandike mustakabali wa utaifa wake ili ijijengee 'narcissism' kama waliyo nayo wazanzibar.

Halafu kura ya maoni ifuate. Kutokana na dhamira hizo kama muungano utaamuliwa kuwepo kila mmoja itabidi aweke kando 'narcissism' yake na akubali kutoa baadhi ya mambo ya utaifa kwa ajili ya muungano.

vinginevyo tutalazimisha tu na tatizo litakuwepo miaka mingi ijayo.
Lakini pia kwanini sisi kama Watanganyika na Wazanzibar tujifunge katika muungano tuu na tusiwe na option nyingine ya kukutana katika jumuiya kama EAC, SADC n.k.

Swali ninalokuacha nalo ni hili, kwanini tujifunge katika muungano na tusifikirie option zingine?
Kuna tatizo gani tukienda EAC tukalinda interest zetu kwa pamoja kila mmoja akiwa na nchi yake?
Kwanini uhusiano wetu wa muda mrefu ujengwe katika katiba na isiwe kama ilivyokuwa mwaka 1964 au kabla?
 
Nitapita tena badae kudadavua zaidi kuhusu Muungano wenu. lakin kwa kifupi
1. Uwoga waTz bara kuujadili muungano huo kinaga ubaga nafikiri wanakhofia asira za JKN enzi zake kwani aliweza hata kuwalazimisha Rais wa Znz wakti ule Jumbe ajiuzuru na hata Wabunge wa Bunge la Muungano G57 wasijadili kuhusu kuanzishwa kwa Serikali ya tanganyika.

2. Upande wa bara kuwa waoga sana kuanzishwa kwa Serikali yao na kila wakti waZnz wanapodai maslahi yao katika mvungano wenu wanakuwa vinala wakubwa wa kuitabiria mabaya na kusahau kujadili namna ya kuanzisha serikali yao hususan katika changamoto walizonazo za Siasa, Ukabila na udini uliotamalaki nchini mwao.

3. Wengi tunaamini HAKUNA DHAMBI MBAYA KULIKO DHAMBI YA KUNUNG'UNIKA. Hiyo ni moja ya watu kutoka upande pili wa muungano. Siku zote wa Znz wamekuwa wakisimama na kulalamikia kuhusu Muungano bila kificho wala aibu yoyote ;lakin majirani zao wao wamekuwa wananung'unika tu bila kupaza sauti.

Mimi naamini kama utafanyika mjadala wa wazi kuujadili muungano wenu bila kuficha kitu na kupalekea kuondoka kero zote basi mtakuwa mumeweka muungano madh'buti lakin huu wa kuzidisha kero kila kukicha kunalemaza na kulegeza muungano na kufikia kusema Bora kila mtu achukue mbao zake. Kwa katika Duniya mtakuwa sio wa kwanza kuvunja Muungano MBONA HATA EAC ilivunjika na JKN ndie aliyekuwa kinara katika kuvunja EAC, kwanini sisiwe kwa Znz na TGK?

Nitapita baadae kidogo nikinafasika Inshallah kujadili kwa kina point zangu.
 
Kwanini Tanzania Bara ndiyo pia Tanganyika? Where do we draw the line? Halafu tena rais wa Tanzania ni rais wa Tanganyika vilevile. Zanzibar wana kila kitu cha kwao halafu tena tunachangia hivi vya kwetu. Ndiyo maana kuna Wazanzibari ni mawaziri kwenye wizara ambazo siyo za muungano. Kuna wanafunzi kibao wanasom shule za msingi huku bara ilhali elimu ya msingi siyo ya mwungano. Where do we draw the line? Tanganyika iwe bayana ndo mambo mengine yajadiliwe. Kwamba serikali tatu ni gharama zaidi kwangu mimi ni dhana dhaifu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mkuu nguruvi3,

Karibu sana katika mjadala; Nadhani pia umepata nafasi ya kusoma hoja zangu kadhaa kwenye bandiko #16 ambapo nilikuwa najibu hoja mbalimbali za mdau mwenzetu jp omuga; Kwa kifupi, hoja zangu kwenye bandiko hilo zilikuwa ni my first presentation kwa kina on where I satdn kuhusiana na subject matter, lakini pia nililenga kusisitiza kwamba nia yangu hapa hailengi sana kujadili mambo ambayo tayari ni redundant i.e. faida na hasara za muungano kwa Tanganyika na Zanzibar kwani suala hili tayari tumeshalijadili kwa kina sehemu mbalimbali kama vile kwenye Duru za Siasa n.k; Ninacholenga katika mjadala huu ni kutoa fursa kwetu sote watanganyika kutafuta majibu juu moja kuu, nalo ni Je:

· Sumu ya Muungano ni ipi kati ya haya mawili: Je ni Kwa Kuikataa Serikali Ya Tanganyika au Ni Kwa Kuikubali Serikali ya Tanganyika?

Niseme tu kwamba sasa nazidi kuelewa fika kwamba katika kujadili swali hili, sio rahisi kuepuka mjadala kuhusu faida na hasara za muungano kwa pande zote mbili za Muungano, lakini bado nadhani kwamba tunaweza kufanya hoja hizi za faida na hasara zikawa ni side notes za kujadili hoja kuu, na sio main notes; Lakini naelewa jinsi gani ni vigumu kufanikisha kwani suala zima lipo very intricate, kama sio very complicated; All that said and done, kuna hoja nyingi za msingi ambazo umezijadili na naomba univumilie maana bandiko langu litakuwa ni refu kidogo; Ningependa nianze kwa kujadili swali lako muhimu kwenye bandiko lanko #23 ambapo umeuliza:

kwanini tujifunge katika muungano na tusifikirie option zingine?
Kuna tatizo gani tukienda EAC tukalinda interest zetu kwa pamoja kila mmoja akiwa na nchi yake?
Kwanini uhusiano wetu wa muda mrefu ujengwe katika katiba na isiwe kama ilivyokuwa mwaka 1964 au kabla?

Kwanza, nadhani tunakubaliana kwamba njia nzuri ya kuelewa kero za muungano ni kwa kurejea mkataba wa muungan00, 1964; Kama tupo sawa katika hili, kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, lengo lilikuwa ni kuja na federation (shirikisho) yenye serikali tatu, sio serikali mbili. Serikali mbili ni sera ya CCM, ambayo ni zao la ndoa ya TANU na ASP; Kumbuka, katika mkataba wa muungano, vyama vya siasa havikutajwa, hivyo kufanya ulazimishaji wa sera ya CCM juu ya mfumo wa muungano, kupitia Katiba ya JMT (1977) kuwa batili; Kuna ushahidi mwingi tu kwamba lengo lilikuwa ni shirikisho, kwa mfano, ukiangalia vifungu ndani ya Mkataba wa Muungano (1964), hasa kwa kutazama yale Masuala Kumi na Moja ya Muungano kwa Mujibu wa Mkataba wa Muungano (1964), ni rahisi kubaini kwamba dhamira ilikuwa ni Serikali tatu – ya kwanza ikiwa ni ile ambayo ingeshughulikia maeneo machache sana (masuala kumi na moja), serikali ya pili ikiwa inashughulika masuala ambayo hayakutajwa katika masuala yale kumi na moja lakini bado yapo Tanganyika (mfano Elimu, Afya, Kilimo n.k), na serikali ya tatu isimame yale nje ya muungano ambayo yapo Zanzibar, kama ilivyokuwa kabla ya 1964; Nashukuru kwamba umeonyesha kukubaliana name katika hili;

Kama tupo pamoja hadi hapa, basi ni rahisi sana kubaini kwamba malalamiko yote kuhusiana na Zanzibar kuwa mzigo kwa Tanganyika yana historia yake ndefu na sio sahihi sana kuwalaumu wazanzibari kwa hilo; Hii ni kwa sababu, historia inatuonyesha kwamba ni Tanganyika (kupitia urais wa Muungano), ndio ilianza mchezo wa kuchakachua mkataba wa muungano kwa kuzidi kuongeza orodha ya masuala la muungano nje ya makubaliano ya muungano (1964); Kwa mfano, kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, sehemu ya 5 (xi), inazungumza kwamba:

“Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha”;

Maswali langu kwako ni je:

· Hii haina maana kwamba Zanzibar walitarajiwa kuchangia sawa na Tanganyika?

