Mwanamosi
Member
- Aug 9, 2010
- 73
- 0
Kwakweli sual la mdahalo ni jambo zuri lakini nadhani kila chama kina mbinu zake katika kusaka ushindi...navyojua mimi midahalo mara nyingi hutumika kuonesha udhaifu wa mtu (hasa kiafrika zaidi.). nasema hivyo kwa kutazama midahalo kadhaa niliyojaribu kufatilia ya kusaka uongozi toka nilipokuwa sekondari hadi chuo na baadhi ya uongozi wa nchi ktk afrika na huko majuu. tofauti niliyoona ni kuwa majuu humchallenge alie madarakani au chama chake kuhusu sera flani ambazo majibu yake yapo kutokana na maandalizi ya mdahalo kwa wahusika kujiandaa na topic husika ila kwa Afrika nilichoona ni siasa za kuchafuana na kuexpose udhaifu wa mtu husika nahic hii ndio sababu CCM wamekwepa mdahalo huu kwani hofu ya kuchafuliwa ni kubwa kutokana na mwenendo wa nchi ulivyo na jinsi chama kilivyobehave ktk 5 years zilizopita. yawezekana pia ni kuwanyima nafasi upinzani kuwaua kwa mabomu yatayobadili uelekeo wa kampeni...so nachoona mimi ni kuwa hiyo ni Political move ya kuendelea na kampeni bila hofu ya kuchafuana kupitia mdahalo ambao unaweza kuamua nani awe rais...huu ni mtazamo tu wa kwnini wamekwepa ila sababu wanazo wenyewe nisingependa kuwajibia. ila nadhani hata bila ya mdahalo bado waTZ wana nafasi ya kujua sera za wagombea na kufanya chaguo sahihi oktoba.