Mwaka 2005 alipopewa changamoto ya kushiriki mdahalo na wagombea wengine wa urais, mgombea wa CCM, JK alikacha bila ya kutoa maelezo ya kuridhisha. Wapambe wake walijua fika kwamba pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kuongea majukwaani, hakuwa na uwezo wa kujenga hoja na kuzieleza kwa makini na ufasaha, ukilinganisha na akina Lipumba na Mbowe.
Aliogopa kuulizwa maswali magumu hasa ya uchumi ambayo Profesa wa uchumi, Lipumba angeweza kumbana nayo.
Safari hii JK amekacha tena na bila shaka anamuogopa Dr Slaa, mgombea wa Chadema kuulizwa maswali kuhusu wizi wa EPA, wizi ambao ambao inaaminika ulikuwa ni brainchild ya CCM ili kujipatia hela za kampeni za kumuingiza JK madarakani na hivyo kuwapiku wagombea wengine wasiokuwa na njia za kujipatia fedha kwa wizi wa namna hiyo.
Leo gazeti laTanzania Daima, limemnukuu Mabere Marando wa Chadema akisema kwamba JK aliingizwa madarakani kwa msaada wa hela za EPA na ametishia kutoa siri hiyo. Marando anajua anochokisema kwani anawatetea baadhi ya watuhumiwa wa EPA katika kesi zao na hivyo bila shaka sasa anajua siri zote.
Kwa hali ya namna hii ni lazima JK amuogope Dr Slaa kwani katika mdahalo, Dr Slaa, katika maelezo yake anaweza pia kuuliza swali kama hili:
"Kwa nini ushahidi kuhusu wizi wa EPA wa bilioni 40 za EPA uliofanywa na kampuni ya Kagoda haujapatikana iwapo CRDB -- zilikopitia hizo pesa na kulipwa cash kwa wezi hao -- wangeweza kiurahisi tu kubanwa kwa lengo la kuwataja hao waliolipwa? Jee ufuatiliaji wa mlolongo wa fedha hizo hadi mwisho si ungeweza kugundua hizo pesa ziliishia katika mikono ya akina nani?
Ni dhahiri JK anaogopa swali kama hili kwani hata ule usanii wake wa kimahiri ungeshindikana! Naamini hilo ndilo linalomkimbiza kwenye mdahalo!