· Nini kilitokea?

Ningepende kujadili hili. Twende mbali kidogo zaidi kwa kuangalia matukio mengine muhimu yaliyojitokeza mara tu baada ya muungano kusainiwa (1964); Kwanza, siku chache baada ya Muungano (1964) kusainiwa, ilitolewa decree titled “Amri ya Utaratibu wa Kipindi cha Mpito”, ambayo katika sehemu yake ya tisa (9) ikasema haya kama amri ya kutekelezwa mara moja:

“Mali zote na haki juu ya mali za Jamhuri ya Tanganyika, na mali zote na haki juu ya mali za Jamhuri ya watu wa Zanzibar zilizokuwa zinamilikiwa au kutumiwa au milikiwa kimsingi kuhusiana na mambo ya muungano, zitakuwa kuanzia siku ya muungano, chini ya jamhuri ya muungano.”

Mkuu nguruvi3, kumbuka kwamba taifa la Zanzibar ndio kwanza lilikuwa limetoka kwenye harakati za kujipatia uhuru wake, na halikuwa limeshafanya tathmini ya mali zake kama taifa, na vile vile, bado Zanzibar kama taifa jipya huru, halikuwa limeandaa Katiba yake mpya;

Matukio mengine yakazidi kuendelea kujitokeza, kwa mfano:

Kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, kipindi cha Aprili 26 1964 hadi Aprili 26 1965 kilikuwa ni kipindi cha mpito, na sehemu ya saba ya mkataba huo, ilitamka kwamba:

· Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamu wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar:
a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Muungano.
b) Ataitisha baraza la kutunga Katiba likiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itayoamuliwa likutane katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakari mapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya jamhuri ya muungano.

Lakini kinyume na makubaliano haya, mwezi kama mmoja hivi kabla ya expiry date ya utekelezaji wa suala hili la uundwaji wa baraza la Katiba, historia inatuonyesha kwamba kilichofuatia ni Katiba ya Muda (1965) ambayo ililenga kuhairisha utekelezaji wa mkataba wa muungano (1964) indefinitely. Cha ajabu zaidi ni kwamba, Katiba hiyo ya Muda ya mwaka 1965, ikamtangaza Rais wa Tanganyika kwamba atakuwa pia ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Hapa ndipo mzigo wa Zanzibar kwa Tanganyika ukawekewa viungo vya mapishi;

Kumbuka pia kwamba kufikia tarehe hii, tayari kulikuwa na makubaliano kwa mujibu wa Mkataba wa muungano (1964) kwamba kwa vile Zanzibar haikuwa na katiba yake tayari, tofauti na Tanganyika ambayo ilikuwa na katiba yake iliyopatikana mwaka 1962, basi Katiba ya Tanganyika ichukuliwe na kufanyiwa marekebisho ili itumike kama Katiba ya muda ya JMT kwa mwaka mmoja tu hadi pale baraza la katiba nililo jadili hapo juu litakapoteuliwa na marais wa pande zote mbili; Kwa maana hii, Katiba ya Tanganyika (1962) ingeendelea kusimamia masuala nje ya muungano kwa Tanganyika, Katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ingesimamia masuala ya muungano kwa mwaka mmoja, na Zanzibar ingeendelea na mchakato wake wa kujipatia katiba ili kusimamia masuala nje ya yale kumi na moja ndani ya ‘orodha ya masuala ya muungano’ per articles of the union, 1964. Specifically, mkataba wa muungano katika sehemu ya (5) ikaeleza kwamba:

· Sheria zote zilizopo Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumia katika maeneo yao.

Tukio lingine muhimu ambalo lilizidi kuweka chmvi na binzari katika upishi wa mzigo wa Zanzibar kwa Tanganyika ni pale Bunge (Dominated na TANU) lilipokuja na Muswada wa kufuta utambulisho wa Tanganyika kwa mujibu wa Sheria Namba 24 ya mwaka 1967 ambayo ikafuta rasmi utambulisho wa Tanganyika na kuzalisha utambulisho wa Tanzania Bara.

Iwapo tupo pamoja hadi sasa mkuu nguruvi3, utabaini kwa urahisi kwanini Zanzibar ikaishia kuwa tegemezi kwa Tanganyika, kinyume na makubaliano ya Mkataba wa Muungano, 1964;

Maswali yako kwenye bandiko #23 i.e:

kwanini tujifunge katika muungano na tusifikirie option zingine?
Kuna tatizo gani tukienda EAC tukalinda interest zetu kwa pamoja kila mmoja akiwa na nchi yake?
Kwanini uhusiano wetu wa muda mrefu ujengwe katika katiba na isiwe kama ilivyokuwa mwaka 1964 au kabla?

Maswali haya, kwa mtazamo wangu, yana sura mbili; Sura ya kwanza ni juu ya utegemezi wa Zanzibar kwa Tanganyika katika uendeshaji wa masuala ya muungano (mengi ambayo yapo nje ya mtabaka wa muungano, 1964) , na nimejaribu kujadili hilo earlier; Sura ya pili ni kuhusiana na options za mahusiano na ushirikiano baina ya Zanzibar na Tanganyika, nje ya muundo uliopo sasa;

Ningependa kujadili suala hilo kama ifuatavyo; Kwanza naomba niseme kwamba sipo hapa kumshambulia Mwalimu Nyerere kuhusiana na suala zima la muungano, badala yake, nia yangu ni kukosoa mtazamo wake kwamba ulikuwa na mapungufu, hasa kwa kuzingatia kwamba sina tatizo na NIA ya Mwalimu, tatizo langu ni juu ya UTEKELEZAJI WA NIA husika; Ndio maana always nimekuwa of an opinion kwamba:

‘Achievements za Mwalimu Nyerere hazikutokana sana na Success of His strategies (especially the Union and the Arusha Declaration), bali his ability to persuade donors as well as the population (Tanzania) kwamba his objectives were sincere; And indeed, they were sincere;’

All that said and done, sote tunafahamu kwamba Nyerere alikuwa ni mmoja wa waasisi wa wazo la United States of Africa, mwasisi mwingine akiwa ni Hayati Kwame Nkrumah; Kuna suala muhimu la kujadili hapa ambalo nadhani wengi hawana uelewa nalo wa kina; Katika suala la United States of Africa, kulikuwa na two schools of thoughts:

