Mdau: Baada ya baba kupotea, rafiki yake ametuma watu wenye silaha kuvamia nyumba yetu akitaka tuhame

Mdau: Baada ya baba kupotea, rafiki yake ametuma watu wenye silaha kuvamia nyumba yetu akitaka tuhame

1.Je, huyo unayemwita Kilumile anatoa hoja Zipi hasa za kudai kwamba hiyo nyumba ni mali take?? Uhalali wa madai yake uko wapi baada ya nyinyi kumsikiliza madai yake??
2.Baba yenu hiyo ardhi aliipataje??Yaani historia ya umiliki wa ardhi kwa baba yenu ikoje??
3.Ina maana mama yenu hajui kitu chochote kuhusiana na upatikanaji wa hicho kiwanja ambacho baba yenu alijenga nyumba??
4.Wakati baba yenu alipopotea, Je, mlifuata hatua zozote zile ktk kushughulikia suala hilo?Je, mliripiti Polisi na kupata nyaraka zozote zile za upotevu wa huyo baba yenu kutoka Polisi au kutoka katika Mamlaka yoyote ile ya Serikali??
5.Baada ya purukushani za huyo Kilumile kudai kwamba nyumba aliyojenga baba yenu ni mali yake, Je, nyinyi kama watoto mlichukua hatua gani za kumhusisha Bw. Kilumile kuwa ni mshukiwa namba moja wa tuhuma za upotevu au kutoweka kwa baba yenu??Je, mmejaribu kuripiti Polisi kwamba Bw. Kilumile ndiye mhusika wa tukio la kupotea kwa baba yenu??
6.Baba yenu alikuwa na hisa kiasi gani kwenye umiliki wa hiyo kampuni ambayo sasa ipo chini ya usimamizi wa Bw. Kilumile??
7.Je, nyinyi kama watoto mlichukua hatua gani ktk kujihusisha na kampuni hiyo aliyoiacha baba yenu mara tu baada ya baba yenu kutoweka ktk mazingira ya kutatanisha??

Bado Nina maswali mengi sana kuhusu hili suala lenu, isipokuwa muda wa kuandika hapa sina wa kutosha ili kuweza ku-deal ipasavyo na hili tukio.
Watoke ardhi yangu haraka
 
Watu huwa mmasumbuka buree wakati mnaweza tatua shida zenu. Nendeni kwa waganga konki hapo malawi mtamjua mbaya wenu ni yupi na mzee yupo wapi. Mnaweza chukua hatua kali za kumlarua mbaya wenu either yeye binafsi au na wanae/mkewe maana mchuma janga hula na wakwao. Amkeni nendeni malawi au nendeni kongo hapo biashara mtamaliza jua la saa nne, mkirudi watu hawapo hai tena. Zaidi ya hapo mtageuka makaini mchini.
 
Andiko la Mdau wa kutoka Goba kuhusu watu wanaotaka kupora nyumba yao baada ya baba yao kupotea:

Usiku wa kuamkia leo Alhamisi Julai 6, 2023 kuna watu wamevamia katika nyumba yetu iliyopo Goba, Mtaa wa Kiburuni, Dar es Salaam na kuanza kuvunja sehemu ya nyumba, ikiwemo madirisha na milango, baada ya hapo wakamjeruhi ndugu yetu mmoja na kusema kuwa kama hatutahama kwenye nyumba hiyo watarejea kesho yake ambayo ni usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 7, 2023.

Wahalifu hao walifika wakiwa makundi, wanne wakaingia ndani na wengine ambao sijui idadi yao walibaki nje, majirani wanasema kuwa walikuwa na silaha za moto ndio maana hata wao walisita kutoa msaada kwa haraka.

Walikuwa wanamtaka kiongozi wa familia ambaye alikuwa katika chumba kingine, wakati akifanya uharibifu huo wakamchukua ndugu yetu mmoja na kuanza kumpiga huku wakimtaka aseme alipo ndugu yetu ambaye ni mtoto wa kwanza wa mzee.

Alikataa kutii kile walichotaka na wakaendelea kumpiga hadi alipopata nafasi ya kuwatoroka na kwenda kuripoti Polisi.

Polisi walikuja baadaye wakakuta wahalifu wale ambao tunaamini wametumwa na aliyekuwa rafiki wa baba yetu kwa kuwa ndiye ambaye tuna mgogoro naye wa nyumba tunayoishi.

Kwa nini rafiki wa baba anahusishwa?
Anahusishwa kwa kuwa mshukiwa anayefahamka kwa jina la Thomas Daniel Kilumile, mzaliwa wa Iringa ambaye kwa sasa anaishi Mwanza, alikuwa ni kama ndugu kwetu wakati baba alipokuwa nasi.

Wawili hao walikuwa marafiki na hata kufikia hatua ya huyo rafiki yake kuwa anakuja kwenye nyumba yetu analala na kwa pamoja walikuwa wakimiliki kampuni.

Walikuwa wafanyabiashara walioshirikiana muda mrefu, ghafla Mwaka 2018 baba akiwa ametoka na gari kwenda kwenye mizunguko yake ya kawaida hakurudi tena mpaka leo.

Hatujui kama ni mzima au ameshakufa na hata gari lake pia halikuwahi kuonekana.

Rafiki wa baba aanza kudai nyumba
Baada ya baba kupotea, ndugu tukaanza kufuatilia madeni na biashara zake alizokuwa anafanya, hapo ndipo sokomoko likaanza, huyo Thimos akaja kudai kuwa nyumba tunayoishi ni mali yake na tunatakiwa kuhama.

Mgogoro ukaanzia hapo, tukamtaka aende Mahakamani ili haki ipatikane, hakufanya hivyo, aliishia kwenda Polisi na suala letu lilifika hadi Serikali za mtaa lakini hakukuwa na utatuzi uliopatikana.

Nyaraka za nyumba zinaonesha zina jina la baba yetu aliyepoteza lakini Kilumile alikuja na nyaraka anazodai ni za kiwanja na kuwa kile ni kiwanja chake.

Kinachoshangaza ni kuwa rafiki huyo wa baba hakuwahi kusema chochote kuhusu umiliki wake wa nyumba hiyo, na kwa kinachoendelea tunapata mashaka kupotea kwa baba na hiki kinachoendelea.

Vitisho
Mzee Kilumile alianza kutupa vitisho yeye na mwanaye ambaye inadaiwa ni Mwanajeshi wakitutaka tuhame, shauri lilifika Kituo cha Polisi Goba, kwa kuwa alikosa ushahidi akawa ni kama ameshindwa kuendelea.

Nyumba hiyo ilianza kujengwa Mwaka 2011 na ikakamilika Mwaka 2014 ambapo ndipo familia ikahamia.

Mama yetu hayupo hapa anaishi Mwanza, aliwahi kusema rafiki wa baba anataka kutupora nyumba yetu kinyume cha sheria.

Kwa kuwa rafiki huyo wa baba mtoto wake ni mwanajeshi, amekuwa akidai kuwa lazima atatuhamisha na kwa mazingira yanayoonekana sasa inaonekana kuna vitu ambavyo anaweza kuhusika kwa kupotea kwa baba.

Tulitegemea pia baada ya baba kupotea angekuja kutuambia kuhusu biashara aliyokuwa akishirikiana na baba, tulipomuuliza hakuwa na majibu.

Mikopo hiyo. Hakuna watu wanakuja na Silaha. Mchana mda wote huo wawe wahalifu.

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(DAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY)
AT DAR ES SALAAM
MISCELLANEOUS CIVIL APPLICATION NO. 479 OF 2022
(Originating from the High Court of Tanzania, Dar es Salaam
District Registry in Civil Case No 167 of2016)
CRDB BANK PLC............................................................................ APPLICANT
VERSUS
TIMOTH DANIEL KILUMILE CO. LTD.....................................1st RESPONDENT
DAWSON BUBERWA ISHENGOMA........................................2nd RESPONDENT

Baba yako hayupo hapo? Inawezekana baada ya Baba yako kupotea, jamaa akalipa deni lote, na labda hiyo Nyumba ndo ilikuwa bond, ninaamini ana haki of some sort
 
Okay, ndio maana Mimi niliwauliza maswali mengi kwenye post yangu ya awali hapo juu na mleta uzi hakujitokeza kuja kuyajibu kwa sababu anajua kilichopo nyuma ya pazia. Njia ya muongo ni fupi.
Yeye alidhani hapa Jf kuna watu wajinga tupu kama alivyo yeye kiasi kwamba anaweza kuwadanga kiurahisi.
 
Mikopo hiyo. Hakuna watu wanakuja na Silaha. Mchana mda wote huo wawe wahalifu.

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(DAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY)
AT DAR ES SALAAM
MISCELLANEOUS CIVIL APPLICATION NO. 479 OF 2022
(Originating from the High Court of Tanzania, Dar es Salaam
District Registry in Civil Case No 167 of2016)
CRDB BANK PLC............................................................................ APPLICANT
VERSUS
TIMOTH DANIEL KILUMILE CO. LTD.....................................1st RESPONDENT
DAWSON BUBERWA ISHENGOMA........................................2nd RESPONDENT

Baba yako hayupo hapo? Inawezekana baada ya Baba yako kupotea, jamaa akalipa deni lote, na labda hiyo Nyumba ndo ilikuwa bond, ninaamini ana haki of some sort
Kama alilipa kwanini hakuishirikisha Familia waone wanalilupaje? Huyo ni tapeli tu
 
tatizo la siku hizi ma baba wengi wakiwa wazi na mali zao wanaona wanajipeleka makaburini kabla ya kuwapa urithi.
sio tu kupotea kuna mzee arifakiri kamuachia mtu kuendesha na kusimamia miradi huku familia ifahamu lolote.
jamaa kajimilikisha na buyu kali sababu kila document na kinachoendelea anajua kilipo.
 
Hiyo biashara ndiyo chanzo cha haya. Soon wanakuja wabobezi wa kazi zao watatuambia pale mexco biashara inaendaje
 
Mikopo hiyo. Hakuna watu wanakuja na Silaha. Mchana mda wote huo wawe wahalifu.

IN THE HIGH COURT OF TANZANIA
(DAR ES SALAAM DISTRICT REGISTRY)
AT DAR ES SALAAM
MISCELLANEOUS CIVIL APPLICATION NO. 479 OF 2022
(Originating from the High Court of Tanzania, Dar es Salaam
District Registry in Civil Case No 167 of2016)
CRDB BANK PLC............................................................................ APPLICANT
VERSUS
TIMOTH DANIEL KILUMILE CO. LTD.....................................1st RESPONDENT
DAWSON BUBERWA ISHENGOMA........................................2nd RESPONDENT

Baba yako hayupo hapo? Inawezekana baada ya Baba yako kupotea, jamaa akalipa deni lote, na labda hiyo Nyumba ndo ilikuwa bond, ninaamini ana haki of some sort
mkuuu una elekea level ya mfunyukuzi aisee uko juuuu
 
Huyo Kilumula anajua alipomzika baba yenu, kazi kwenu, mnatakiwa kumkamata huyo mtoe maelezo polisi ahojiwe kwa kina juu ya kupotea baba yenu nae akiwa kama rafiki yake wa karibu, lazima atakuwa anajua kitu, haiwezekani awe na tamaa na mali ya marehemu bila sababu, naamini hiyo tamaa yake ndio iliyochangia kumpoteza baba yenu.

Akamatwe na kuhojiwa.
 
Huyo mdhulumaji ndio kampoteza baba yenu, kesi ianzie hapo
"No research no right to speak".
By Mao, a former Chairman and the founder of CPC, China.

Not only that, but also, "He who alleges must prove".

Kwa muktadha huo, mleta hoja hajathibitisha madai yake, kwa sababu madai au hoja yake inaibua na inaacha maswali mengi zaidi bila majibu.
Kwa mantiki hiyo, kwa sasa ni vigumu sana kumtuhumu kwa utapeli huyo mtu wanayemtaja kuwa ni Kilumile. Mleta hoja kwanza anapaswa kuthibitisha madai yake kwanza kabla ya kumgeukia huyo Kilumile.
 
Back
Top Bottom