Mdahalo wa Katiba (UDASA) kupitia Star TV - Agosti 3, 2014

Mdahalo wa Katiba (UDASA) kupitia Star TV - Agosti 3, 2014

Kwani wasira kavurugwa kama mpangala? Kama kuongeza serikali ni kuboresha demokrasia tufanye ziwe serikali tano au kanda zote ziwe na rais wake na mawaziri wakuu pamoja na makamu wa rais wake kama hiyo ndiyo hoja.

Hebu tueleze serikali mbili nizipi?

Zanzibar na nini? yapili ni ipi?
 
Katibaaa ikihairishwaaaa....ccm wanachukuaaa nchi tenaa....
 
Profesa Gaudence Mpangala wa RUCO Iringa ameanza kuzungumza.Anasema mara baada ya wabunge wa UKAWA kutoka nje ya BMK yeye,Prof .PLO Lumumba na Prof. mwingine wa UDSM walifanya utafiti.Utafiti wao ulihusu chanzo cha mkwamo huo na utatuzi wake ni nini?.Waliuliza wadau mbali mbali na wakagundua chanzo ni sababu 5.Sababu hizo ni 1. kutozingatia misingi ya sheria inayoelekeza mchakato wa uundaji wa katiba mpya 2. Kuibeza na kuiponda Tume pamoja na uzinduzi wa BMK kwa rais kuzindua 3.Mazingira ya mjadala yalighubikwa na kubeza na kukashifiana 4.Kutokana na sababu hizo 3 UKAWA walitoka nje 5.Mapungufu ya sheria iliyounda mabadiliko ya katiba ambapo bunge maalum limejaa wanasiasa. Kuhusu UTATUZI amesema vitu vitano 1.Rasimu iliyotokana na wananchi wa Tanzania ndiyo ijadiliwe2.UKAWA warudi bungeni na wajadili rasimu iliyoletwa na Warioba 3.Wabunge wote watakaorejea waweke utaifa mbele na waache kujali vyama na kubezana.TANESCo wamechukua umeme

safi sana. Hii ndio reporting inayotusaidia tulio machakani. Umeme ukirudi endelea kutujuza mkuu. Sina tv nina nokia asha
 
Profesa Gaudence Mpangala wa RUCO Iringa ameanza kuzungumza.Anasema mara baada ya wabunge wa UKAWA kutoka nje ya BMK yeye,Prof .PLO Lumumba na Prof. mwingine wa UDSM walifanya utafiti.Utafiti wao ulihusu chanzo cha mkwamo huo na utatuzi wake ni nini?.Waliuliza wadau mbali mbali na wakagundua chanzo ni sababu 5.Sababu hizo ni 1. kutozingatia misingi ya sheria inayoelekeza mchakato wa uundaji wa katiba mpya 2. Kuibeza na kuiponda Tume pamoja na uzinduzi wa BMK kwa rais kuzindua 3.Mazingira ya mjadala yalighubikwa na kubeza na kukashifiana 4.Kutokana na sababu hizo 3 UKAWA walitoka nje 5.Mapungufu ya sheria iliyounda mabadiliko ya katiba ambapo bunge maalum limejaa wanasiasa. Kuhusu UTATUZI amesema vitu vitano 1.Rasimu iliyotokana na wananchi wa Tanzania ndiyo ijadiliwe2.UKAWA warudi bungeni na wajadili rasimu iliyoletwa na Warioba 3.Wabunge wote watakaorejea waweke utaifa mbele na waache kujali vyama na kubezana.TANESCo wamechukua umeme

Tangu nianze kufatilia hii Mada wewe ndg ndio umekiwa mtu wa kwanza kuwa msaada kwa walio mbali na.TV tunakishukuru sana hoa.wengine wanamwagika POVU tu,,,,!!!!
 
kwa mtazamo wa wasira ndio maana rais anayumba kwenye misimamo yake anahitaji washauri lakini sio wasira na lukuvi.
 
Kwani kitila ametoka lini ukawa kama zitto ni ukawa kwa nini kitila asiwe ukawa anashiriki vikao vya ukawa kila siku.

Ulitaka Aongee maelezo ya Wassira?

Hebu kwa kifupi kabisa tuambie Wassira kaongea hoja zipi? walau tatu.... zaid ya kutolea macho Tundu Lisu?
 
kitila anasema wajumbe wa BMK hawana weledi na uwezo wa kutengeneza katiba kinyume na tulivyotarajia. anashauri jk ahimizwe ili atumie mianya ya kisheria kulisimamisha bmk
 
Dr.Mkumbo sasa anaongea kama Zito.anataka marekebisho ya katiba iliyopo iruhusu umri wa urais upunguzwe.
 
Kuna propaganda na siasa uchwara zinafanywa humu jukwaani na mitandao mingine na waganga njaa eti ccm imesomba watu na kuwapeleka kwenye mdahalo nkrumah.huu ni uzushi mtukufu na ni mwendelezo wa siasa mufilisi. Ccm sio saccos kama hizo zenu wala sio chama cha ukoo. Ni taasisi iliyojengeka miaka na miaka yenye mfumo wake maalum ambao watanzania wote wameukubali na kukipenda chama hiki.

nawataka hao waganga njaa mitandaoni watambue kuwa wameshindwa mapema mno.
 
mjadala una wahudhuriaji wengi lakini uko undercontrol.ule wa wanywa viroba unakuwaga na fujo sana.
 
Back
Top Bottom