Elections 2010 Mdahalo wa Wagombea vijana Movenpik 25/09/2010

A positive step in the long journey towards changes. They need to do many of these activities throughout their campaign to get members and supporters to join their parties. CCM wao bado wanakula matunda ya uhuru. Wamelala hawana shida ya kuelezea kwa wananchi nini wanapangilia kukifanya
 
Nimependa assumption yako mkuu
ila umenikera hapa
Nimempa Tsh 10,000/= ya bia a,efurahi sana na alamia,bia atakipigia Chadema kura. nika mwambia awashawishi na waudumu wenzie wakipigie chama ambacho kinaonyesha nia ya kuleta mabadiliko kwenye chi hii.
una bahati sikufahamu n ingekulengesha kwa TAKOKURU. next time tumia nguvu ya hoja kumkabili asiyeelewa ili achukue uamuzi sahihi usitumie njia wanazotumia CCM kuwahadaa watu
 
Na mie Bibi Ntilie nimekuja mjini toka kijijini (ambako hakuna umeme kwa hiyo hakuna TV) na nimeweza kuuona mdahalo wa vijana wanaowania kuchaguliwa kuwa Wabunge kutoka vyama vya CUF na CHADEMA. Naweza kudiriki kusema kwamba vijana wote (pamoja na wale walioonekana kama wazee!) wamejieleza vizuri lakini wa CHADEMA wameonekana kujieleza vizuri zaidi wakielewa nini chama chao kinasimamia na wakaeleza na kujibu kiufundi na kisomi zaidi kuliko wagombea wa CUF. Hata hivyo, waliokuwa wakipigiwa makofi zaidi ni CUF, hususan Mtatiro ambaye baadhi ya mambo aliyokuwa akieleza yalikuwa ni yaleyale ya CHADEMA lakini akayaeleza kwa namna tofauti na akapigiwa makofi hayo.

Pengine swali la kujiuliza ni kwa nini vijana wa CHADEMA - Halima Mdee, Zitto Kabwe, John Mnyika, Regina na Mrema hawakupigiwa makofi ya kutosha ingawa ndio walioeleza sera zao vizuri zaidi? Kwa nini hawakuweza kupata makofi ya nguvu hata pale walipojaribu kuwaeleza wasikilizaji jinsi wabunge wa CHADEMA wa bunge lililopita walivyofanya kazi kubwa ya kuichachafya serikali ya CCM bungeni? Yawezekana pia huenda wapiga makofi wale walikuwa ni wana CCM wenzangu ambao kwa kuwa hakuna mgombea wetu aliyejitokeza basi wakaamua ama walipangwa kuingia kwenye mdahalo kuwadhoofisha CHADEMA kwa kutowapigia makofi waliyostahili. Naambiwa eti Chama chetu CCM siku hizi hakiaminiki tena!

Lakini, upo upande mwingine wa shilingi kwamba huenda katika wakati huu tulionao wa joto la uchaguzi kupanda, kwenye kampeni ama midahalo ya aina hii wananchi wanapenda kusikia maneno ya kishabiki zaidi kuliko yale ambayo yanaweza yakawa na uzito mkubwa lakini hayagusi hisia za kishabiki!

Nawashauri vijana mnaowania kuchaguliwa mkiwa kwenye majukwaa mbalimbali muangalie aina ya wasikilizaji wenu, muwe makini mgundue haraka wasikilizaji wale wanataka kusikia nini kutoka kwenu na kwa lugha ya aina gani. Muwe tayari kubadilisha mbinu haraka pale mnapoona makofi hayawi mengi ipasavyo! Mnyika amchunge Mtatiro asijempoka tonge mdomoni.
 
Jamani tuwekeeni video basi kama kuna mtu ameweza kuinasa
 
Tusipowekewa mkanda huo wa mdahalo hapa basi ni kwamba cuf ndio walioongoza kwa hoja safi!!! Kama kweli chadema ndio wameongoza subutu tuwekeeni huo mkanda tuuwone musijifanye kuwa mumeshindwa kuuweka hapa!! Mbona mkanda wa kikwete alipoanguka mulituwekea? Na slaa akihutubia mbona picha zake huwa munabandika mara moja!!

Ukiona chadema wanapata kigugumizi cha kubandika mkanda ktk jf ujue wamezidiwa!!!!!
 
Duh! Hii kali. Yaani ccm siku hizi naiona kama mifisi fulani hivi, au mimbweha inayohangaika kujiokoa na mitego ya waadilifu. Wana kazi kweli kweli. Mpaka wanakimbia midahalo na ubabe wao wote?!