· Nkrumah’s school of thought au tuite Nkrumaism;
· Nyerere’s school of thought au tuite Nyerereism;

Tukianza na Nkrumah, yeye aliamini katika radical (fast) unionization of Africa – Afrika kuungana na kuwa moja immediately; Tukija kwa Nyerere, yeye aliamini katika incremental unionization of Africa, hasa kwa kupitia regional blocks kwanza, ili baadae hizi regional blocks ndio zije kuungana, hasa baada ya bara zima kukombolewa kutoka kwenye makucha ya mkoloni na mkaburu; Awali, Nyerere alionekana kuwa na mtazamo wa ovyo, huku Nkrumah akionekana ni shujaa wa mpya wa Africa; Lakini kwa jinsi miaka ilivyokuwa inasonga mbele, reliaty ikaanza kumsuta Nkrumah na kuweka Nyerere juu, na hali hii inaendelea kuwa hivyo hadi leo - – yani the route towards the United States of Africa kwa Version ya Mwalimu imekuwa proved ndio route sahihi kuliko ile ya Nkrumah; Kwa mfano, EAC, SADC, yote haya ni brainchild ya Mwalimu Nyerere;

Tukizidi kujikumbusha kidogo historia, in early 1960 kiliundwa chombo kwa jina la – Pan African Freedom Movement For East and Central Africa (PAFMECA). In PAFMECA, Nyerere ndiye aliyeonekana kuwa na ushawishi mkubwa kuliko wenzake. Kufuatia majadiliano ya kina baina ya viongozi wa nchi huru za kiafrika mjini Addis Ababa katika m,kutano mmoja, mkutano huo ulitoa msimamo ufuatao kupitia Mwalimu Nyerere (rejea gazeti la Tanganyika Standard, 16/11/1964):

“Wengi wetu tunakubali bila ya hoja kuwa shirikisho la nchi za Afrika Mashariki ni jambo linalokubalika; Tumesema hayo kwa imani kuwa mipaka ya nchi iliyopo hivi sasa imetengenezwa na mabeberu, na sio sisi wenyewe, na katika hali hiyo basi ipo kama kizingiti cha muungano baina yetu; Lazima tuikabili ofisi ya mkoloni na kudai uhuru sio wa Tanganyika, na baadae Kenya, Uganda na Zanzibar kila nchi peke yake, bali uhuru huo tuudai tukionesha sote ni wamoja kisiasa.”

Nguruvi3, katika hili unaweza pata tafsiri nyingi, binafsi nina mbili muhimu – kwanza, kama ilivyo Tanganyika, Zanzibar ilitambulika kama nchi kabla hata ya muungano, tofauti na hoja za wengi kwamba Zanzibar ni ndogo na iwe kama Mkoa n.k; Pili, Mwalimu alilenga shirikisho, kwa maana ya kwamba kila nchi ingeendelea kutambulika katika shirikisho husika kupitia serikali yake (mfano Tanganyika); Na Tatu ni kwamba Siasa zilipewa kipaumbele kuliko kitu kingine chochote, mfano rejea maneno “…tukionesha sote ni wamoja kisiasa…”; Hii ilikuwa ni dosari kubwa kwani kwani inaonyesha jinsi gani Mwalimu Nyerere alifanya maamuzi husika under the assumption kwamba shirikisho labarani afrika litatokana na umoja wa vyama vilivyopigania uhusu wa kisiasa kama vile TANU, KANU etc; Hakuangalia uwezekano wa shirikisho nje ya Umoja wa kisiasa, hasa huko mbeleni kwamba mapambano ya uhuru wa kiuchumi yangezaa vyama vingi vya siasa; Ndio maana ujio wa vyama vingi vya siasa nchini kidogo ulimpa wakati mgumu Mwalimu Nyerere kuhusiana na mfumo upi wa muungano ni bora katika muktadha wa vyama vingi vya siasa (kuanzia mwaka 1992), na ndio maana akamteua Jaji Bomani kuja na solution, of which ikawa ni kuiga mfumo wa mgombea mwenza kutoka federation ya USA; Tafsiri hapa ni kwamba, kwanza, kumbe mfumo wetu ulilenga federation system na sio unitary system, lakini pili, CCM iliahirisha (sio kuepuka) balaa la uwezekano wa nchi kuwa na Rais wa muungano kutoka chama kimoja cha siasa, huku Rais wa Zanzibar akitoka chama kingine cha siasa;

Katika mkutano mwingine wa PAFMECA 1963, Zanzibar ilijadiliwa (ingawa haikuhudhuria kwa vile bado ilikuwa sio nchi huru), na mkutano huo ukaja na tamko lifuatalo (source – ibid):

“Ingawaje Zanzibar haikuwakilishwa katika mkutano huu, inatulazimu tuseme wazi kuwa nayo inakaribishwa kujiunga na mkutano huu wenye lengo kuwa na shirikisho; Mara tu baada ya Zanzibar kumaliza taratibu za uchaguzi serikali yake itashirikishwa katika kufuatilia jambo hilo au kamati nyingine yoyote ile itakayoanzishwa katika kufikia lengo hilo la shirikisho.”

Kuna tafsiri nyingi hapa lakini kwa sasa nitaje moja tu – kwamba tunazidi kupata ukweli kwamba lengo la Mwalimu kuhusiana na muungano wetu lilikuwa ni muungano wa shirikisho,na ndani ya muungano huo wa shirikisho, kila taifa litakuwa linatambuliwa kuwa na serikali yake; Sasa nini kilifuatia baada ya Muungano 1964 ambapo Serikali ya Tanganyika ikatoweka?

Tukirudi nyuma kidogo – Mwalimu kupitia OAU, Julai, 1964 (kumbuka hii ni miezi mitatu baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar) alithibitisha kwa maneno yake mwenyewe akiwa na hamasa kubwa kwamba mfumo wa serikali moja au mfumo wa tangamano la majimbo usingefaa katika mazingira ya Kiafrika; Mara baada ya kikao hiki kumaliza, Mwalimu alitoa waraka mrefu na ambao ulipatiwa fursa ya kuchapishwa kwenye African Forum ambapo aliendeleza hoja yake hii ya msingi kwa kusema kwamba:

“Bara lenye ukubwa wake kamili, moja na lisilogawika, ndilo nataka liwepo; Hii haina maana huku ni kuwa na serikali moja kwa bara lote, katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote; Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja inayounganisha nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo Fulani Fulani; Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyenginezo, hizi zikiwa na mamlaka yaliyo hafifu kidogo, na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na katiba za ndani sio kutoka serikali kuu; Hii ni sawa na kusema kuwa afrika mpya inaweza kuwa ni dola ya shirikisho, ambayo nguvu zake zinagawiwa baina ya serikali kuu na serikali za mataifa washiriki kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo (Source: Julius K. Nyerere: The nature and requirements of African Unity” Katika African Forum Vol 1, Na. 1 (1965), ukusara 46. Kwa makala yote, soma kurasa 38 – 52;”

Mkuu nguruvi3, sidhani kama nahitaji kufafanua kwa kina nukuu ya mwalimu hapo juu watu kama Nape waelewe kwamba Mwalimu mtazamo wa Mwalimu kuhusiana na suala la mfumo wa muungano haukuwa static bali very dynamic kutegemeana na mazingira; Cha msingi hapa ni kwamba, idea ya Mwalimu ilikuwa ni Shirikisho la Afrika, shirikisho ambalo lingetambua serikali shiriki; Swali muhimu linalofuata ni je:

· Kwanini Mwalimu alikuja kugeuka baadae kuhusiana na mfumo wa muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar?

