Mkuu nguruvi3,
Karibu sana katika mjadala; Nadhani pia umepata nafasi ya kusoma hoja zangu kadhaa kwenye bandiko
#16 ambapo nilikuwa najibu hoja mbalimbali za mdau mwenzetu jp omuga; Kwa kifupi, hoja zangu kwenye bandiko hilo zilikuwa ni my first presentation kwa kina on where I satdn kuhusiana na subject matter, lakini pia nililenga kusisitiza kwamba nia yangu hapa hailengi sana kujadili mambo ambayo tayari ni redundant i.e. faida na hasara za muungano kwa Tanganyika na Zanzibar kwani suala hili tayari tumeshalijadili kwa kina sehemu mbalimbali kama vile kwenye Duru za Siasa n.k; Ninacholenga katika mjadala huu ni kutoa fursa kwetu sote watanganyika kutafuta majibu juu moja kuu, nalo ni Je:
· Sumu ya Muungano ni ipi kati ya haya mawili: Je ni Kwa Kuikataa Serikali Ya Tanganyika au Ni Kwa Kuikubali Serikali ya Tanganyika?
Niseme tu kwamba sasa nazidi kuelewa fika kwamba katika kujadili swali hili, sio rahisi kuepuka mjadala kuhusu faida na hasara za muungano kwa pande zote mbili za Muungano, lakini bado nadhani kwamba tunaweza kufanya hoja hizi za faida na hasara zikawa ni
side notes za kujadili hoja kuu, na sio
main notes; Lakini naelewa jinsi gani ni vigumu kufanikisha kwani suala zima lipo very intricate, kama sio very complicated; All that said and done, kuna hoja nyingi za msingi ambazo umezijadili na naomba univumilie maana bandiko langu litakuwa ni refu kidogo; Ningependa nianze kwa kujadili swali lako muhimu kwenye bandiko lanko
#23 ambapo umeuliza:
kwanini tujifunge katika muungano na tusifikirie option zingine?
Kuna tatizo gani tukienda EAC tukalinda interest zetu kwa pamoja kila mmoja akiwa na nchi yake?
Kwanini uhusiano wetu wa muda mrefu ujengwe katika katiba na isiwe kama ilivyokuwa mwaka 1964 au kabla?
Kwanza, nadhani tunakubaliana kwamba njia nzuri ya kuelewa kero za muungano ni kwa kurejea mkataba wa muungan00, 1964; Kama tupo sawa katika hili, kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, 1964, lengo lilikuwa ni kuja na federation (shirikisho) yenye serikali tatu, sio serikali mbili. Serikali mbili ni sera ya CCM, ambayo ni zao la ndoa ya TANU na ASP; Kumbuka, katika mkataba wa muungano, vyama vya siasa havikutajwa, hivyo kufanya ulazimishaji wa sera ya CCM juu ya mfumo wa muungano, kupitia Katiba ya JMT (1977) kuwa batili; Kuna ushahidi mwingi tu kwamba lengo lilikuwa ni shirikisho, kwa mfano, ukiangalia vifungu ndani ya Mkataba wa Muungano (1964), hasa kwa kutazama yale Masuala Kumi na Moja ya Muungano kwa Mujibu wa Mkataba wa Muungano (1964), ni rahisi kubaini kwamba dhamira ilikuwa ni Serikali tatu ya kwanza ikiwa ni ile ambayo ingeshughulikia maeneo machache sana (masuala kumi na moja), serikali ya pili ikiwa inashughulika masuala ambayo hayakutajwa katika masuala yale kumi na moja lakini bado yapo Tanganyika (mfano Elimu, Afya, Kilimo n.k), na serikali ya tatu isimame yale nje ya muungano ambayo yapo Zanzibar, kama ilivyokuwa kabla ya 1964; Nashukuru kwamba umeonyesha kukubaliana name katika hili;
Kama tupo pamoja hadi hapa, basi ni rahisi sana kubaini kwamba malalamiko yote kuhusiana na Zanzibar kuwa mzigo kwa Tanganyika yana historia yake ndefu na sio sahihi sana kuwalaumu wazanzibari kwa hilo; Hii ni kwa sababu, historia inatuonyesha kwamba ni Tanganyika (kupitia urais wa Muungano), ndio ilianza mchezo wa kuchakachua mkataba wa muungano kwa kuzidi kuongeza orodha ya masuala la muungano nje ya makubaliano ya muungano (1964); Kwa mfano, kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, sehemu ya 5 (xi), inazungumza kwamba:
Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini na kusimamiwa na idara ya forodha;
Maswali langu kwako ni je:
·
Hii haina maana kwamba Zanzibar walitarajiwa kuchangia sawa na Tanganyika?
