Elections 2010 Mdahalo wa Wagombea vijana Movenpik 25/09/2010

Elections 2010 Mdahalo wa Wagombea vijana Movenpik 25/09/2010

Swali la kampeni, wafisadi kusifiwa maana yake nini, swali lachakachuliwa
 
Bonge la kichapo kwa CCM, adai inavunja ndoa za watu, nadhani watamnyanganya mic. Jamaa anambamiza Kikwete moja kwa moja, anasema imefikia sehemu inawakumbatia kina Chenge.

Kasesela anadai Elimu Bure ni gharama kubwa kibajeti, anasema CHADEMA ilani za vyama vya upinzani zote ni za gharama sana na watapata wapi hela.
 
Zitto anamjibu Kasesela kuwa amejuaje kuwa upinzani utakuwa na wabunge wachache. Maana CHADEMA imeweka wagombea 176 nchi nzima, amejuaje hawa wote hawatakuwa wabunge?

Anasema pesa zipo, anasema ndo maana wamekuwa wakitoa bajeti kivuli kila mwaka ili kuonyesha kuwa bado kuna mbadala wa mapato ikiwa ni pamoja na Tanzanite na dhahabu ambavyo vinaweza kulinufaisha taifa
 
Mwisho wa mdahalo wakuu. Jenerali anasema haitawezekana kuendelea maana inawezekana kukesha
 
Swali la tatu, ahadi ni nyingi watatekelezaje? yaani vyanzo vya mapato zi wapi?

Zitto asema vyanzo ni misamaha ya kodi, pia madini na gesi , nyerere aiweza kwa korosho na chai, wao wataweza. Vipaumbele vitazingatiwa

Cuf wasema watatenga asilimia kubwa ya fedha ya serikali, fedha zipo shida ni vipaumbele.
 
Mrema of CHADEMA is smart too, safi vijana mnaotuwakilisha this time
 
Ahsante sana Jenerali Ulimwengu kwa uhitimishaji, umenifanya nifurahi kwa weledi wako
 
dah mdahalo umekwisha wakati ndo umepamba moto na kweli vijana wamekata nondo za uhakika.
 
Wadau vijana wa chadema wanatisha kwa kweli wamefunika leo movenpick na wamejipanga vya kutosha.ccm wameingia mitini tena na cuf walikuwa na msemaji mmoja mtatiro du chadema mwaka wetu??
 
Big up Ulimwengu, Very smart ma! ameweza kumudu vyema kuongoza mdahalo.
 
Angalua huyu jamaa wa CUF aliyeingia sasa ni kijana kidogo
halafu mbona CUF wanamtegea Mtatiro? au ndo kama Hamad Rashid alivyokuwa akiwabeba bungeni? CUF leteni watu compitent jamani

Mtatiro anajibu ndani ya muda. Sasa nyinyi kama mnaona hao wengine waakina Mrema wanaotoa maelezo mengi bila ya kujibu swali huku muda ukuiisha ndiyo utaratibu mzuri wa "kupeana zamu" na "siyo kubebana", bora muendelee na utaratibu huo. Wakati huo huo Mtatiro wa CUF anaenda right to the point na kumaliza kujibu swali within the given time frame.
 
Mdahalo haujaisha jamani msiondoke, leteni hoja tuzijibu hapa ukumbini.
 
SLAA AKAE MAKITABa???????

Kukusahihisha tu, alichosema John Mrema ni kuwa kama Slaa akiwa Rais atatengeneza utaratibu wa kujeng ama kuboresha maktaba kila wilaya na ataweka utaratibu wa kuzitembelea kadiri atakavyo weza ili kuhakikisha wanafunzi wanaendelea vizuri.
 
Wadau mtatiro julius amefumika mdahalo wa wagombea vijana leo movenpick,kwa kweli jamaa anatisha na ndugu mnyika ana kazi ngumu sana ubungo
 
Back
Top Bottom