Honestly, sina majibu ya kujitosheleza kwa swali hili, ila ningependa kumalizia bandiko hili kwa kulijadili swali hili japo kidogo kama ifuatavyo:

Wakato wote, suala la Federation huwa linahitaji to adjust and adapt to competing objectives, lakini muhimu zaidi, to conflicting objectives; Kwa kawaida, federalism ina sura kuu mbili: Kwanza, federalism is instrunment of unity within states na hivyo ndivyo intra-state dimension arises; Sura ya pili ni kwamba, federalism is a means by which established states zinajaribu to forge closer relationships between states, na hivyo ndivyo inter-state dimension arises; Kutokana na hali hii, binafsi sishangai kwanini Mwalimu alijichanganya, hasa katika kipindi kile ambapo kulikuwa na two paths (options) za kutafuta maendeleo katika mataifa mpaya ya dunia ya tatu – yani options y akufuata Ujamaa/Ukomunisti na ile ya Ubepari;
 
Ni kwa kuikataa! Nyerere hakuwa Mungu! tena wakati anangatuka alisema yeye hakuwa mwema asilimia 100. Alisema alikuwa na mazuri yake na mabaya yake!
 
Mkuu Mchambuzi, kwanza shukurani kwa ufafanunuzi wako wa kina. Pili, nilichofanya ilikuwa si kurejea kwa faida au hasara za muungano bali kujibu hoja zako na za Jp Omuga. Kwa bahati mbaya mambo yapo so intertwined na ni rahisi ku-veer off the road hata katika umakini.

Nichangie kuwa sumu ya muungano kwa sasa ni kuikataa Tanganyika ndani ya muungano.
Sumu hiyo ilianza tangu muungano wa mwaka 1964 ulipoafikiwa huku kukiwa na ahadi za kufanya mabadiliko na marekebisho bila kutokea kama ilivyotarajiwa au kukusudiwa.

Ninapotofautiana nawe ni penye hoja kuwa nia njema ilikuwepo isipokuwa kulikuwa na recklessness katika utekelezaji ambao ulizaa mvurugano na kupotea kwa Tanganyika huku Znz ikiwa tegemezi. Kwa upande wangu nia pekee haikutosha, kulitakiwa kuwepo na ridhaa ya wenye nchi kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa muungano.

Pili muungano ulifanyika haraka sana bila kufuata Nyerereism school of thought. Ni wazi kilichochagiza ni political instability bila kuwa na usahihishaji wa kosa baadaye.
Tumeendelea kuishi na undefined hybrid hadi leo.

Nikijadili school of thoughts katika mada hii, nitaanaza na ya Nkrumah ambayo ilikuwa ni radical ya kuamka asubuhi moja na kuwa na United states of Africa. Hili lisingewezekana kwasababu kulikuwa na post independence euphoria iliyoambatana na pride na power struggle, mfano mzuri ni wa Kenya kukataa EAC 1963 Nyerere alipo propose.

Kosa hilo alitaka kulirudia Ghadaffi kwa kuua OAU na kuunda AU kuelekea United states of Africa kwa kujua kuwa post independence euphoria imeondoka na kusahau kuwa kulikuwa na political instability na power struggle in Africa.

Nyerereism ililenga kujenga ushirikiano wa kikanda kabla ya wa Africka.
Sababu ilikuwa ni kuanza kuelewana katika kanda na kuwa rahisi kuunganish kanda zilizoelewana.

Mfano, ni rahisi sana kuunganisha EAC na ECOWAS au SADC kuliko individual states
.Dhana hii ililenga mataifa mengi kwa ukanda pengine zaidi ya mawili, ingawa kuanzia na mawili ingekuwa jambo jema.

Naipenda Nyerereism kuliko Mkrumahism na nitaziunganisha na hoja yetu ya muungano.
Tulikusudia shirikisho mwaka 1964 chini ya article of union iliyokuwa na mambo 11.
Kwasababu kulikuwa na mutual agreement ya viongozi na si watu, yuliishia kupata undefined structure kwa miaka 50. Kwa bahati mbaya tunataka kurudia kosa hilo mwaka 2013.

Tukiangalia ukiukwaji wa akubaliano mbali mbali kama 1965,1967,1977 kama ulivyoainisha hapo juu na kwa kuzingatia ukweli kuwa mambo yaliyokubaliwa kama shirikisho yalikuwa 11 na rasimu ya sasa imepunguza hadi 7 na bado hatuna makubaliano, ni wazi kuwa shirikisho haliwezekani.
Na hapa Nyerereism ime feli kwa mataifa mawili.

Kufeli kunatokana na Tanganyika na Zanzibar zimekuwa na repelling forces zaidi ya attractive forces kutokana na wanasiasa kama nilivyoeleza jana. Lakini kufeli si 100% bado kuna nafasi ya Nyerereism kwa njia mbadala.

Kwanza, tuvunje muungano ili twende EAC ambako kuna nchi kubwa kama Tanzania na ndogo kama Zanzibar. Kutakuwa na nchi 6, 3 zikiwa ndogo na 3 zikiwa kubwa na hivyo kuondoa kabisa antagonism. Tanganyika haitaiona Zanzibar ndogo kwasababu ipo Rwanda na Burundi, na wala haitajiona kubwa kwasababu zipo Kenya na Uganda.

Automatic tutaweza ku-iron out the differences ambazo hatuwezi kuziondoa kwasasa kwakuwa kuna upinzani kati ya mkubwa na mdogo.

Ili kutimiza azama ya shirikisho kuna mambo tunapaswa kufanya
1. Kusahihisha makosa kwa kuuliza wananchi kama wanahitaji muungano wa Tanganyika na Zanz
2. Kuwauliza wangependa tuwe na uhusiano gani kama watataka, au tuvunje kama hawataki

3.
(i)Wakikubali tuanze na shirikisho la serikali 3
(ii)Wakikataa twende EAC au SADC ambako ni rahisi kushiriki zaidi ya pande zetu mbili.

Nimalizie kwa kusema kama kuna makosa tunarudia ni kurejea tu jinsi shirikisho lilivyokusudia awali, na jinsi tunavyoweza kusuluhisha tofauti bila kuuliza wananchi kama wapo tayari au la.

Irrespective of what is going on in political landscape , the return of Tanganyika is mutate mutandis

Nguruvi3, nadhani kama nimekusoma kuhusu wapi tunapishana, nadhani ni kwenye neno "NIA" ya muungano; naelewa hoja yako msingi, pengine niseme basi kulikuwa na enough justification for the said federation, hasa iwapo tunakubaliana na kwanza, umuhimu wa kuja kwa united states of africa, lakini kwa nyerereism approach, not nkrumah's approach kwa sababu ambazo umezijadili kwa kina hapo juu ambazo naziafiki; Je, kuhusu justification, hapo tunapishana?