·
Nini kilitokea?
Ningepende kujadili hili. Twende mbali kidogo zaidi kwa kuangalia matukio mengine muhimu yaliyojitokeza mara tu baada ya muungano kusainiwa (1964); Kwanza, siku chache baada ya Muungano (1964) kusainiwa, ilitolewa decree titled Amri ya Utaratibu wa Kipindi cha Mpito, ambayo katika sehemu yake ya tisa (9) ikasema haya kama
amri ya kutekelezwa mara moja:
Mali zote na haki juu ya mali za Jamhuri ya Tanganyika, na mali zote na haki juu ya mali za Jamhuri ya watu wa Zanzibar zilizokuwa zinamilikiwa au kutumiwa au milikiwa kimsingi kuhusiana na mambo ya muungano, zitakuwa kuanzia siku ya muungano, chini ya jamhuri ya muungano.
Mkuu nguruvi3, kumbuka kwamba taifa la Zanzibar ndio kwanza lilikuwa limetoka kwenye harakati za kujipatia uhuru wake, na halikuwa limeshafanya tathmini ya mali zake kama taifa, na vile vile, bado Zanzibar kama taifa jipya huru, halikuwa limeandaa Katiba yake mpya;
Matukio mengine yakazidi kuendelea kujitokeza, kwa mfano:
Kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, kipindi cha Aprili 26 1964 hadi Aprili 26 1965 kilikuwa ni kipindi cha mpito, na sehemu ya saba ya mkataba huo, ilitamka kwamba:
· Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kukubaliana na Makamu wa Rais ambaye ni kiongozi wa serikali ya Zanzibar:
a) Atateua tume kwa ajili ya kutoa mapendekezo kwa ajili ya katiba ya Muungano.
b) Ataitisha baraza la kutunga Katiba likiwa na wawakilishi kutoka Tanganyika na Zanzibar katika idadi itayoamuliwa likutane
katika kipindi cha mwaka mmoja tokea kuanza kwa muungano kwa madhumuni ya kutafakari mapendekezo ya tume iliyotajwa juu na kupitisha katiba ya jamhuri ya muungano.
Lakini kinyume na makubaliano haya, mwezi kama mmoja hivi kabla ya expiry date ya utekelezaji wa suala hili la uundwaji wa baraza la Katiba, historia inatuonyesha kwamba kilichofuatia ni Katiba ya Muda (1965) ambayo ililenga kuhairisha utekelezaji wa mkataba wa muungano (1964) indefinitely. Cha ajabu zaidi ni kwamba, Katiba hiyo ya Muda ya mwaka 1965, ikamtangaza Rais wa Tanganyika kwamba atakuwa pia ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Hapa ndipo mzigo wa Zanzibar kwa Tanganyika ukawekewa viungo vya mapishi;
Kumbuka pia kwamba kufikia tarehe hii, tayari kulikuwa na makubaliano kwa mujibu wa Mkataba wa muungano (1964) kwamba kwa vile Zanzibar haikuwa na katiba yake tayari, tofauti na Tanganyika ambayo ilikuwa na katiba yake iliyopatikana mwaka 1962, basi Katiba ya Tanganyika ichukuliwe na kufanyiwa marekebisho ili itumike kama Katiba ya muda ya JMT kwa
mwaka mmoja tu hadi pale baraza la katiba nililo jadili hapo juu litakapoteuliwa na marais wa pande zote mbili; Kwa maana hii, Katiba ya Tanganyika (1962) ingeendelea kusimamia masuala nje ya muungano kwa Tanganyika, Katiba ya Tanganyika iliyorekebishwa ingesimamia masuala ya muungano kwa mwaka mmoja, na Zanzibar ingeendelea na mchakato wake wa kujipatia katiba ili kusimamia masuala nje ya yale kumi na moja ndani ya orodha ya masuala ya muungano per articles of the union, 1964. Specifically, mkataba wa muungano katika sehemu ya (5) ikaeleza kwamba:
· Sheria zote zilizopo Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kutumia katika maeneo yao.
