geraldkowero1
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 1,838
- 646
Shida Ya Watanzania Ukweli Hawautaki,sasa Kitendo Cha Kumpa Nafasi Mzungumzaji Mmoja Jukwaa Kuu Halafu Wengine Unasema Umeisha,hv Hapa Panahitaji Elimu Gani Kujua Mwenyekiti Kapwaya?
Sio kapwaya tu ila inaonekana wazi kakatiwa fungu. Mchanganyiko wa wasikilizaji na wadau waliokuwa pale kwa mwerevu aligundua miongoni mwao walikuwepo mamluki wa kulipwa kwa ajili ya kuzomea. Hii ni kuzidi kukididimiza chuo kikuu chetu kwani wahitimu wake watakosa uwezo wa kuelimisha wasio na elimu kubwa. Pia uwezo wao kusimamia wanayoyaamini utapungua sana na kukosa viongozi bora.Ni hatari kama jamii haitaona tofauti kiuwezo kati ya mhitimu wa chuo kikuu na raia ambae hajasoma. M/kiti wa mjadala mara nyingi alikuwa akishauriwa mara kwa mara baada ya kugundulika hana uwezo wa kumudu mdahalo ule. Uchaguzi wa wachangiaji ulipangwa na ndio maana walizomewa na kushindwa kuchangia kabisa.Nashukuru hawakuendelea kuchukua wachangiaja wengine kwani mdahalo ungevunjika na vurugu kutokea.Mmeona tofauti kubwa ya uendeshaji midahalo kati ya ule wa juzi wa Mwakitwange, wa jana uliomjumuisha prof. Lumumba toka Kenya na naamini hata wa kesho wa wajumbe wa kamati ya kukusanya maoni ya katiba. Mdahalo huo utarushwa live kesho 4/8na itv kuanzia saa 9 mchana. Wadau msikose kuuangalia.