Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Elections 2010 Mdahalo wa wagombea urais 2010

Status
Not open for further replies.
Kama ccm wamekataa mdahalo kuna haja CHADEMA ya kuandaa mdahalo na vyama vingine ambavyo vimesimamisha mgombea uraiskama TLP,CUF,DP,NCCR ili kwamba tuweze kutangaza sera zetu VYEMA DHIDI YA WAPINZANI WENGINE kwani hata wao wanatupinga ndio maana wanasimamisha wogombea.
 
Kama ccm wamekataa mdahalo kuna haja CHADEMA ya kuandaa mdahalo na vyama vingine ambavyo vimesimamisha mgombea uraiskama TLP,CUF,DP,NCCR ili kwamba tuweze kutangaza sera zetu VYEMA DHIDI YA WAPINZANI WENGINE kwani hata wao wanatupinga ndio maana wanasimamisha wogombea.

Safi kabisa, JK atauona kwenye vyombo vya habari tu! Kwani lazima JK awepo kwenye mdahalo jamani? Aendelee kukusanya shilingi bilioni 50 za kununulia khanga, chumvi, sukari, nk ili "kuwaneemesha" walalahoi wakati wa uchaguzi kwa "kuwakirimu" maana mambo magumu sana kwake mwaka huu! Ameanza kudai kuwa "usimdharau adui!" Tunamshukuru angalau amekuwa 'honest!'
 
Maswali kwa JK
1. EPA, hatima yake ni nini?
2. KAGODA, RICHMOND, KIWIRA, DOHANS mbona kimya?
3: LOLIONDO, mkataba wao ni kwakuchukua wanyama, kuingia nchi bila visa, kuwa na jeshi, kuwa na masiliano yao ndani ya nchi yetu?
4. FEDHA ZA BOT, nini kinachoendelea
5. ATC, shirika la ndege kwanini limekufa? na mbia mbona hajaanza nini kikwazo????<<< 10% au???>>>>
6. TRC, udhaifu wa mikataba kwa umakini wa viongozi wake, je walioandaa hiyo mikataba mibovu wamechukuliwa hatua????
7. TTCL, kubinafishwa majengo kuuuzwa kwa bei ya chee, mtaji wa iliyokuwa Celtel ulitoka wapi?? je ilivyouzwa tulipata nini???
8. MATUMIBI MABOVU FEDHA ZA SERIKALI<< TRILION 1.7>>> je ameshalifanyika kazi???

Ongezeni Maswali Plz
 
KIKUBWA KINGINE NI JINSI ALIVYOSHUGHULIKIA SUALA LENYEWE LA EPA KIUSANII....ALIWAAMBIA WEZI WALE WARUDISHE PESA ANAWASAMEHE WAKATI HATA YEYE HAYUPO JUU YA SHERIA ...ALITUAMBIA WAMERUDISHA WAKATI HATUKUJUA NI PESA KIASI GANI NA ZIMEENDA WAPI ..MI NILIJUA KAMA KWELI KUNA PESA ZILIZORUDI BASI LAZIMA BUNGE LINGETAARIFIWA ILI LIPANGE BUDGET KWAYO.......aliwadanaganya watrz kuwa anawajua wala rushwa kwa majina wa tra lakini akanyamaza....akawadanganya watz kuwa anayo majina ya wala rushwa hapo siku za karibuni lakinio katudanganya pia.....
kiongozi muongio namna hiyo atakubali kushiriki mdahalo na watu wasomi na waelewa kama dr slaaaaaaa?????????????????
 