Tukio lingine muhimu ambalo lilizidi kuweka chmvi na binzari katika upishi wa mzigo wa Zanzibar kwa Tanganyika ni pale Bunge (Dominated na TANU) lilipokuja na Muswada wa kufuta utambulisho wa Tanganyika kwa mujibu wa Sheria Namba 24 ya mwaka 1967 ambayo ikafuta rasmi utambulisho wa
Tanganyika na kuzalisha utambulisho wa
Tanzania Bara.
Iwapo tupo pamoja hadi sasa mkuu nguruvi3, utabaini kwa urahisi kwanini Zanzibar ikaishia kuwa tegemezi kwa Tanganyika, kinyume na makubaliano ya Mkataba wa Muungano, 1964;
Maswali yako kwenye bandiko
#23 i.e:
kwanini tujifunge katika muungano na tusifikirie option zingine?
Kuna tatizo gani tukienda EAC tukalinda interest zetu kwa pamoja kila mmoja akiwa na nchi yake?
Kwanini uhusiano wetu wa muda mrefu ujengwe katika katiba na isiwe kama ilivyokuwa mwaka 1964 au kabla?
Maswali haya, kwa mtazamo wangu, yana sura mbili; Sura ya kwanza ni juu ya utegemezi wa Zanzibar kwa Tanganyika katika uendeshaji wa masuala ya muungano (mengi ambayo yapo nje ya mtabaka wa muungano, 1964) , na nimejaribu kujadili hilo earlier; Sura ya pili ni kuhusiana na options za mahusiano na ushirikiano baina ya Zanzibar na Tanganyika, nje ya muundo uliopo sasa;
Ningependa kujadili suala hilo kama ifuatavyo; Kwanza naomba niseme kwamba sipo hapa kumshambulia Mwalimu Nyerere kuhusiana na suala zima la muungano, badala yake, nia yangu ni kukosoa mtazamo wake kwamba ulikuwa na mapungufu, hasa kwa kuzingatia kwamba sina tatizo na NIA ya Mwalimu, tatizo langu ni juu ya UTEKELEZAJI WA NIA husika; Ndio maana always nimekuwa of an opinion kwamba:
Achievements za Mwalimu Nyerere hazikutokana sana na Success of His strategies (especially the Union and the Arusha Declaration), bali his ability to persuade donors as well as the population (Tanzania) kwamba
his objectives were sincere; And indeed, they were sincere;
All that said and done, sote tunafahamu kwamba Nyerere alikuwa ni mmoja wa waasisi wa wazo la
United States of Africa, mwasisi mwingine akiwa ni Hayati Kwame Nkrumah; Kuna suala muhimu la kujadili hapa ambalo nadhani wengi hawana uelewa nalo wa kina; Katika suala la United States of Africa, kulikuwa na two schools of thoughts:
· Nkrumahs school of thought au tuite Nkrumaism;
· Nyereres school of thought au tuite Nyerereism;
Tukianza na Nkrumah, yeye aliamini katika radical (fast) unionization of Africa Afrika kuungana na kuwa moja immediately; Tukija kwa Nyerere, yeye aliamini katika incremental unionization of Africa, hasa kwa kupitia regional blocks kwanza, ili baadae hizi regional blocks ndio zije kuungana, hasa baada ya bara zima kukombolewa kutoka kwenye makucha ya mkoloni na mkaburu; Awali, Nyerere alionekana kuwa na mtazamo wa ovyo, huku Nkrumah akionekana ni shujaa wa mpya wa Africa; Lakini kwa jinsi miaka ilivyokuwa inasonga mbele, reliaty ikaanza kumsuta Nkrumah na kuweka Nyerere juu, na hali hii inaendelea kuwa hivyo hadi leo - yani the route towards the United States of Africa kwa Version ya Mwalimu imekuwa proved ndio route sahihi kuliko ile ya Nkrumah; Kwa mfano, EAC, SADC, yote haya ni brainchild ya Mwalimu Nyerere;
