LGE2024 Mdau, yapi maoni yako ya Jumla kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024?

LGE2024 Mdau, yapi maoni yako ya Jumla kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
1.Uchaguzi haukuwa na haki na huru
2.Mwitikio wa watu kujitokeza kupiga kura hakuwa mzuri mfano Eneo langu la mtaa walioandikishwa kupiga kura ni 3764 na waliopiga kura ni 280 kwa mujibu wa mawakala waliokuwa wanatunza kumbukumbu ktk vituo vyao.
3.vyama vilishawishi watu ila watu wakiuliza je kura zetu hazifai wa? na kwa wagombea eneo letu ktk kampeni alipata haki sawa za mikutano
4.vijana na wanawake waljitokeza na kugombea
5.uboreshaji kwa uchaguzi 2025 ni kuwa na tume huru na sio mfumo huu tulionao wa wakuu wa mikoa na wilaya,wakurugenzi,watendaji wasihusishwe ktk uchaguzi ilishindikana kusiwepo na uchaguzi CCM washiriki wenyewe.tumeona kura bandia zikiandaliwa na hao.
6.ukuaji wa demokrasia nchi ni Tanzania hakuna bado sana na nigelesha
 
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024: Changamoto, Mafanikio, na Mustakabali wa Demokrasia Yetu

Novemba 27, 2024, Watanzania walishiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa lengo la kuchagua viongozi wa vijiji, vitongoji, na mitaa. Uchaguzi huu, kama chombo muhimu cha kukuza ushiriki wa wananchi katika uongozi wa maeneo yao, umekuja na matukio mbalimbali yanayostahili kujadiliwa kwa kina.

Maswali Muhimu:​

  1. Mchakato wa Uchaguzi: Je, uchaguzi ulikuwa wa haki na huru? Kuna changamoto zipi zilijitokeza kabla, wakati, na baada ya upigaji kura?
  2. Ushiriki wa Wananchi: Je, mwitikio wa wananchi ulikuwa wa kuridhisha? Ni kwa nini baadhi ya watu hawakushiriki ipasavyo?
  3. Nafasi ya Vyama vya Siasa: Vyama vya siasa vilipata nafasi gani katika kushawishi uchaguzi huu? Je, wagombea wa vyama vyote walipata haki sawa?
  4. Ushiriki wa Vijana na Wanawake: Je, makundi haya yalihamasishwa ipasavyo kushiriki au kugombea nafasi za uongozi?
  5. Mafanikio na Mapungufu: Ni nini kilichofanikiwa, na ni maeneo gani yanahitaji kuboreshwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025?
  6. Mustakabali wa Demokrasia: Je, uchaguzi huu umeonesha ukuaji wa demokrasia nchini au bado kuna changamoto kubwa zinazohitaji kushughulikiwa?

Tunakaribisha mawazo, uzoefu, na mapendekezo yenu. Tafadhali shiriki kwa hoja za msingi na mifano halisi ili kujenga mjadala wenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu.

Jiunge na mjadala huu, tusaidie kubaini njia bora ya kuimarisha demokrasia yetu!
Ule ulikuwa uchafuzi si uchaguzi, kuanzia uandikishaji hadi uchafuzi wenyewe.
 
Back
Top Bottom