Kama ameweza kumuachia aendeshe chama kwanini ashindwe kumpeleka akamukilishe kwenya mdahalo? Ndege wa aina moja huruka pamoja!!
 
huu ni wakati wake kuwaambia watanzania nini amewafanyia na nini atafanya, ktk karne hii tunayoishi kiongozi kuogopa mdahalo
ni sababu tosha ya kumnyima kura kwa maana kama anakuwa mwoga kuwaeleza watanzania wenzake sababu za kumchagua tena.
hii pia kinamna ni kama dharau fulani kwa sababu kama mtu kila siku kusafiri ulaya na marekani kukutana na wazungu kwa kutumia
mabilioni ya walipa kodi, Leo hii tunataka atueleze hayo mabilioni aliyotumia kusafiri mara kwa mara yametusaidia nini hataki hii ni
dharau kubwa kubwa kwa Watzan. kwa kutumia jasho la kukataa kueleza matunda ya safari zako.
 
Sipendi kuamini kwamba Rais Kikwete ataingia mitini pindi atakapohitajika Kufanya mdahalo na Wagombea wengine, kama Kikwete ni muoga hivi anaweza kweli kukaa na the like of Vladmir Putin, Ahmedejad kweli
 
Kama ccm wamekataa mdahalo kuna haja CHADEMA ya kuandaa mdahalo na vyama vingine ambavyo vimesimamisha mgombea uraiskama TLP,CUF,DP,NCCR ili kwamba tuweze kutangaza sera zetu VYEMA DHIDI YA WAPINZANI WENGINE kwani hata wao wanatupinga ndio maana wanasimamisha wogombea.

Hili nafikiri ni wazo zuri sana, CCM iachwe nje, wagombea wengine wapambanishwe, halafu watanzania waambiwe wazi kuwa mgombea wa CCM amekimbia. Mimi natamani hasa Slaa na LIpumba ndio wapambanishwe halafu waulizwe kwa nini wasiunganishe nguvu kuibwaga CCM tusikie majibu ya kila mmoja, kwani sisi tumechoshwa kuona wanamageuzi wanapingana, inatukera sana sana. Lazima muwaambie watanzania kwa nini mmeshindwa kukaa pamoja na kama mko hivyo ikulu mtaiweza?
 
Mchungaji Slaa kwanini asifanye mdahalo na mkewe atoke CCM na kuamia Chadema? kama kashindwa kum-convince mkewe atamuweza nani?

Huyu mchungaji yuko weak iweje mkewe mpaka leo kabaki CCM? inamaana hamuamini mumewe? Afanye mdahalo chumbani na mkewe kabla hajafanya na wananchi

You are not well informed ,not anymore. Get the updates lazy!!!
 
SERA YA CHADEMA NI ILEILE YA MPENDAZOE(UFISADI) HAWANA SERA MBADALA....NDO MAANA HATA MPENDAZOE ALIPOENDA HUKO HAWAKUONA JIPYA WAKAMWAGA......! maendeleo ya michezo, uchumi, miundombinu,elimu SI AJENDA ZA CHAMA HIKI......WANA AJENDA MOJA KUU KWA MIAKA MITANO......LABDA CHAMA KINGINE....NEEEEEEXT....!
Sasa hii ina uhusiano gani na mdahalo... haya ni mawazo yako kuhusu chama sisi tunajadili JK kukwepa mdahalo... get real!
 
CCM says JK won't participate in debate Saturday, 07 August 2010 10:16
By Hellen Nachilongo and Subira Kaswaga

The ruling party, CCM, yesterday ruled out any possibility for President Jakaya Kikwete will participate in a live debate with other presidential candidates in this year's General Election.

The party's deputy secretary for propaganda and publicity, Mr Richard Tambwe Hizza, said at a press briefing that President Kikwete do not need such a debate to reach out for voters.

"Our party chairman and presidential candidate is qualified and has a track record that does not require him to participate in any debate. We advise the opposition to run own shows as they are the ones who lack knowledge on running public affairs," said Mr Tambwe.

He was responding to a challenge thrown by Chadema's presidential aspirant, Dr Willibrod Slaa, on Tuesday suggesting that President Kikwete should face him in an open public debate to defend their parties' policies.

