Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,324
Ni kweli na ni hapana. Ni kweli kwa maandishi na hapana kwa vitendo.
Ulinzi na usalama ni suala nyeti la muungano. Kunakuwa na Amir Jeshi mmoja tu at any point in time.
BLW limemfanya rais wa znz kuwa Amir jeshi kwa njia nilizosema (circumnavigate) na kumuita mkuu wa vikosi maalum. Waemweza hata kumpa hadhi ya mizinga 21.
Baraza la mitihani ni suala la muungano, BLW limeweza kuanzisha baraza lao bila kufuata utaratibu na hawajakemewa.
Ndani ya BLW kuna wabunge wanaokwenda Dodoma. Hao wakiungana wanaweza kupeleka mswada kisheria kabisa. Kwa wakati huu wangeungwa mkono na wapinzani na baadhi ya CCM
Kuna njia ya kuondoa watendaji wa znz katika serikali ya muungano akiwemo makamu wa Rais. hakuna atakayeshtakiwa kwa hilo lakini automatic litakuwa limehitimisha muungano.
Sasa labda uniambie kwanini watumishi wa znz katika muungano hawajajaribu kulifanya hilo hata siku moja.
Tukiangalia mambo ya muungano ambayo znz imeyakiuka bila kuchukuliwa hatua ni mengi sana kiasi kwamba hili la kujitoa halina uzito.
Nimemijubu Mchambuzi kuwa kwenda kwa vifungu hilo haliwezekani kwasababu vipo vifungu mahususi kuzuia.
Lakini technically linawezekana kwa ku-circumnavigate kama walivyofanya znz mara nyingi sana na kufanikiwa kukiuka katiba ya muungano kiufundi na kwa nguvu.
Nilitaka nikusaidie hapo nilipo BLUE.
Kama umesoma na kuelewa mambo ya muungano hususan kipengele hicho cha Ilmu. Utaona Tanganyika na Zanzibar mumeungana KATIKA ELIMU YA JUU TU SIO SECONDARY WALA PRIMARY LEVEL.
Kwa hiyo mamlaka ya Dr Shukuru Kawambwa nmwisho Chumbe kwani Znz wana waziri wao wa Elimu. Na ukitazama Mamlaka ya Dr Ndalichako na Baraza lake yapo chini ya wizara ya Ilmu ya Jmtz hivyo hana mamlaka Kisharia kuoperate Znz.
Na hata kama utatazama muundo wa Baraza hilo la Mitihani halijaundwa Kimuungano angali kwa kupitia Tovuti yake Muundo huo kisha linganisha na ile yenye sura ya muungano kama BOT n.k.
Zanzibar kisharia wana haki kamili kuunda baraza lao la Mitihani kwa mujibu wa sharia zote ile ya Znz na ile ya JMTz.
Pole sana punguza jazba na ushabiki