Nikirudi kwenye nia, nadhani nipo nawe iwapo hoja yako ya msingi ni kwamba mchakato uliotumika kufikia maamuzi ya Muungano unaonyesha ukosefu wa nia thabiti kwani kuna ushahidi mwingi kwamba umma haukushirikishwa;

Suala participation ya umma wa pande zote mbili liliwahi kujadiliwa huko nyuma, hasa iwapo BMZ kwa upande wa znz lilipitisha na kutunga sheria kukubali muungano kama vile bunge kwa upande wa tanganyika inavyoelezwa kwamba lilifanya; Kwa mfano, mwanasheria mkuu wa zamani wa znz, wolfang dorado aliwahi nukuliwa akisema wazi kwamba kwa kadri ajuavyo, hakuna sheria yoyote iliyopitisha makubaliano hayo ya muungano ambayo ipo katika vitabu vya sheria vya zanzibar, na aboud jumbe amelijadili hili pia huko nyuma;

Kwa upande mwingine, issa shivji nae amethibitisha kutokuwepi kwa tangazo katika gazeti lolote la serikali juu ya kupitishwa kwa mkataba wa muungano, na anasisitiza kwamba hii inadhihirisha kwamba hakuna sheria ya aina hiyo iliyochapishwa katika gazeti lolote la serikali znz; Shivji anaeleza kwamba kwa upande wa Tanganyika, kuna tangazo rasmi la serikali lilitoka, tangazo namba 243 la Mei 1, 1964 lenye sahihi ya mwanasheria mkuu wa serikali wa wakati huo; Kwa mujibu wa shivji, tangazo hilo lilisema kwamba sheria ya kuafiki mkataba wa muungano ilitungwa na BMZ kwa mashirikiano na baraza la mawaziri aprili 25, 1964; Lakini tangazo hilo halikuthibitisha mamlaka yoyote husika katika kunukuu hayo; kwa kifupi, suala zima linaacha maswali mengi kuliko majibu, hasa juu ya ushiriki wa wazi wa wananchi au wawakilishi wa pande zote mbili za muungano;

Nina maswali matatu ambayo ninngependa kusikia maoni yako:

*Je, unavyouona muungano wetu ulivyo kwa sasa (kisheria), kuna fursa yoyote ya nchi shiriki kujitoa iwapo inahisi hakuna faida inayopatikana kwa watu wake?

*Je, unadhani ccm itafanya maamuzi gani kuhusiana na mfuno wa muungano ndani ya katika mpya na nini kitatokea as a result? Jaribu to time travel kidogo assuming unaweza predict move ya ccm;

*Mwisho, je, unadhani chama kama chadema kinaweza tumia suala la Tanganyika as a political assest towards 2015? Je kufanya hivyo ni kitu sahihi kwa chadema au sio kitu sahihi? Kwanini?
Kuhusu the right track kuelekea muungano imara, nakubaliana na hoja zako zote hapo juu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nguruvi3.

kama utautazama kwa kina kabisa Muungano wenu bila kuweka hata chembe ya ushabiki kushabikia upande wowote wa Mvungano huo utagundua kuwa SUMU KUBWA YA MUUNGANO WENU NI VIONGOZI WENU KUWA NA SIRI KATIKA MUUNGANO HUO KIASI CHA KUPELEKEA HATA HATI YA MUUNGANO KUWA SIRI KWA WANANCHI WA KAWAIDA NA HATA KWA SERIKALI ZENYEWE.

Usiri huo ndio unazaa hayo yote yanayotokea hivi sana.

Ok all in all tusubiri tu kuona kesi hiyo iliyofunguliwa huko Znz na waznz kudai hati ya muungano. Kwani hapo itafungua mengi.

mengine nitajadili baadayn nikinafasika.

pole sana Ahali yangu
 
Nguruvi3, nadhani kama nimekusoma kuhusu wapi tunapishana, nadhani ni kwenye neno "NIA" ya muungano; naelewa hoja yako msingi, pengine niseme basi kulikuwa na enough justification for the said federation, hasa iwapo tunakubaliana na kwanza, umuhimu wa kuja kwa united states of africa, lakini kwa nyerereism approach, not nkrumah's approach kwa sababu ambazo umezijadili kwa kina hapo juu ambazo naziafiki; Je, kuhusu justification, hapo tunapishana?

Nikirudi kwenye nia, nadhani nipo nawe iwapo hoja yako ya msingi ni kwamba mchakato uliotumika kufikia maamuzi ya Muungano unaonyesha ukosefu wa nia thabiti kwani kuna ushahidi mwingi kwamba umma haukushirikishwa;

Suala participation ya umma wa pande zote mbili liliwahi kujadiliwa huko nyuma, hasa iwapo BMZ kwa upande wa znz lilipitisha na kutunga sheria kukubali muungano kama vile bunge kwa upande wa tanganyika inavyoelezwa kwamba lilifanya; Kwa mfano, mwanasheria mkuu wa zamani wa znz, wolfang dorado aliwahi nukuliwa akisema wazi kwamba kwa kadri ajuavyo, hakuna sheria yoyote iliyopitisha makubaliano hayo ya muungano ambayo ipo katika vitabu vya sheria vya zanzibar, na aboud jumbe amelijadili hili pia huko nyuma;

Kwa upande mwingine, issa shivji nae amethibitisha kutokuwepi kwa tangazo katika gazeti lolote la serikali juu ya kupitishwa kwa mkataba wa muungano, na anasisitiza kwamba hii inadhihirisha kwamba hakuna sheria ya aina hiyo iliyochapishwa katika gazeti lolote la serikali znz; Shivji anaeleza kwamba kwa upande wa Tanganyika, kuna tangazo rasmi la serikali lilitoka, tangazo namba 243 la Mei 1, 1964 lenye sahihi ya mwanasheria mkuu wa serikali wa wakati huo; Kwa mujibu wa shivji, tangazo hilo lilisema kwamba sheria ya kuafiki mkataba wa muungano ilitungwa na BMZ kwa mashirikiano na baraza la mawaziri aprili 25, 1964; Lakini tangazo hilo halikuthibitisha mamlaka yoyote husika katika kunukuu hayo; kwa kifupi, suala zima linaacha maswali mengi kuliko majibu, hasa juu ya ushiriki wa wazi wa wananchi au wawakilishi wa pande zote mbili za muungano;

Nina maswali matatu ambayo ninngependa kusikia maoni yako:
*Je, unavyouona muungano wetu ulivyo kwa sasa, kuna fursa yoyote ya nchi shiriki kujitoa iwapo inahisi hakuna faida inayopatikana kwa watu wake?

*Je, unadhani ccm itafanya maamuzi gani kuhusiana na mfuno wa muungano ndani ya katika mpya na nini kitatokea as a result? Jaribu to time travel kidogo assuming unaweza predict move ya ccm;

*Mwisho, je, unadhani chama kama chadema kinaweza tumia suala la Tanganyika as a political assest towards 2015? Je kufanya hivyo ni kitu sahihi kwa chadema au sio kitu sahihi? Kwanini?
Kuhusu the right track kuelekea muungano imara, nakubaliana na hoja zako zote hapo juu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Umezungumza vizuri sana.

Unajuwa mpaka sasa wananchi wa nchi hizo ni vipofu kuhusu muungano huo hakuna aliewahi kuona hati hiyo ya muungano iliyosainiwa na maraisi wa nchi hizo mbili bali tunabaki kujadili kitu tusikuwa na uhakika nacho. Cha msingi kwanza ni kuona HATI HIYO YA MUUNGANO iliyosainiwa na marais wa nchi hizo mbili huru zilizoungana iliyofichwa kama ipo kisha ndio mengine yafuatwe.