Yesterday, the Chadema director for international relations and foreign Affairs, Mr John Mnyika, described the CCM move as "cowardly" and said the party would never face anyone in public due to alleged ills it has committed.

"The rejection shows how CCM likes to conduct its politics in secrecy and away from the public. President Kikwete cannot respond to critical national issues in the open because he will be exposed," said Mr Mnyika.

In defending President Kikwete, Mr Tambwe Hiza said the CCM candidate had already given his nomination acceptance speech in public and would soon embark on a campaign trail to sell his policies to the people and not in a forum organised by the opposition.

"Dr Slaa and his group are only interested in using the President's name to sell their ideas in the pretext of a debate. They do not have a selling point and have lurched to the idea of a debate as bait," said Mr Tambwe who defected from the opposition.

According to Mr Tambwe, CCM policies were known to the majority of its members and supporters.

But Mr Mnyika dismissed Mr Hiza, saying he was not informed of the global trend on open policy debates by candidates in leadership race, including for the presidency.

"Debates are a global phenomenon today and progressive leaders anywhere have never shied such events. Those opposed could only be said to lack the confidence of their own records," the Chadema official told The Citizen, adding that during such events, the public is given time to interrogate the candidates.

"The debate between presidential aspirants is done in different countries in the world and is a sign of maturity in democracy. It is surprising that CCM fears such debates if the party is clean, serious, and confident about its policies."

Meanwhile Mr Mnyika said Dr Slaa's running mate will be known on October 12 after the party's NEC meeting which will decide on a suitable candidate. Dr Slaa is today expected to hold his first public rally at Jangwani grounds in Dar es Salaam since his nomination to run for the country's top post.
Source:Mwananchi Newspaper.
 
Ninachojua mimi ni kwamba kwa trend ya siasa za sasa za uwazi na ushindani, open debate kwa wagombea ni muhimu sana ambapo wagombea wananadi na kutetea sera zao na kuonyesha/ku-prove uelewa wao wa kile wanachokiamini na kukijua kuhusu mambo kadha wa kadha.

Ni sehemu tofauti na majukwaani ambapo wafuasi wa mgombea wanashangilia kila kitu hata kama ni pumba na hakuna fursa ya maswali challenging.

Hivi karibuni CCM kupitia viongozi wake watendaji tofauti tofauti wamepinga idea ya mgombea wao kushiriki mdahalo. Sababu wanazotoa hazijaniingia akilini bali naona ni uoga na kumsitiri mgombea wao na udhaifu wake wa kujenga hoja mbele ya watu wenye mawazo tofauti na yake kama ambavyo anapenda kuongea na watu wanaomshabikia (wana-CCM ambao huwa anawaita 'wazee wa mkoa wa Dodoma au Dar-es-salaam).

Mfano mkuu wa kitengo cha Propaganda (Propaganda simply means uongo geuza ukweli) nimemnukuu kwenye Gazeti la Citizen la majuzi akisema "Our Party Chairman and presidentialcandidate is qualified and has a track record that does not require him to participate in any debate. We advise the opposition to run their own shows as they are the one who lack knowledge of running public affairs".

Kama huo ndio uelewa wa CCM juu ya essence ya public debate ya candidate, basi hapo hatuna chama makini. Nashauri, taasisi itakayotaka kuandaa huo mdahalo, iandae na kualika wagombea wote na viti vyao viwepo tena viwe labelled na atakayekosa kuja-aibi kwake!!! I believe, kina Tambwe hawana lolote zaidi ya kumuogopa Dr. Slaa. Laiti wangekuwepo wasindikizaji wao, kina Lipumba, wangeukimbilia mbiombio.
Naomba uwepo wa huo mdahalo ili wapambanishwe na washindanishe sera na hoja zao LIVE!

Nawasilisha!!!!
 
