Haya ni maoni yangu:
Binafsi napenda sana kuona siku moja watanzania kwa mamilioni nchi nzima wanaandamana kudai mabadiliko. Hata hivyo,, kwa sasa naona ni vigumu kwasababu mbalimbali mojawapo ikiwa ni hii mbinu ya kupanga tarehe fulani kuwa ni siku ya maandamano.
Kwa Tanzania yetu hii, maandamano yanapaswa kuwa ni jambo la kushitukiza mara tu pale linapoktokea jambo la kuumiza na kukera watanzania mfano kile kitendo cha kundi ka Polisi kumshambulia raia mmoja pale Mahakama ya Kisutu hivi karibuni.
Kwahiyo, ili maandamano yafanikiwe, watanzania wanapaswa waandaliwe kisaikolojia kuandamana kwa wingi pale panapotokea matendo ya kinyama na mambo mengine kama kauli za kejeli na Viburi kutoka kwa watawala bila kutangaza tarehe maalumu ya maandamano na kutoa fursa kwa vyombo vya dola kujipanga.
Hivyo, japo naamini watanzania wengi kwa sasa wana machungu na hasira kutokana na vitendo kama mauji, utekaji, chaguzi fake, wizi, ufisadi, uminyaji wa demokrasia,. n.k, bado wengi hawataandamana na ninaona kati ya watanzania 100, ni watanzania 10 tu ndio wanaweza kujitokeza kuandamana na maenreo mengine hawatajitokeza kabisa.
Kuhusu upigaji kura: kwa jinsi nchi inavyoendeshwa na hali halisi ya mambo ilvyo, Oktoba 29 ni watanzania wachache sana watajitokeza kwenda kupiga kura. kwasbabu watanzania weng hawaoni kama kuna uchaguzi zaidi ya maigizo tu.
Hivyo, ni imani yangu, katika watanzania 100, ni watanzania 10 tu ndio watakuwa tayari kupiga kura tena zaidi vijijini na mijini hali inaweza kuwa mbaya zaidi.
CCM mmelikoroga, subirini kuona matokeo siku si nyingi.
Click to expand...