Kiukweli kazi bado tunayo tena kubwa sana, nilikuwa njiani kurudi nyumbani nilipo chungulia JF mara moja nika kutana na hii topic, ilinibidi nisitishe safari ya kwenda nyumbani na nika pita bar ilitu niweze kutizama huo mdahalo. Wakati mdahalo unaendelea muudumu wa bar akasikikia akisema "hamna lolote nyie wezi tu na kura hampati" wakati huo alikuwa anazungumza Zitto, baada ya mda nilimuita na kumuuliza
M: kwa nini umesama hawana lolote, ni akina nani wenye lolote?
Muudumu: Chadema/CUF wote wezi tu na kura hawapati mwaka ,CCM ndio wenyewe bana
Mganyizi: Ok, Kwa hiyo mwaka huu utapigia chama gani kura na ni sababu gani zitakufanya ukipigie kura?
Muudumu: CCM kwa sababu na kipenda isitoshe viongozi wake wanapesa
Mganyizi: dah! utakipigia kura kwa sababu unakipenda na siyo kwamba kimefanya mengi ya kwa taifa hili
huoni jinsi wanavyo tumia madaraka tuliyowapa vibaya?
Muudumu: ndiyo ni kwa sababu na kipenda na Mbunge fllani (akamtaja jina ) ni bwana angu
Mganyizi: Dah hiyo kali kwa kweli, na kushauri ufikirie uhamuzi wako juu ya kura yako usiitumie vibaya kwa kuwapa watu wasiyoweza kubadilisha maisha yako kwa miaka 49 sasa...
Muudumu: sawa nitafikiria kuhusu hilo, naomba ninunulie bia Kaka...
Kwa kweli huyu muudumu amenishagaza sana kwa majibu yake, ukweli ni kwamba watanzania wengi wenye helimu ya chini na wasiyo na kipato cha kutosha wako nyuma sana kifikra na ndio type ya huyu muudumu wa bar"ni mdada mzuri kweli kweli sema hana elimu ndio maana yuko bar sehemu ambayo hakustahili kuwepo pale the way alivyo jaliwa.
Nimempa Tsh 10,000/= ya bia a,efurahi sana na alamia,bia atakipigia Chadema kura. nika mwambia awashawishi na waudumu wenzie wakipigie chama ambacho kinaonyesha nia ya kuleta mabadiliko kwenye chi hii..