Tukizidi kujikumbusha kidogo historia, in early 1960 kiliundwa chombo kwa jina la Pan African Freedom Movement For East and Central Africa (PAFMECA). In PAFMECA, Nyerere ndiye aliyeonekana kuwa na ushawishi mkubwa kuliko wenzake. Kufuatia majadiliano ya kina baina ya viongozi wa nchi huru za kiafrika mjini Addis Ababa katika m,kutano mmoja, mkutano huo ulitoa msimamo ufuatao kupitia Mwalimu Nyerere (rejea gazeti la Tanganyika Standard, 16/11/1964):
Wengi wetu tunakubali bila ya hoja kuwa shirikisho la nchi za Afrika Mashariki ni jambo linalokubalika; Tumesema hayo kwa imani kuwa mipaka ya nchi iliyopo hivi sasa imetengenezwa na mabeberu, na sio sisi wenyewe, na katika hali hiyo basi ipo kama kizingiti cha
muungano baina yetu; Lazima tuikabili ofisi ya mkoloni na kudai uhuru sio wa Tanganyika, na baadae Kenya, Uganda na Zanzibar kila nchi peke yake, bali uhuru huo tuudai tukionesha sote ni wamoja kisiasa.
Nguruvi3, katika hili unaweza pata tafsiri nyingi, binafsi nina mbili muhimu kwanza, kama ilivyo Tanganyika, Zanzibar ilitambulika kama nchi kabla hata ya muungano, tofauti na hoja za wengi kwamba Zanzibar ni ndogo na iwe kama Mkoa n.k; Pili, Mwalimu alilenga shirikisho, kwa maana ya kwamba kila nchi ingeendelea kutambulika katika shirikisho husika kupitia serikali yake (mfano Tanganyika); Na Tatu ni kwamba Siasa zilipewa kipaumbele kuliko kitu kingine chochote, mfano rejea maneno
tukionesha sote ni wamoja kisiasa
; Hii ilikuwa ni dosari kubwa kwani kwani inaonyesha jinsi gani Mwalimu Nyerere alifanya maamuzi husika under the assumption kwamba shirikisho labarani afrika litatokana na umoja wa vyama vilivyopigania uhusu wa kisiasa kama vile TANU, KANU etc; Hakuangalia uwezekano wa shirikisho nje ya Umoja wa kisiasa, hasa huko mbeleni kwamba mapambano ya uhuru wa kiuchumi yangezaa vyama vingi vya siasa; Ndio maana ujio wa vyama vingi vya siasa nchini kidogo ulimpa wakati mgumu Mwalimu Nyerere kuhusiana na mfumo upi wa muungano ni bora katika muktadha wa vyama vingi vya siasa (kuanzia mwaka 1992), na ndio maana akamteua Jaji Bomani kuja na solution, of which ikawa ni kuiga mfumo wa mgombea mwenza kutoka
federation ya USA; Tafsiri hapa ni kwamba, kwanza, kumbe mfumo wetu ulilenga federation system na sio unitary system, lakini pili, CCM iliahirisha (sio kuepuka) balaa la uwezekano wa nchi kuwa na Rais wa muungano kutoka chama kimoja cha siasa, huku Rais wa Zanzibar akitoka chama kingine cha siasa;
Katika mkutano mwingine wa PAFMECA 1963, Zanzibar ilijadiliwa (ingawa haikuhudhuria kwa vile bado ilikuwa sio nchi huru), na mkutano huo ukaja na tamko lifuatalo (source ibid):
Ingawaje Zanzibar haikuwakilishwa katika mkutano huu, inatulazimu tuseme wazi kuwa nayo inakaribishwa kujiunga na mkutano huu wenye lengo kuwa na
shirikisho; Mara tu baada ya Zanzibar kumaliza taratibu za uchaguzi
serikali yake itashirikishwa katika kufuatilia jambo hilo au kamati nyingine yoyote ile itakayoanzishwa katika kufikia lengo hilo la shirikisho.
