Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Status
Not open for further replies.
Itakuwa vyema kama huo mdahalo utafanyika ili sera ziwekwe wazi lakini hizo ni ndoto
 
Baada ya mgombea urais kupitia Chadema Dr. Wilbroad Slaa kutoa mwito kwa Rais Kikwete kusimama nae katika mdahala kujadili mustakabala wa Taifa hili, Rais Kikwete ameingia mitini kwa kuhofia kuumbuliwa hadharani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tambwe Hiza Kwa Vyombo vya Habari jana, amesema rais hatafanya hivyo kwa kuwa saa 1 haitoshi kuelezea sera za CCM na wanaotaka kujua nini CCM inataka kufanya miaka mitano ijayo yote yameainishwa katika 'election maifesto' yao na rais atapita nchi nzima kuelezea wananchi

Hii inadhihirisha tunaongozwa na viongozi wa aina gani. Iwapo bwana kikwete angethubutu kusimama na Dr Slaa katika mdahalo wanatambua wazi kuwa angeumbuka kwa kuwa hata katika hotuba zake anaandaliwa data muhimu na wakati mwingine sio sahihi.

Hivyo kama ataulizwa maswali ya papo kwa papo wakati mwingine anaweza kukosa majibu. Vile vile wanatambua asingeweza kukabiliana na challenge za Dr Slaa kuhusu madudu aliyoyafanya miaka mitano iliyopita hasa kushindwa kuwashughulikia mafisadi pamoja na uchumi ambao unaanguka licha ya kuwadanganya wananchi kuwa pato la mtanzania limeongezeka wakati wa utawala wake. (They did not tell the people about inflation rate and how the purchasing power of the common citizen has been affected)

Je wanajamii mna maoni gani kuhusu msimamao wa rais wetu?
 

Mwaka 2005 alipopewa changamoto ya kushiriki mdahalo na wagombea wengine wa urais, mgombea wa CCM, JK alikacha bila ya kutoa maelezo ya kuridhisha. Wapambe wake walijua fika kwamba pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kuongea majukwaani, hakuwa na uwezo wa kujenga hoja na kuzieleza kwa makini na ufasaha, ukilinganisha na akina Lipumba na Mbowe.

Aliogopa kuulizwa maswali magumu hasa ya uchumi ambayo Profesa wa uchumi, Lipumba angeweza kumbana nayo.

Safari hii JK amekacha tena na bila shaka anamuogopa Dr Slaa, mgombea wa Chadema kuulizwa maswali kuhusu wizi wa EPA, wizi ambao ambao inaaminika ulikuwa ni brainchild ya CCM ili kujipatia hela za kampeni za kumuingiza JK madarakani na hivyo kuwapiku wagombea wengine wasiokuwa na njia za kujipatia fedha kwa wizi wa namna hiyo.

Leo gazeti laTanzania Daima, limemnukuu Mabere Marando wa Chadema akisema kwamba JK aliingizwa madarakani kwa msaada wa hela za EPA na ametishia kutoa siri hiyo. Marando anajua anochokisema kwani anawatetea baadhi ya watuhumiwa wa EPA katika kesi zao na hivyo bila shaka sasa anajua siri zote.

Kwa hali ya namna hii ni lazima JK amuogope Dr Slaa kwani katika mdahalo, Dr Slaa, katika maelezo yake anaweza pia kuuliza swali kama hili:

"Kwa nini ushahidi kuhusu wizi wa EPA wa bilioni 40 za EPA uliofanywa na kampuni ya Kagoda haujapatikana iwapo CRDB -- zilikopitia hizo pesa na kulipwa cash kwa wezi hao -- wangeweza kiurahisi tu kubanwa kwa lengo la kuwataja hao waliolipwa? Jee ufuatiliaji wa mlolongo wa fedha hizo hadi mwisho si ungeweza kugundua hizo pesa ziliishia katika mikono ya akina nani?

Ni dhahiri JK anaogopa swali kama hili kwani hata ule usanii wake wa kimahiri ungeshindikana! Naamini hilo ndilo linalomkimbiza kwenye mdahalo!
 
mmh bora amekataa mwaya manake aibu ingewajaa wana ccm
mdahalo ni kitu chema sana yani tungejua nani akili zake za kimbayu wayu asiyezchanganya na za jirani b4 ajasmama kwenye kutoa hotuba!!!!
 
JK hana ubavu wa kusimama kwenye mdahalo kwa sasa maana alivyofunika miaka hii 5 >>>>>haifai kabisa kusimama kujibu maswali.....aibuuu kama anabisha akubali aone moto wake
 
okl lkn pia dk slaa ataulizwa simple question
nini uhusiano wake na kanisa katoliki?

Ni muumini wa Kanisa Katoliki kama ilivyo kwa Jakaya Khalifan Mrisho Kikwete na Ibrahimu Lipumba kwa Islaam.
 
Jamani mbona mnataka kumwonea JK. Hivi nyie mnaona kweli Dr JK anaweza kukabiliana na Dr Slaa kwa hoja!!!!!! Ni sawa na kuwa na debate kati ya mwanafunzi wa form 2 wa shule za kata zenye walimu wa vodafasta na graduate wa Phd wa Havard university
 
lakini JK anayodini yake mbona aliweza kuingiza moja ya ilanii ya uchaguzi katika ccm yaani maakama ya kazi ili wajipatie wafuasi .

Vipi hapo unasemaje.
Je kuna mgombea asiye na dini ?.
Na kama yupo ni nani?
 
Nafikir ipo haja mdahalo uwekwe kwenye sheria za nchi.
 
Ndio tabu ya viongozi wetu kuogopa challenge mbali mbali,kuna kitu nimekumbuka JK aliwahi kwenda kwa Obama na lundo la makaratasi kuongea nae,hii inaonesha alikuwa hana data kichwani na hajui cha kuongea mpaka aandaliwe,hivyo Tambe Hiza kusema watu wakasome makaratasi yao ni sawa maana hata JK mwenyewe anajua matatizo ya watanzania kwenye makaratasi.
Natoa hoja.
 
Wangepanga masaa matano au wanayoona yanatosha...mbio za nini.?
 
okl lkn pia dk slaa ataulizwa simple question
nini uhusiano wake na kanisa katoliki?

Simple yeye ni muumin kanisa hilo kama wewe ulivyo muislam, tatizo lako ni chukikwa ukristo,bora uhame nchi hii uende Iran nyumbani kwa bosi wako RA
 
Nafikir ipo haja mdahalo uwekwe kwenye sheria za nchi.
Kipindi hiki cha kampeni Mdahalo nchini Australia umekuwa sawa na kichekesho kwa waziri mkuu kajikoroga. Imegeuka kwa waziri mkuu anataka mdahalo urudiwe upinzani wamechomoa. Sasa kama JK anaukimbia mdahalo babake basi hiyo nchi kashamba ka bibi kila mtu anafanya atakalo.
 
Jamani msilazimishe kikwete aende kwenye mdahalo aibu haitakua kwake na ccm tu bali kwa watanzania wote kwa kuwa na rais kama yeye for the past 5 years
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom