MDAU: Blacks and Arabs ni races zenye upumbavu wa Milele.

MDAU: Blacks and Arabs ni races zenye upumbavu wa Milele.

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Je unakubaliana na Infropreneur
Screenshot_20241103-152439_1.jpg
 
Inategemea na yeye huyo muhusika anavyojiona.

Anavyojiona ndio hivyo anawaona na wengine na kujidhani kuwa yeye ndiyo hao.

Nakuambia kiakili kicivilization kimaendeleo tupo watu tusiooona huo utofauti wa makabila/races kwamba huyu yupo vile na hawezi kuwa vile.

Mi naamini yeyote anaweza kuwa yeyote. Hata yeye.

Huyo aliyetania kuhusu wasukuma atambue sio kabila wala vinasaba bali ni utamaduni, culture. Msukuma anapoishi na kuamini Mungu ni LIWELERO ana muitikio tofauti kabisa na mtu atakayeamini kuwa mungu wake ni binafsi na anaishi chini ya dari ya nyumba yake.

Mmoja atakuwa mkarimu kwa ndugu ambao ni ulimwengu mzima (Mungu universal), mmoja hata jirani zake tu atawaona ni watu wa nje (mungu wake binafsi). Ni imani na vile mtu anajiona ukihusianiaha na watu wengine bwana Infropreneur
 
Huyo jamaa ni mfano hai wa mada yake mwenyewe. Watu ambao ni wachache sana one might say.

Sitoongelea kuhusu waarabu sababu siwajui na wala hatufanani kivyovyote, na nina uhakika huyo genius anaongelea waarabu sababu yuko biased kidini. Bila shaka ni Christian. Religious indoctrination is a dangerous thing.

Naona anaongelea wazungu akimaanisha Europeans, kama the Paragon of civilization. Labda sababu ya mafanikio yao, kitu kinachodhihirisha upumbavu wake anaousema. Sababu kama angekuwa na akili chache hata za kuvukia barabara basi angegundua Europeans ndio walioleta ukoloni Barani Afrika, waligeuza mababu wa kiafrika watumwa, wakawatumikisha kama wanyama bila chembe ya huruma, kuwatesa, na kuwaua. Hivyo Europeans sio wapumbavu tu wasiopenda amani, bali ni washenzi na makatili. Na hawakufanya ushenzi Afrika tu, bali dunia nzima. Ikiwemo kwenda kuchukua ardhi za watu kinguvu na kuwaua wenyewe, au anadhani Marekani ni ardhi ya wazungu ile? Vita vya dunia walikuwa wanapigna kina nani kama sio Wazungu? Au Hitler alizaliwa kimbiji na alikuwa mweusi?

Wazungu ni matajiri sababu ya ukatili walioufanya, hivyo utajiri sio morality na Umasikini sio upumbavu, sababu ulikuwa moral enough kutofanya ukatili kwa wengine ili ufanikiwe wewe.

Huu ni ujinga uliopitiliza viwango.
 
Back
Top Bottom