Tuvute subra.
 
Tatizo ni kwamba watanzania (wanaokana utanganyika) tumekuwa trained and groomed kujiona kwamba sisi ni bora kuliko waafrika wengine wote; Pia, tumekuwa trained and groomed kusingizia wengine matatizo yetu; hivyo ndivyo tulivyofika tulipofika na hivyo ndivyo tutaanguka huko tuendako;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tatizo ni kwamba watanzania (wanaokana utanganyika) tumekuwa trained and groomed kujiona kwamba sisi ni bora kuliko waafrika wengine wote; Pia, tumekuwa trained and groomed kusingizia wengine matatizo yetu; hivyo ndivyo tulivyofika tulipofika na hivyo ndivyo tutaanguka huko tuendako;
Mchambuzi, sina uhakika unaongelea katika mizania gani, ninachofahamu ni kuwa hakuna Mtanganyika anayekataa Utanganyika. Kilichotokea yalikuwa ni mambo mawili au matatu
1. Kwanza Watanganganyika walijiona Watanzania kuliko Watanganyika katika soirit ya muungano. Kwamba ili mradi kufanya hivyo kulikuwa ni kuendeleza muungano ambao wao waliamini ni kitu kizuri basi hawakupenda kurudi nyuma

2. Ilikuwa ni awareness kuhusu utaifa wao. Na hapa narudia tena kuwa waliosaidia ku-sensitize ni wazanzibar kwa sababu ya kujivunia Uzanzibar wao. Pamoja na hayo elimu kubwa katika mitandao imesaidia sana watu kujitambua na kutambua kuwa umuhimu wa Tanganyika ni mkubwa kuliko waakti mwingine. Nguvu hiyo ndiyo inafanya hata makubaliano ya sasa ya muungano yawe magumu sana. Mtanganyika hakubali tena ili hali ya kuwa yeye ndiye mwenye wajibu wa muungano.

3. Viongozi kama akina Nape wanotisha kuhusu ujio wa Tanganyika wanapeleka conflicting message kwa wananchi.
Kumbuka robo tatu ya raia hakuwahi kuishi katika Tanganyika na nusu yao hawajasoma hsitoria ya Tanganyika wakaielewa kwahiyo ni rahisi sana kuamini kuwa @Nape Nanuye anawaambi dude la kutisha sana

Nakuhakikishia kuwa leo 2013 Tanganyika ina wapenzi wengi sana kuliko ilivyokuwa mwaka 2010. Nilishangaa watu kufikiria wimbo wa taifa wa Tanganyika uitwe 'tazama ramani' tena wanauomba hapa mtandaoni. Nimeshangaa kuona bendera ya Tanganyika inarudi na watu wanajivunia. Kwahiyo Utanganyika umeshika kasi sana na hilo ni jambo jema linalosuniri muda kutimia.

Mimi binafasi natamani Tanganyika irudi ikiwa ndio njia rahisi sana ya kuachana na Zanzibar. Sioni faida za muungano huu hata kidogo hasa kwa Mtanganyika.

cc JokaKuu Jasusi
 
Nguruvi3,
*Je, unavyouona muungano wetu ulivyo kwa sasa (kisheria), kuna fursa yoyote ya nchi shiriki kujitoa iwapo inahisi hakuna faida inayopatikana kwa watu wake?

*Je, unadhani ccm itafanya maamuzi gani kuhusiana na mfuno wa muungano ndani ya katika mpya na nini kitatokea as a result? Jaribu to time travel kidogo assuming unaweza predict move ya ccm;

*Mwisho, je, unadhani chama kama chadema kinaweza tumia suala la Tanganyika as a political assest towards 2015?
Je kufanya hivyo ni kitu sahihi kwa chadema au sio kitu sahihi? Kwanini?
Kuhusu the right track kuelekea muungano imara, nakubaliana na hoja zako zote hapo juu;
Mchambuzi, kuna fursa za kisheria za mshirika wa muungano kujitoa. Kwabahati mbaya au nzuri kulingana na upande mtu atakaochukua, fursa hizo zinafungamana sana na siasa za nchi, vyama na madaraka ya kisiasa.

Kwa mfano, kuna fursa ya wabunge kupeleka miswada ambayo technically haitasema kuvunja muungano lakini implimentation yake ni kuvunja muungano. Wabunge wa ZNZ ndani ya bunge letu wanaweza kufanya hivyo kwa kuondoa UCCM na UCUF kama hawaoni faida za muungano

Pili, BLW linaweza kuwa na mswada na kujadili bila kuingiliwa kama walivyofanya katika mambo mengi.
Tatizo ni kuwa lazima wawe wamoja CUF na CCM na waungwe mkono na BML na SMZ.
Hapo ndipo penye utata. Still hoja siyo kuvunja muungano bali kuhitaji kura ya maoni itakayopelekea kujitoa

Kwa uapande wa Tanganyika, wabunge wake wanaweza kushinikiza uwepo wa serikali ya Tanganyika.
Serikali ya Tanganyika ambayo technically ndiyo imebeba muungano ina uwezo wa kuuvunja muungano huo na kujitoa kwa kukataa kubeba gharama za muungano peke yake.

Kwa hili nisema kuwa ukifuata vifungu vya sheria na katiba vilivyowekwa hili ni gumu sana kwasababu vifungu hivyo vimewekwa kwa makusudi ya kuzuia, lakini kuna loophole nyingi za ku circunmvigate na kujitoa katika muungano bila kurusha jiwe au risasi.

Kuhusu swali la Pili, kwasasa hivi CCM inataka serikali 2 kwa faida zake kisiasa .
Kinachofuata baada ya kufundisha mabaraza ya kata ni kuweka shinikizo kwa viongozi wa tume ya Warioba.
Hadi sasa tayari wameanza kuwatisha kuwa nchi inaingia katika matatizo kwasababu yao.

Halafu watatumia bunge la katiba kupitisha kwa nguvu rasimu ambayo wao wanaitaka.
Wanachotaka ni ku buy time kuwa rasimu ya mwisho iwe na option mbili ya serikali mbili na tatu.

Wakivuka kikwazo hicho basi watatumia bunge la katiba ambalo kwa namna lilivyokubaliwa litakuwa na wajumbe wengi wa CCM. Hoja itapitishwa kwa nguvu kuwa wananchi wanataka serikali 2.

Bunge la katiba litakuwa na CCM wengi ambao matamanio yao ni 2015. Wengi hawataweza kufanya maamuzi ambayo ni independent kwa faida ya nchi. Nguvu ya wapinzani itazimwa kwasababu bunge hilo litakuwa na spika wa CCM atakayerekebisha mambo. Kura itatumika sana kuzima hoja za upinzani

Kuhusu swali la tatu,
Chadema haiwezi tena kutumia hoja ya Tanganyika kama political assert. Chadema walipewa agenda na wananchi wakaitoa kwa CCM kwa sifa. JK alipotangaza mchakato wa rasimu ya katiba, jambo hilo halikuwa katika manifesto of election, halikujadiliwa na kikao chochote cha chama, it was solo move.

Mbowe akamsifia rais kwa kukubali kusikiliza hoja za rasimu ya katiba. Hakupaswa kufanya hivyo alipaswa kusimama kidete na kuhakikisha mchakato wa katiba unafuta taratibu zinazokubalika.