Imefika wakati Watanzania tuamke, tujue kusema ukweli na hiyo kweli iwe amali katika tamaduni za jamii zetu. Tuache kufuata mkumbo wa watu wachache ambao ama kwa makusudi au kwa kutokujua wamekuwa wakipotosha ukweli kwa manufaa yao na kutupilia mbali maslahi ya Taifa.

Hivi kwa mtu mwenye akili timamu tu, achilia mbali msomi, kwa kuwa wasomi nchi hii ni wachache sana, kuna ulazima gani wa kutumia nguvu na muda mwingi kushinikiza mdahalo kwa nchi kama hii yetu ambayo uhuru wa kuzungumza umeachiliwa kwa kila raia, awe mpiga kura ama awe mgombea. Rais alishatoa nafasi ya kumuuliza maswali kupitia luninga, akaeleza na kujibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wapiga kura wake, ya nini basi kuacha kuyafanyia kazi aliyowaahidi na kuzama kwenye kuwaza mdahalo ambao hauna manufaa kwa Taifa.

Wanaolazimisha mdahalo, je, walitumia fursa ya kuwasiliana na Rais kwa kiasi gani? Hebu basi tujidahalo wenyewe kwanza, tumefanya nini ambacho tulikwenda Serikalini tukanyimwa msaada wa kupiga hatua moja mbele? Kwa vipi basi twaweza kupaza sauti kama mazuzu kwa mambo ambayo hata wewe mwenyewe huwezi kueleza hata mantiki yake? Kwani Watanzania ni bendera fuata upepo hadi wakubaliane na kila kitu bila kutafakari? Na je mnataka kutuambia kuwa Rais wetu ni wa kupelekwa kama jahazi baharini?

Hebu tujidahalo, kuna mambo mengi sana mazuri mno ambayo Rais ameyafanya, na mengine hadi sasa yapo kwenye kiwango kizuri cha kutekelezwa, mbona hamuyasemi?

Tuwe wakweli na tuache uzabi-zabina.
 
Hakuna mpambe wala pamba bali mapambano ya hoja na sera badala ya sura Vijana Bwana. Sijui wakoje siku hizi. Wakati sisi tulikuwa tayari kukubali tunayoambiwa, tuliwaamini watu, vijana wa siku hizi wanataka kuhoji kila kitu. Wanataka kupima na kujiamulia wenyewe. Hebu angalia pepe hili hapo chini. Mwishiwa Makengeza, Shikamoo! Na baada ya kushika miguu yako bila sababu (hivi kweli hatuwezi kupata salaam nyingine ya heshima?) naomba nitoe dukuduku zangu kwako kama kijana wa nchi yetu. Sisi vijana ndio walio wengi katika nchi hii, tena walio wengi sana, lakini inavyoonekana, watu wanataka tushike miguu yao tu, badala ya kuelewa na kutenda kwa faida ya nchi. Kwa kuwa wametuona tumeinama tu wanatudharau, na tukiasi kuinama wanatuita wahuni wasio na heshima blaa blaa blaa hadi balaa.

Ngoja nijieleze kidogo. Kwanza nakuandikia wewe kwa sababu naamini unataka mabadiliko chanya kwa ajili ya taifa letu. Si kwa sababu ya chama hiki au kile, bali uchaguzi huu unatoa fursa nzuri kuachana na miaka hii mitano ya kashfa baada ya kashfa. Unatoa fursa kwa ajili ya kupeleka kizazi kipya (si kiumri, kimtazamo) bungeni ili, wawe wa chama hiki au kile, waweze kuweka misimamo na sera bora zaidi. Lakini ili kufanya hivyo, tunahitaji kuwasikia wagombea mbalimbali wakibadilishana mawazo, wakipeana changamoto, kukosoana na kurekebishana, siyo tu kutamba jukwaani, bali kukutana pamoja ili tuweze kupima nani anasema ukweli zaidi, nani ana sera zaidi, nani amefikiria kwa kina zaidi kwa ajili kututoa katika lindi la kukata tamaa linalowameza vijana wengi. Ndiyo. Huwezi kumpima mtu jukwaani maana anatamba peke yake na wapambe wanampamba akitamba (na kumjaza pamba masikioni).