Kuna tafsiri nyingi hapa lakini kwa sasa nitaje moja tu kwamba tunazidi kupata ukweli kwamba lengo la Mwalimu kuhusiana na muungano wetu lilikuwa ni muungano wa shirikisho,na ndani ya muungano huo wa shirikisho, kila taifa litakuwa linatambuliwa kuwa na serikali yake; Sasa nini kilifuatia baada ya Muungano 1964 ambapo Serikali ya Tanganyika ikatoweka?
Tukirudi nyuma kidogo Mwalimu kupitia OAU, Julai, 1964 (kumbuka hii ni miezi mitatu baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar) alithibitisha kwa maneno yake mwenyewe akiwa na hamasa kubwa kwamba mfumo wa serikali moja au mfumo wa tangamano la majimbo usingefaa katika mazingira ya Kiafrika; Mara baada ya kikao hiki kumaliza, Mwalimu alitoa waraka mrefu na ambao ulipatiwa fursa ya kuchapishwa kwenye
African Forum ambapo aliendeleza hoja yake hii ya msingi kwa kusema kwamba:
Bara lenye ukubwa wake kamili, moja na lisilogawika, ndilo nataka liwepo; Hii haina maana huku ni kuwa na serikali moja kwa bara lote, katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote; Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja
inayounganisha nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo Fulani Fulani; Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyenginezo, hizi zikiwa na mamlaka yaliyo hafifu kidogo,
na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na katiba za ndani sio kutoka serikali kuu; Hii ni sawa na kusema kuwa afrika mpya inaweza kuwa ni dola ya shirikisho, ambayo nguvu zake zinagawiwa baina ya serikali kuu na serikali za mataifa washiriki kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo (Source: Julius K. Nyerere: The nature and requirements of African Unity Katika African Forum Vol 1, Na. 1 (1965), ukusara 46. Kwa makala yote, soma kurasa 38 52;
Mkuu nguruvi3, sidhani kama nahitaji kufafanua kwa kina nukuu ya mwalimu hapo juu watu kama Nape waelewe kwamba Mwalimu mtazamo wa Mwalimu kuhusiana na suala la mfumo wa muungano haukuwa
static bali very dynamic kutegemeana na mazingira; Cha msingi hapa ni kwamba, idea ya Mwalimu ilikuwa ni Shirikisho la Afrika, shirikisho ambalo lingetambua serikali shiriki; Swali muhimu linalofuata ni je:
· Kwanini Mwalimu alikuja kugeuka baadae kuhusiana na mfumo wa muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar?
Honestly, sina majibu ya kujitosheleza kwa swali hili, ila ningependa kumalizia bandiko hili kwa kulijadili swali hili japo kidogo kama ifuatavyo:
Wakato wote, suala la Federation huwa linahitaji to adjust and adapt
to competing objectives, lakini muhimu zaidi,
to conflicting objectives; Kwa kawaida, federalism ina sura kuu mbili: Kwanza, federalism is instrunment of unity within states na hivyo ndivyo
intra-state dimension arises; Sura ya pili ni kwamba, federalism is a means by which established states zinajaribu to forge closer relationships between states, na hivyo ndivyo
inter-state dimension arises; Kutokana na hali hii, binafsi sishangai kwanini Mwalimu alijichanganya, hasa katika kipindi kile ambapo kulikuwa na two paths (options) za kutafuta maendeleo katika mataifa mpaya ya dunia ya tatu yani options y akufuata Ujamaa/Ukomunisti na ile ya Ubepari;