CCM wanafahamu fika kuwa wana madhambi mengi wanayowatendea watanzania na wanaona kwenda kwenye midahalo ni kwenda kuaibika na kukididimiza chama kabisa kwani hawana majibu ya kero zinazowakabili watanzania zilizosababishwa na utawala wao mbovu na wizi wa maliasili za nchi yetu.
 
Wekeni hapa huo mkanda basi wacheni blaaa..... Blaaa..... Nyingi hapa!! Tuonesheni kama nyinyi ni wakweli!!
 

hahaaa!umenifurahisha!ukampa rushwa ya elfu kumi ili apigie chadema yeye na wafanyakazi wenziwe....hahahaaa!
 
Wekeni hapa huo mkanda basi wacheni blaaa..... Blaaa..... Nyingi hapa!! Tuonesheni kama nyinyi ni wakweli!!

Kwa nini wewe usiweke, unangojea wanaume wa record wanunue bandwidth halafu wakuwekee tena unadai kama vile umelipia. Eboo
 
Ukiona chadema wanapata kigugumizi cha kubandika mkanda ktk jf ujue wamezidiwa!!!!!

Mimi nadhani kama una amni CHADEMA walichemsha ungetakiwa uwe wa kwanza kuuweka hapa ili uwaumbue, sasa unapodai CHADEMA waweke mdahalo hapa as if wao ndiyo kila kitu unajishusha mkuu, hata wewe unaweza kufanya mambo makubwa kama CHADEMA
 
Wadau mtatiro julius amefumika mdahalo wa wagombea vijana leo movenpick,kwa kweli jamaa anatisha na ndugu mnyika ana kazi ngumu sana ubungo

Mtatiro anajulikana Manzese tu ukienda Kimara mpaka Mbezi huko hawamjui huko ni Mnyika tu mpaka Mabibo ni Mnyika tu
 
Mtatiro anajulikana Manzese tu ukienda Kimara mpaka Mbezi huko hawamjui huko ni Mnyika tu mpaka Mabibo ni Mnyika tu


Ha ha ha hata manzese nina shaka mkuu, nilikuwa Pale tip Top kwa jamaa wauza Magodoro, yaani wao Mnyika ni kama ilivyokuwa kwa Watanzania na Jeikei wao 2005! Mtatiro ni Kijana Mpiganaji Ameogombea Ubunge akijua kabisa Hatashinda but Mnyika asishinde vile vile, ila Kwa Dar Mkuu this time wabunge wengi watashinda kwa <50%
 

Mkuu umetumwa nini? Mbona wamesahau kukutuma kwenye mdahalo ukawawakilishe???
 
Tukiacha ushabiki ukweli ni kwamba Mtatiro alifunika jana.. Japokuwa mdahalo ule ulikuwa na wananchi ambao walionekana kama ni wa CUF kwani yale makofi na mapango ya picha za wagombea wa CUF inazihirisha walikuwa wameandaliwa kwa kazi hile.
 

Acha uongo wako wa kujifanya wewe CCM. Ule ulikuwa mdahalo, unatakiwa kuonyesha uwezo wa kujibu maswali haraka na kwa muda uliowekewa. Ule ilikuwa siyo RTD ya Nyerere aliyekuwa anaongea masaa 3 mfululizo bila ya kuzingatia muda na kubaki kuchekacheka.

Wazungumzaji wa CHADEMA walibaki kujisifia kuwa wao ndiyo wamefanya hivi na wao ndiyo wamefanya vile kwenye bunge. Yaani watu 11 wanaweza kutufanya sisi tuamini kuwa ndiyo waliopitisha sheria mpya ya madini? Swali la vipi mtapiga vita na kuondoa kero ya ufisadi, jibu linaanza kuelezea historia ya bunge liliopita matokeo yake swali halijibiwi na muda unaisha. Ukiulizwa 1+1 ni ngapi na una muda mdogo wa kujibu na ukaanza kueleza kuna robo ngapi kwenye hiyo moja na kuna nusu ngapi kwenye kila moja ya hiyo moja, hayo ni matatizo ya wazungumzaji wenu. Wakulaumiwa siyo wazungumzaji wa CUF!
 
Mtatiro anajulikana Manzese tu ukienda Kimara mpaka Mbezi huko hawamjui huko ni Mnyika tu mpaka Mabibo ni Mnyika tu

Huko Kimara na Mbezi si ndiyo walipojazana Wachagga? :becky:
 

Yeah right. Katafute data na jiulize huko Manzese, kuna serikali za mitaa mingapi inayoongozwa na CUF halafu ndiyo uje na pumba hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…