Mdhamini mkuu wa Yanga GSM kudhamini timu nyingine saba za ligi kuu siyo fair

Fly emirates anadhamini timu moja kwenye ligi ,kama madrid tu kwenye ligi yao
Nafikiri umeanza kufuatilia soka miaka ya karibuni au huna taarifa sahihi na unachokiongea mzee. Basi Ngoja nikupe taarifa sahihi .Fly Emirates amewai kuwa mdhamini mkuu wa Chelsea na Arsenal pale EPL Kwa wakati mmoja. Pia club zifuatazo ndio zinadhaminiwa na fly Emirates Kwasasa na zinakutana mara nyingi tu
AC Milan

Arsenal F.C.

Olympique Lyonnais

Real Madrid

S.L. Benfica
PSG
 
Simba wanaweweseka sana, sio sifa ya simba kuwa ivyo na mpigwe tu hamna namna
 
Ficha ujinga wako. Babra hakushinda kuizuia GSM kudhamini ligi nzima, alishinda Simba isiweke nembo za gsm kwenye matambala yake. Kwa kuwa gsm alitaka timu zote zimtangaze simba ikagoma, hivyo deal likafa maana haitakuwa ligi tena.

Sasa pata shule hapa
Tuhuma zilizopo, kwamba hakuna fair competition katika ligi ya Tanzania sababu GSM anafadhili (sponsors) clubs nyingi tanzania hazina mashiko, ni kowango cha juu cha ujinga. Zinatajwa:-

1. Yanga
2. Coastal
3. Singida
4. Pamba
5. Namungo.
6.

Haya tunaijibu kwa kuiangalia Umbro ndani ya EPL ligi kubwa duniani.

Umbro sponsored Teams in EPL

1. West Ham United.
2. Ipswich Town FC.
3. Brentford FC.
4. Hearts FC.
5. AFC Bournemouth.
6. Huddersfield Town.
7. Luton Town.

Kwa majibu haya, tuendelee na mjadala au tuufunge?

Simba wekezeni kwa kusajili wachezaji wazuri. Hoja mnazoleta ni utoto mtupu na ishara ya kushindwa mashindano. Mlizoea kuzifunga timu ambazo hazina hata nauli, wamepata wafadhili, wanasafiri, wanalala hotel, wanakula, wanakunywa, wanalipa mishahara, halafu nyie mnatamani wapokonywe ufadhili huo warudi nyuma?

Kama mnadhani ni rahisi, mwambieni Mo aaxhe kutoa mikopo umiza afadhili timu zote zilizobaki halafu mje tushindane
 
Kazidhamini wewe basi; unataka zisipate mdhamini ili iweje.
 
Angalia wadhamini wa Namungo:
(1) Azam Max
(2)Shananga Group
(3)Bluewave Cargo
(4)GSM
(5)Sportpesa


 
1. GSM siyo main club sponsor lakini ni sponsor wa Yanga. Main club sponsor anapewa eneo kubwa kujitangaza, ni SPORTPESA
2. Kosa lingine mnalifanya ni kudanganya GSM anaimiliki Yanga. Hadi sasa Yanga hatuna mwekezaji. Gsm ni club sponsor lakini pia ni mfadhili. Mfano amefadhili mchakato wa mabadiliko ya club.
3. GSM kudhamini club zaidi ya moja, siyo kampuni ya kwanza, zipo nyingi zimefanya hivyo. Sportpesa ina vilabu kadhaa, MBET wanafadhili KMC na Simba sc, Azam anafadhili ligi yote na ana timu ndani ya ligi, DSTV ndiye mwenye ligi south africa na ana timu inaitwa supersport utd hivyo siyo suala geni dunia.
4. Wakati GSM akiwa na Yanga, Coastal, Namungo, Singida big stars na Pamba, UMBRO ya EPL Inafadhili Wets Ham, Ipswitch, brentford, AFC Bournemouth, Huddesfield na Luton

Hamna Hoja
 
GSM NI TAPELI LENGO NI KUIKOMOA SIMBA WANA KISASI CHA MANJI ALICHOFANYWA
 
Hoja yako inaweza kuwa valid kwa kuiangalia kinadharia ingawa ukija kimatendo hoja yako sio sahihi. Ningekuelewa iwapo hizo timu zinazodhaminiwa na GSM hazitoi upinzani kwa Yanga. Mathalan, ligi ya 2023/2024, timu za Coastal na Namungo (zina udhamini wa GSM) zilitoa upinzani mkubwa sana kwenye michezo yao na Yanga. Wakati huo timu ambazo hazidhaminiwi na GSM mfano KMC na Simba zilibugizwa magoli mengi na Yanga (mechi moja goli 5). Hatua ya udhamini tuliyofikia tuliililia kwa muda mrefu. Hivyo, ni muhimu kuendelea kuwatia moyo wadhamini waliopo na kuwaomba wengine waingie kudhamini timu zetu. Hii itatusaidia kuwa na timu imara katika mashindano ya ndani ya nchi na kimataifa.
 
GSM anadhamini timu zaidi ya 7 halafu anasema Yanga Bingwa. We hauogopi?
 
Madhamini mkuu wa Yanga ni Sportspesa sio GSM
 
Mifano uliyoleta tofauti kabisa... Iko ivi haitakiwi mdhamini/mmiliki mmoja kuwa kwenye timu zaidi ya moja kwenye loko ligi(ligi ya ndani), na hii kitu unaipata Tanzania pekee.
 
Mifano uliyoleta tofauti kabisa... Iko ivi haitakiwi mdhamini/mmiliki mmoja kuwa kwenye timu zaidi ya moja kwenye loko ligi(ligi ya ndani), na hii kitu unaipata Tanzania pekee.
Nimekuletea mifano ya ligi na nchi nyingine unasema sio mifano sahihi afu mwisho unamaliza hii iko Tanzania pekee !,Nakosa namna ya kukupa elimu aseeh.Basi kama unaona ni Tanzania pekee basi wewe hujui au hufuatilii mpira kabisa maana ata nikikuambia ulete kifungu cha sheria iyo utaweza kweli. Fuatilia mpira sio mapenzi ya timu
 
Mifano uliyoleta tofauti kabisa... Iko ivi haitakiwi mdhamini/mmiliki mmoja kuwa kwenye timu zaidi ya moja kwenye loko ligi(ligi ya ndani), na hii kitu unaipata Tanzania pekee.

Nani aliyesema haitakiwi? Ni wewe au ni FIFA au nani aliyesema haitakiwi?
1) Adidas wana sponsor
Arsenal, Fulham, Man united

2) Nike wana sponsor
Brighton, Chelsea, Liverpool na Tottenham

3) Umbro nao wana sponsor timu zaidi ya moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…