OC-CID
JF-Expert Member
- Jul 13, 2023
- 200
- 463
Kutakuwa na mdahalo wa wagombea uenyekiti wa Chadema leo kuanzia saa 3:30 usiku pale Star Tv.
wagombea wanaotarajia kuwepo kwenye mdahalo huo ni pamoja na jabali wa siasa, Tundu Lissu pamoja na Odero Odero.
Freeman Mbowe hatahudhuria mdahalo huo kwasababu ambazo zipo nje ya uwezo wake.
Msimamizi wa mdahalo huo atakuwa Chief Odemba mtaalam wa mahojiano.
Soma Pia: Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025
Live updates zitakujia hapa
Lissu Amesema yeye akipata madaraka, atachunguza kiini cha rushwa ndani ya chama.
Aidha ameongeza kuwa akiwa Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kwa sababu rushwa ni tatizo wataunda \tume ya chama kuchunguza kiini cha rushwa pia atataka chama kiazimie kufuta rushwa, hatolipa visasi
Lissu amesema kuwa tuhuma za kwamba yeye ni mropokaji zilianza mara tu baada ya kuanza kupinga maridhiano kati ya CHADEMA na Rais Samia na kwamba inashangaza sana kuwa ameshika nafasi nyingi ndani ya CHADEMA lakini hoja za kuwa mropokaji zimeanza miezi 2 iliyopita
Tundu Lissu: Askofu Gwajima ndiye alikua mshenga wa Lowassa kuja CHADEMA
"Dkt. Slaa ndiye aliyemleta Edward Lowassa CHADEMA, ndiye aliyeanzisha hilo wazo, ndiye aliyeongoza timu zote majadiliano za CHADEMA kujadiliana na timu ya Lowassa na ndiye aliyeitisha kikao cha Kamati Kuu cha kumkaribisha Lowassa na ndiye aliyenipigia mimi simu nikiwa jimboni kwangu Singida, Mashariki tarehe 26, 27 kama sikosei ya Julai 2015 na kuniambia njoo tuna Kamati Kuu ya dharula kesho"
"Na usiku wakati nasafiri kuja Dar es Salaam akanipigia simu kunambia kwamba Chama kimeuzwa alafu nilipokutana nae kesho yake na Mwenyekiti na Askofu Gwajima…mshenga alikuwa Gwajima wa Edward Lowassa…."
Kuhusu kuitwa mropokaji Lissu amesema;
"Chama chetu kinamjadala mkubwa sana kwasababu ya kusema hayo na nje ya huo mjadala tutapata suluhu ya matatizo hayo kwasababu rushwa sasa inazungumzika, tunaweza tukaikabili."
"Kwasababu Samia amekataa mabadiliko ya Katiba na tume expose huu uongo wa maridhiano ndio maana tunazungumza habari ya 'No reform, no election', tusingefanya hivyo tungeambiwa kwamba mambo yanaenda vizuri, msijali watu wanaendesha maisha yao. Kwahiyo maneno yangu, ukweli niliousema…nasisitiza ni ukweli."
"Mimi sio mropokaji kama ambavyo nimesema wasingenipa dhamana yote hii ambayo waminipa miaka yote…nimesahau nilikuwa…waliniteua kuwa mgombea wa Urais wa nchi hii mwaka 2020 kwa uropokaji wangu na kwa haya yote wanayo yasema haya, ni maneno ya watu ambao hawana hoja yoyote ya maana kuhusiana na Uchafu ambao nimeuweka wazi."
"Niongeze kingine, kuna mambo ambayo kama ningeyasema hadharani….kuna mambo ambayo kama nikiyasema hadharani watu watakimbia sana."