Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu WoS;
Hii nayo ina shida gani?
lol basi member wa JF mtakutana wengi huko kwenye TV......FMES nae alisema atakuwa huo mshkaji wake aatafungua tv station......mtuwakilishe wana JF uko...- Mkuu wasalaam, kumbe na wewe uko njiani, basi tutakutana huko karibuni maana TV station ya jamaa yangu bado inasua sua lakini iko kwenye matayarisho ya mwisho ilikuwa ifunguliwe Jan, lakini ikakwama kidogo, pia waliamua kuhamia kwenye makao yao, anyway naona tutakutana huko soon!
nb; Vipi Bado uko kwenye line ile ile ninataka kukutwangia, ni-PM.
Ahsante.
William.
Mkuu WoS;
Hii nayo ina shida gani?
lol basi member wa JF mtakutana wengi huko kwenye TV......FMES nae alisema atakuwa huo mshkaji wake aatafungua tv station......mtuwakilishe wana JF uko...
......kwanza jamaa yako tv yake anataka iwe ya kibiashara yaani a make profit au kalenga zaidi kuelemisha jamii profit nyuma?
Hii inafanana na manabii fulani hivi... siyo Allien mnaokaa outerspace!
You can't please everyone. uki jaribu utaumwa bure.
Maoni hapa yatajaza eneo hili. Lakini nikileta barua ya kuomba kibarua, unisabilie hiyo Newsroom hapo nitaambatanisha na- plan of action. Kila la kheri Mkuu.Mkuu, huna maoni yoyote mbali na kuomba kibarua?
Allien,
Unaweza pia kuazima jani toka CNN. CNN won the battle of news audiences kwa kuhakikisha wanakuwa watu wa kwanza kuweka kamera kwenye tukio.
Na kuonesha kuwa hawabeep waliwafunika ITV vibaya mno siku ile Osama alipofanya mambo yake Dar es Salaam.
Hakuna aliyeamini eti picha za embassy bombing zinarushwa live na CNN ndani ya nusu saa tu toka tukio litokee wakati local media (kuanzia TV mpaka redio) bado wamelala.
So whatever you plan to do, when it comes to news you have big room. Hakuna live coverage za kutosha, na TV zetu haziwahi kwenye matukio.
Program nyingine zinazopendwa ni Reality Shows. Wabongo washakunywa mvinyo wa Big Brother, Star Search na kwa wenye madish Survival, etc.
Juzi juzi kuna wadau walilocalize mambo na kutengeneza Maisha Plus, wamepata response nzuri ... I am sure mwakani Maisha Plus itakuwa show moja itakayotazamwa sana.
So angalia uwezekano wa kuwa na Reality TV programs pia.
Mwisho kabisa mvuto wa watangazaji. Kuna TV bado hazielewi kuwa TV ni showbiz ... wanaweka watangazaji hawana hata mvuto.
Kina mama na kina dada wanataka kuona vijana handsome, na kina kaka wanataka kuona mademu bomba kwa TV. Usisahau hilo.
Kila la heri.
Wana JF,
Kuna mdau anataka ku-invest katika TV Station DSM na sasa anaandaa Mchanganuo kwa ajili hiyo ili kuufikisha katika vyombo husika by January 2010.
Anapenda TV atakayoianzisha iwe na mambo yafuatayo:
- Iwe na vipindi vya kuvutia sana kiasi kwamba kila anayefungulia asihamie channel nyingine.
- Iwe inaelimisha katika mambo ya msingi ambao Watazamaji watajifunza na yatawasaidia.
- Isaidie Kupiga Vita Ufisadi
- Isaidie kubadilisha Attitude ya Watanzania katika kujiletea maendeleo
- Isaidie katika kuondoa umasikini kupitia vipindi vyake
- Isaidie katika suala zima la Ujasiliamali.
Inatakiwa zaidi ya 60% ya vipindi viwe local programs (Local Content) na chini ya 40% vinaweza kuwa vipindi vya nje (Foreign Content).
- Pia Entertainment, Michezo, Vipindi vya watoto nk. nk.
Je ni nini mawazo yako juu ya vipindi mbalimbali na viendeshwe kwa staili gani ili kufanikisha malengo yake?
Mkuu hili wazo zuri lakini sisi wengine ktk maswala haya huwa tunalipwa hatufanyi kazi ya kanisa ktk biashara...Na maadam kaomba basi mwambie tuwasiliane.
Sharti la kwanza ajiunge JF...
Ni Africa pekee mtu anaweza kutazama TV akiwa na njaa. Watanzania wote mnataka kuwekeza kwenye mambo ya show afu mashamba sijihi alime nani?
WaSaudi wakitaka kupewa ardhi mnalalamika.
Mkuu ina maana wewe unafanya kazi 24/7?
Kwanu uoni miguu yangu?