Tunataka kumsikia akikabiliwa na changamoto kutoka kwa mwingine, asiyekubaliana na mtazamo wake, au sera zake, au takwimu zake. Kwa kiasi fulani kazi hii inaweza kufanywa na vyombo vya habari lakini mpaka sasa sijaona uchambuzi wowote wa sera za vyama mbalimbali, tofauti zao, na kadhalika. Sijawaona wakihoji au kuchambua takwimu zinazotolewa na upande wowote. Lakini zaidi ya yote tunataka kupima na kuamua mwenyewe kwa kuwasikiliza laivu. Hapa hakuna mpambe wala pamba bali mapambano ya hoja na sera badala ya sura. Ndiyo maana vijana tunasema



NO MDAHALO NO VOTE



Kwa maana kwamba asiyekubali kushiriki mdahalo ili kutuwezesha kupima na kuamua tumchague nani kwa faida ya taifa hawezi kupata kura yetu. Na tunasisitiza mdahalo utangazwe na wagombea wote wakaribishwe kushiriki. Asiyekubali atawakilishwa na kiti kitupu na wengine watapewa nafasi ya kujieleza bila upinzani kutoka kwa yule au wale waliokataa kushiriki. Kwa njia hii, tunaamini kwamba wote watakubali kushiriki kwa faida yetu. Maana tunaamini kabisa kwamba asiyekubali kushiriki ni mwoga, hajiamini.
Tuliona hata mfano wa Uingereza juzi. Waziri Mkuu alidengua, alidengua, lakini mwisho ilibidi akubali na Waingereza walifaidi sana. Karibu nchi nzima waliangalia na kuweza kupima na kuamua. Kama hawa wakoloni waliotutesa waliweza kufanya hivyo, kwa nini sisi tuliomtoa mkoloni yuleyule hatuwezi kufanya vile? Nilisoma katika facebook (njia yetu sisi vijana kuwasiliana ndiyo maana tunawashukuru wagombea wenye kurasa zao humu … ingawa wanatakiwa kujibu maswali yetu pia!) jamaa mmoja akapinga kuwepo kwa mdahalo eti rais ni mtawala wetu hivyo hawezi kuongea na sisi watawaliwa, ni kinyume cha itifaki. Ha ha ha ha ha! Sasa kama mtawala haongei na sisi watawaliwa ataongea na nani? Wafadhili na mafedhuli? Ama kweli watu wengine wanachekesha.
Na hatuongelei upande wa urais tu. Siku hizi maredio ya FM yametapakaa kila mahali. Basi wagombea ubunge wa jimbo fulani na hata wagombea wa udiwani wafanye midahalo yao tuweze kupima na kuamua. Tunasema tena, mihotuba kibao, na ahadi dafrao hazitusaidii kuamua hata kidogo. Tunataka laivu, kila mmoja aonyeshe umahiri wa sera yake kwa kukabiliana na wenzake. Na mwenye sura badala ya sera, atokomee huko. Hatumtaki.



