Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,235
- 4,252
Idadi kubwa ya Waafrika wanaamini kuoa au kuolewa ni kufanikiwa maisha ndiyo maana neno ndoa limekuwa likipigiwa kelele kila kona huku maswali ya kuoa au kuolewa yakizidi kusumbua akili za watu wanaoulizwa au kuwakera ikitegemea na namna mtu anavyochukuliwa
Ukweli ni kuwa Kuoa au Kuolewa sio kufanikiwa maisha bali ni kitendo cha kutafutia watu wengine maisha ambao watakuwa watoto wako
Kuoa au kuolewa sio kufanikiwa maisha kwasababu hakuna faida unayoingiza zaidi ya kutoa matumizi maanake ni kuwa unafanya jambo la hasara au kwa maana nyingine kutoa sadaka
Ingelikuwa ni biashara ndipo ungesema unaingiza faida
Unapopata watoto maana yake ni kuwa kazi yako uliyofanya ni kuwaleta duniani watu wapya na uhakikishe unawatafutia maisha tangu wakiwa vijusi mpaka wanapobalehe na uhakikishe baada ya hapo wanaanza maisha yao
Kazi hii hupaswi kutegemea malipo unatakiwa kufanya kama kutoa sadaka sasa ni wewe utaamua
Hao watu ambao unasema ni watoto wako wao wataamua wakulipe fadhila ama waache
Ndiyo maana wapo watu wanaosaidiwa na watoto wao na wengine wakiwa wamegeuziwa mgongo ilihali waliwaleta wao
Mtoto akishazaliwa sio wako bali ni wa muumba na Serikali ndiyo maana mtoto uliyemzaa ana uwezo wa kukupeleka gerezani na ukafungwa kama wafungwa wengine na wapo wazazi wengi sana ambao wameshalala gerezani
Unapoingia katika familia kama wewe ni mwanaume usimnyanyase mke wako na wala mke asikunyanyase kwasababu wote mmeungana pasipo kulipwa na mtu yeyote ili mtoe sadaka ya kuwaleta watu wengine duniani pasipo kutegemea malipo kwahiyo hampaswi kunyanyasana bali unganeni ili mgawane hasara au faida mtakayopata
Kama watoto watawasaidia baadaye basi mtagawana faida na kama watawatelekeza au kushindwa basi mtagawana hasara vivyo hivyo
Kwahiyo ndoa ni kazi ya kujitoa sadaka na wala sio kufanikiwa maisha
Huu ni mdahalo wa ndoa hoja zangu ndizo hizo ukiwa na zako weka hapa watu wachangie