Hata vikao vya Ikulu vilikuwa katika hali hiyo hiyo na msimamo wa upinzani kuhusu maafisa tawala na wakuu wa wilaya kuwa sehemu ya mchakato ulitiwa nyongo na Mbowe.

Sababu kubwa ya JK kuanzisha mchakato ilikuwa kukwepa kiunzi cha muungano.
Alifahamu kuwa kama ajenda ikikbebwa na wapinzania uwezekano wa kufa muungano ni mkubwa.
Ndio maana unaona jitihada za mswada wa kuandika katiba zimejikita sana katika muungano

JK alijua kuwa kura ya maoni ilikuwa imminent na hilo lingevunja muungano hasa kwa kuzingatia kuwa wapinzani hawana cha kupoteza.

Sasa Chadema walipopoteza fursa za kusimamia mchakato wa katiba ambo ulikuwa katika manifesto yao tena wakisema katika siku 100 wataandika katiba mpya, ni wazi hawakuwa na mkakati wa kufanya hivyo bali maneno ya kisiasa. CDM hawawezi kurudi tena kwa Watanzania kuuza hoja waliyopewa wakaiuza kwa bei ya jusi pale Ikulu. Wananchi wanaona na wala wasidhani ni wajinga

Niseme it's immoral kwa Chadema kutumia suala la Tanganyika katika kutafuta uhalali wa kuingia Ikulu.
Imesha feli na haiwezi kuomba ridhaa ya kufelisha tena. Haina moral authority kuhusu katiba.

Nimalizie kwa kusema kuwa kwasababu ya kujitambua na kurudi kwa Tanganyika ambako hakuepukiki kwasasa kutokana na uelewa wa watu na hamasa ya utaifa wao hakuna muundo utakaotoa jibu rahisi la namna gani tuungane.

Njia pekee ni kura ya maoni. Nina uhakika kabisa kuwa waznz bado wanataka muungano ndio maana kila mara utasikia mkataba, serikali 3 au mbili na mivutano zaidi kuliko Tanganyika.
Tanganyika wameshatengeneza mind kuwa lazima Tanganyika irudi muungano kama itabidi.

Kunusuru muungano lazima serikali ianze kwenye kura ya maoni ili kujenga uhalali kuwa wananchi wanataka muungano halafu mengine yafuate.

Mchambuzi
nakuhakikishia kuwa suala hili baada ya miezi 3 litakuwa zito sana na linaweza kugharimu watu kazi au kuleta madhara.

Sasa hivi kuna two opposing forces, kuzileta pamoja unahitaji extra energy kama unavyoijua fizikia.
 
Nilipo REd.

kama umeisoma katiba ya Znz na ile ya JMTz ibara ya 19 kifungu cha 4 imebainisha wazi kabisa zote zimebainisha wazi kuwa BLW lina mamlaka ya kujadili mambo yale yasiyo ya muungano tu. Na mambo yote ya muungano na yale yanayokhusu upande wa Tanzania bara yanajadiliwa na Bunge la JMTz.

sasa muungano ni kitu cha Muungano BLW hawana mamlaka kukijadili.

Tuendelee sasa
 
Mchambuzi, sina uhakika unaongelea katika mizania gani, ninachofahamu ni kuwa hakuna Mtanganyika anayekataa Utanganyika. Kilichotokea yalikuwa ni mambo mawili au matatu
1. Kwanza Watanganganyika walijiona Watanzania kuliko Watanganyika katika soirit ya muungano. Kwamba ili mradi kufanya hivyo kulikuwa ni kuendeleza muungano ambao wao waliamini ni kitu kizuri basi hawakupenda kurudi nyuma

2. Ilikuwa ni awareness kuhusu utaifa wao. Na hapa narudia tena kuwa waliosaidia ku-sensitize ni wazanzibar kwa sababu ya kujivunia Uzanzibar wao. Pamoja na hayo elimu kubwa katika mitandao imesaidia sana watu kujitambua na kutambua kuwa umuhimu wa Tanganyika ni mkubwa kuliko waakti mwingine. Nguvu hiyo ndiyo inafanya hata makubaliano ya sasa ya muungano yawe magumu sana. Mtanganyika hakubali tena ili hali ya kuwa yeye ndiye mwenye wajibu wa muungano.

3. Viongozi kama akina Nape wanotisha kuhusu ujio wa Tanganyika wanapeleka conflicting message kwa wananchi.
Kumbuka robo tatu ya raia hakuwahi kuishi katika Tanganyika na nusu yao hawajasoma hsitoria ya Tanganyika wakaielewa kwahiyo ni rahisi sana kuamini kuwa @Nape Nanuye anawaambi dude la kutisha sana

Nakuhakikishia kuwa leo 2013 Tanganyika ina wapenzi wengi sana kuliko ilivyokuwa mwaka 2010. Nilishangaa watu kufikiria wimbo wa taifa wa Tanganyika uitwe 'tazama ramani' tena wanauomba hapa mtandaoni. Nimeshangaa kuona bendera ya Tanganyika inarudi na watu wanajivunia. Kwahiyo Utanganyika umeshika kasi sana na hilo ni jambo jema linalosuniri muda kutimia.

Mimi binafasi natamani Tanganyika irudi ikiwa ndio njia rahisi sana ya kuachana na Zanzibar. Sioni faida za muungano huu hata kidogo hasa kwa Mtanganyika.

cc JokaKuu Jasusi

Nguruvi3,

Mimi naomba nikudadavulie kidogo kukhusu muungano wake chanzo chake na muonekano wake kwa mujibu wa SHARIA.

Mzizi asili haswa wa muungano ni kauli, ya Nyerere na Karume.

Kilichofanyika ni kwa Nyerere na Karume tu kufikia makubaliano ya msingi (kwa hati ya dharura) na mambo mengine yakaburuzwa. Aidha, Mkataba huo wa Muungano ulitoa mwelekeo tu na kuacha mambo mengine muhimu kushughulikiwa baadaye na Tume ya Katiba ambayo chini ya Mkataba huo, ingeundwa katika muda usiozidi miezi 12 kuandaa Katiba ya Muungano. Katika kipindi hiki, Muungano uliendelea kutumia Katiba ya Tanganyika (kama ilivyorekebishwa) hadi hapo Muungano utakapopata Katiba yake.

Tunachofahamu ni kwamba, si Tume ya kupendekeza Katiba wala Bunge la Katiba (Constituent Assembly) lililoundwa au kuitishwa katika muda wa makubaliano hadi miaka 13 baadaye ilipotungwa Katiba ya kudumu ya 1977, kinyume na utaratibu unaotajwa kwenye Mkataba wa Muungano na Sheria ya Muungano.
Madhumuni ya kuunda Tume ya Katiba na Bunge la Katiba kipindi kile, yalikuwa ni kutoa nafasi kwa raia wa nchi hizi mbili kushiriki, kutoa maoni yao kuhusu aina ya Katiba ya Muungano wanayotaka, Muundo wa Muungano na mgawanyo wa madaraka ya kiutendaji ndani ya Muungano.