NO MDAHALO NO VOTE



Kwenye ngazi zote! Haya. Nije kwa wengine ambao pia wanataka tushike miguu ya watu (na ni wazi ukishika miguu ya mtu, lazima upige magoti mbele yake!) ni hao ambao wanadai wanataka kuendesha elimu ya uraia kwa wapiga kura. Nasikia mashirika mbalimbali, yakiwemo ya vijana wamepewa pesa kibao kujua kutuhubiria umuhimu wa kura zetu, tupige kura badala ya kuiuza, na maneno mengine yasiyo na mwisho. Kwani hatuyajui yote hayo? Ni sawa na kutuambia UKIMWI unaua na tubadili tabia. Tunajua na watu wanapewa nafasi ya kutafuna pesa kama wehu kwa kuja kututambia kwa kutuambia sifuri. Bora hata wangetuambia ufisadi unaua, mafisadi wabadili tabia, na kutupa nafasi ya kutafakari jinsi ya kuwakomesha mafisi wa ufisadi kabla hawajatutafuna wazimawazimu. Ndiyo, Makengeza. Sisi vijana tulifikiri elimu ya wapiga kura maana yake ni kutuwezesha sisi wapiga kura kukutana na kutoa mawazo yetu na kuandaa hoja za kumkabili kila mgombea si kukaa na kusikiliza hubiri zilezile kutokana na mamluki waliopewa pesa kwa ajili ya hubiri hizo.


Bora wangekuja kutuhubiri kwa kujitolea ha ha lakini lini hayo yatatokea? Hivi lini watu, wakiwemo wafadhili na mafedhuli, watajifunza kwamba hatusikilizi mihotuba ya walio nacho. Sisi tunatenda kutokana na kupewa nafasi ya kushiriki kikamilifu sisi wenyewe. Kwa hiyo sisi vijana tunasema tunataka kushiriki kwa vitendo si masikio tu. Tunasema watu wasipoteze muda kutuhonga. Tumedhamiria na tutahongwa na mipango mizuri kwa vijana inayotekelezeka, si fedha, si ahadi ya fedha kama mabilioni ya huyu au yule.



Tutahongwa na sera si sura. Na kama vijana tutasimama imara kuhakikisha kwamba katika kila kituo cha kupiga kura, kila kata, na kila jimbo mafisadi hawatapewa nafasi ya kuharibu uchaguzi kwa kujaza kura feki, au kununua kura au mbinu zozote chafu. Na kama sote tumedhamiria hivyo, na tunatekeleza, tunao uhakika kwamba wenye nia mbaya ya uchaguzi, wanaoamini kwamba sisi tutakumbatia magoti ya watu ili mradi pesa tu, watakuja kujuta kwa nini walimwaga pesa zao zote bila mafanikio.

Ufisadi na wizi unawezekana kama tunauruhusu kwa kutofanya lolote. Narudia kusema Makengeza. Laiti vijana tungekuwa na chama chetu … lakini kwa kuwa hatuna, tutakuwa makini kusikiliza sera za kila chama, kila mgombea ili tuweze kumchagua yule ambaye kweli ataleta mabadiliko mazuri katika maisha yetu. Au vipi? Kijana asiyeinama bali anasimama imara. Jamani wasikia hayo. Vijana hawana utani mwaka huu. Asiyesikiliza asije akajuta baadaye.


Source:Mwananchi Jumapili
 
Siku moja Nchi itakuwa inaibiwa pamoja na kuwa inaibiwa mpka sasa kwa sababu
viongozi wetu ndo walewale zero brain
 
Wadau,

Magazeti ya leo yamemnukuu mwenyekiti wa kamati ya kampeni ya CCM (A Kinana) akisisitiza msimamo wa chama chao kuwa mgombea wao hatashiriki mdaharo kwa kisingizio kuwa mda hautoshi.
Mimi ndahani mzee IQ yake ni ndogo, wasaidizi wake wanalijua hilo na wanaogopa wakimruhusu kushiriki udhaifu wake katika kutafakari mambo utakuwa wazi zaidi na hivyo kukosa nafasi ya kuwadanganya WADANGANYIKA, au kuna sababu nyingine ya msingi?????
 
kAMA anashindwa kuhudhuria mdahalo, anayo agenda ya siri, lengo sikutaka wana wa cnhi wa msikie...nadhani ana mapungufu fulani anayaficha na kama ni hivyo, HATUTAKI HATA SPEECH zake za kila mwisho wa mwezi au matukio maalumu ( mgomo wa TUCTA)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom