Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 673
- 1,318
Recorded video🎥👇🏼
MASUALA MUHIMU YALIYO ZUNGUMZWA
Jambo kubwa zaidi lililozungumzwa na wagombea wote ni suala la mamlaka na wajibu wa TLS kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha 4 cha Sheria ya TLS. Hata hivyo, mbali na hilo, kuna mambo kadhaa yaliyojitokeza katika mdahalo huu, ikiwemo suala la Katiba Mpya, matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa, utekaji, rushwa, pamoja na kama wagombea hao watakubaliana na matokeo iwapo watashindwa katika uchaguzi huo.
Suala la Katiba Mpya
Mwabukusi anasema ataishinikiza serikali kuhusu suala hili kwani ni moja ya majukumu ya TLS.
Muga, kwa upande wake, anasema akiwa Rais wa TLS hatoweza kujihusisha na suala la Katiba kwa sababu sio jukumu la TLS wala la Wakili.
Mkuba anasema mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya unacheleweshwa na siasa za nchi, na anakiri kuwa yeye ni mwanachama wa CCM.
Kaunda anasema akiwa Rais wa TLS, atahakikisha anaikumbusha na kuishawishi serikali kuhusu suala la Katiba Mpya.
Pia soma: Boniface Mwabukusi ashinda kesi dhidi ya Tanganyika Law Society. Ruksa kugombea Urais wa Chama hicho
Bendera anasisitiza kuwa Katiba Mpya inapaswa kuboreshwa katika ibara zinazohusiana na haki za binadamu, akieleza kuwa polisi wamekuwa wakivunja haki za binadamu mara kwa mara.

Matumizi Mabaya ya Rasilimali za Taifa
Mwabukusi anasema kuwa Rais Magufuli alituachia zawadi ya sheria za ulinzi wa rasilimali za nchi.
Kauli, kwa upande wake, anasisitiza umuhimu wa kutekeleza sheria.
Muga anaamini kuwa wananchi ndio wenye jukumu la kuzilinda rasilimali hizo, wakati Mkuba anasema tatizo ni kubwa na mikataba yote inasainiwa kibiashara, hali inayowanufaisha zaidi wageni kuliko Watanzania.
Kaunda anasema tatizo kubwa ni kuwa TLS haikutimiza majukumu yake ya kuishauri na kuishinikiza serikali kwamba rasilimali ni za wananchi wote, huku Bendera akisema siasa zetu ndio zinazosababisha rasilimali kugawanywa visivyo.

Suala la Utekaji
Mwabukusi anasema akiwa Rais wa TLS atasisitiza uwajibikaji wa serikali na kuhakikisha kuwa vyombo vya polisi vinasimamiwa vizuri, ikiwa ni pamoja na IGP kuwa na chombo cha kumsimamia.
Kauli anaona tatizo liko katika vyombo vya usalama na hana uhakika kama TISS inafanya kazi yake vizuri, akisisitiza umuhimu wa polisi na TISS kufanya kazi kwa pamoja.
Muga, kwa upande wake, anasema hajui kama Rais wa TLS atafanya nini kuhusu suala la utekaji, bali atawaachia wanachama waone wanafanya nini.
Mkuba anasema akiwa Rais wa TLS, masuala yote ya uhalifu yatapigiwa kelele na kuhakikisha yanashughulikiwa na kuzuiwa.
Kaunda anasema akiwa Rais, atashauri baraza la uongozi liishauri serikali iunde tume ya kijaji kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa masuala ya uhalifu.

Suala la Rushwa
Mwabukusi anasema mtu anayetoa na anayepokea rushwa ni mpumbavu na anaamini kuwa rushwa inaweza kutumika katika uchaguzi huu wa 2024.
Muga anasema rushwa ni suala la gizani na ni lazima utumie mbinu kuvutia watu, akifafanua kuwa unatakiwa kuwa na rekodi nzuri ili kuvutia mawakili.
Mkuba anasema haamini kama mgombea wa urais wa TLS atatumia rushwa katika uchaguzi wa mwaka huu na anasema hajawahi kutumia rushwa katika uongozi wake tangu akiwa darasa la saba.
Bendera anasema rushwa ni adui wa haki na hatoi wala kuunga mkono suala la rushwa, akiwataka mawakili kutopokea rushwa.

Kukubaliana na Matokeo ya Uchaguzi
Kuhusu suala la kama wagombea hao watakubaliana na matokeo iwapo watashindwa katika uchaguzi huo, wagombea wote wameahidi kuwa watamheshimu yeyote atakayeshinda katika uchaguzi huo na kukubaliana na matokeo pamoja na kumtii mshindi.