Kuna utata namna Katiba ya 1977 ilivyotungwa. Utaratibu unaotajwa katika Mkataba wa Muungano na Sheria ya Muungano unaelekea ulivunjwa kidogo, kwamba badala ya kuundwa Tume huru mahsusi kwa ajili ya kupendekeza Katiba, Tume ya vyama vya TANU na ASP ya watu 20 (ambayo haikuwa na Mwanasheria hata mmoja, bali wakereketwa wa siasa watupu), iliyoundwa mahsusi kuunganisha vyama hivyo viwili, iligeuzwa kuwa ndiyo Tume ya Katiba ya Chama na kupendekeza Katiba.

Mapendekezo ya Tume hiyo na ya Bunge la Katiba kama ilivyotakiwa, badala yake yaliwasilishwa na kujadiliwa kwenye Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama na baadaye kwenye Bunge la kawaida. Pamoja na hayo, Bunge hilo halikuyajadili mapendekezo ya "Tume" kwa sababu alizozitaja Waziri Mkuu wa wakati huo, Rashidi Kawawa, kwamba "Kwa kuwa NEC ilikuwa imeijadili, Bunge halikuwa na mamlaka ya kujadili wala kubadili kitu".

Utata wa Muundo wa Muungano ulijitokeza tena kama hoja wakati wa Tume ya Jaji Nyalali na kupatiwa suluhisho kwa njia ya mapendekezo ya kurekebisha Katiba. Lakini badala ya mapendekezo ya Tume hii makini kufanyiwa kazi, yalitiwa kapuni na hivyo kupoteza nafasi nyingine nzuri ya kutibu ugonjwa unaousumbua Muungano wetu.

Lakini, kwa nini Tume ya Katiba haikuundwa kwa mujibu wa Mkataba na Sheria ya Muungano? Moja ya sababu ni kwamba waasisi wa Muungano huo, Nyerere na Karume, walianza kugundua kwamba walikuwa tofauti mno kwa kila hali; kuanzia maumbile, kitabia na kifikra, elimu na mtazamo juu ya Muungano waliotia sahihi.

Nyerere " Sisi ni ndugu, kwa nini tusiungane?".
Karume " Tuungane, wewe rais. mimi makamo".

Shughuli ilianza na kumalizika in a split of a second!.

Kwa vile hizi ni nchi mbili tofauti zenye uhuru wake na zote ni Jamuhuri huru, kauli pekee haitoshi kuziunganisha, lazima kufuata taratibu, sheria na kanuni ili kuhalalisha nia na kauli hizo, ndipo zikaandaliwa hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.
Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

Kisharia Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.

sasa kazi kwako kusuka au kunyoa.

cc JokaKuu Jasusi
 
Tatizo ni kwamba watanzania (wanaokana utanganyika) tumekuwa trained and groomed kujiona kwamba sisi ni bora kuliko waafrika wengine wote; Pia, tumekuwa trained and groomed kusingizia wengine matatizo yetu; hivyo ndivyo tulivyofika tulipofika na hivyo ndivyo tutaanguka huko tuendako;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Kifupi au kwa lugha ya kistaharabu tunaweza kusema kuwa watanganyika wanaiga tarbia ya mbuni ya kuficha kichwa chake chini ya ardhwi akidhani kuwa amejificha haonekani kumbe mwili wote upo kweupeeeeeeeeeeee.

Jitambueni na mjikwamue kutoka katika utumwa huu wa akili.
 
Nilipo REd.

kama umeisoma katiba ya Znz na ile ya JMTz ibara ya 19 kifungu cha 4 imebainisha wazi kabisa zote zimebainisha wazi kuwa BLW lina mamlaka ya kujadili mambo yale yasiyo ya muungano tu. Na mambo yote ya muungano na yale yanayokhusu upande wa Tanzania bara yanajadiliwa na Bunge la JMTz.

sasa muungano ni kitu cha Muungano BLW hawana mamlaka kukijadili.

Tuendelee sasa
Ni kweli na ni hapana. Ni kweli kwa maandishi na hapana kwa vitendo.
Ulinzi na usalama ni suala nyeti la muungano. Kunakuwa na Amir Jeshi mmoja tu at any point in time.
BLW limemfanya rais wa znz kuwa Amir jeshi kwa njia nilizosema (circumnavigate) na kumuita mkuu wa vikosi maalum. Waemweza hata kumpa hadhi ya mizinga 21.

Baraza la mitihani ni suala la muungano, BLW limeweza kuanzisha baraza lao bila kufuata utaratibu na hawajakemewa.

Ndani ya BLW kuna wabunge wanaokwenda Dodoma. Hao wakiungana wanaweza kupeleka mswada kisheria kabisa. Kwa wakati huu wangeungwa mkono na wapinzani na baadhi ya CCM

Kuna njia ya kuondoa watendaji wa znz katika serikali ya muungano akiwemo makamu wa Rais. hakuna atakayeshtakiwa kwa hilo lakini automatic litakuwa limehitimisha muungano.
Sasa labda uniambie kwanini watumishi wa znz katika muungano hawajajaribu kulifanya hilo hata siku moja.

Tukiangalia mambo ya muungano ambayo znz imeyakiuka bila kuchukuliwa hatua ni mengi sana kiasi kwamba hili la kujitoa halina uzito.

Nimemijubu Mchambuzi kuwa kwenda kwa vifungu hilo haliwezekani kwasababu vipo vifungu mahususi kuzuia.
Lakini technically linawezekana kwa ku-circumnavigate kama walivyofanya znz mara nyingi sana na kufanikiwa kukiuka katiba ya muungano kiufundi na kwa nguvu.
 
Last edited by a moderator:

For some reaons, umenikumbusha maneno ya shivji katika article yake in
"Let the people speak: Tanzania down the road to neo-liberalism";

Anasema:

"If the union survived during karume era, it was because of two reasons:

a) Because zanzibar continued to have its own party;
b) Because Karume ignored constitutional restrictions on his power;

Pia kuna sehemu shivji anasame:

"...Karume however had no time for legal arrangements;he continued to exercise powers in complete disregard of union matters;Karume declared that there could not be elections in zanzibar for the next 50 years."

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

Kila wakti nakuhasa punguza ushabiki na jazba kwani sumu ktk mnakasha,
lakini hata haya maradhwi ya takriban wa Tanganyika wengi ya kupenda kunung'unika ndio kabisa yanaangamiza hata ktk mambo yenu na haki zenu za msingi.

Nimewahi bainisha hakuna dhambi mbaya kuliko ya kunung'unika na hiyo ndio inayowasibu waTanganyika. Kumbuka kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kunung'unika na kulalamika.

Kumbuka wa Znz wanalalamika sana na kupaza sauti zao wakati jirani zao wa Bara wananung'unika kimoyomoyo huku wanaumia.

Baada ya utangulizi huo naomba kukusaidia kisharia kuhusu madai yako kuwa Znz kuvunja katiba kwa kuwa na majeshi na mengineo.
Kumbuka kuwa Tz inaongozwa kwa utawala wa sharia. sasa kwa kutumia katiba ya JmTz wajibu wa kutii sharia za nchi, sharia ya 1984 na.15 ib.6 kifungu cha 1 na 2 kinakupa mamlaka mtu wajibu kufuata na kutii katiba, na na vile vile haki ya kufuata utaratibu uliowekwa na sharia, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya katiba na sharia za nchi.

Sasa acha kunungunika chukua hatua kwenda mahakamani kwayo kama walivyofanya waZnz kwenda mahakamani kuhoji kuhusu hati ya mvungano wenu.
 
Back
Top Bottom