Hoja ya mbunge wa viti Maalumu Halima Mdee kuhusu Sh10 bilioni imeendelea kutikisa katika mitandao ya kijamii wengi wakihoji alipata wapi kiasi hicho.
Hata hivyo jana Mdee alizungumzia jambo hilo na kukanusha kuwa hana kiasi hicho kwenye akaunti yake bali amesema kwa maana ya kufikisha ujumbe kwa Serikali.
“Ni kweli nilisema, lakini kwa namna nyingine watu wasingenielewa bali nilikuwa natumia njia hiyo kufikisha ujumbe kwa Serikali, hivi katika usawa huu mtu uwe na kiasi hicho si mambo yatakuwa mazuri sana, ule ulikuwa utani,” alisema Mdee akiwa nje ya ukumbi wa bunge.