Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

vita ya madwa ya kulevya inasimamiwa na Kamishna Sian'ga na mpaka sasa amekamata wahalifu wengi tu kwa approach inayostahili.

Bashite aweke vyeti mezani hatutaki blah blah
Hebu nawe weka vyeti vyako hapa isikuwa unadai vyeti vya mwingine wakati wewe huna hata cheti cha madrasa.
 
Kwa ufupi

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.


Aaaaah! Kumbe ni mtoto wa baba yake mkubwa!!!! Hata hivyo ni ndugu hawa. Kwani hakuweza kwenda kumwona kaka yake wakyamaliza nyumbani kuliko anavyofanya hivi???? Mmmh mimi nimchome kaka yangu au dada yangu mbele ya kadamnasi????? Mmmmh!!!!
 
Ndugu wa Ngwajima anasema Ngwaji hajawai hata kufufua panya ndio aweze binadamu hahaha sasa misukule ina amini atafufua binadamu...
Ndio hoja mliyobaki nayo! Na hujui hao unaowaita misukule % kubwa mule kanisani ni kijani. Endelea kujitoa ufahamu.
 
Akuwekee atakutoa wapi sasa??? Weka namba ako ya simu hapa akupigie???

Hahaaa mnataka vyeti mnajificha nyuma ya keyboard nyambafuuyu
Hii ni mijadala huru mkuu kuitana nyambafuu sio kitu chema.

Majina ya wauza unga alitutajia kwenye simu?
 
Ha ha ha!!! Naona anamonea wivu ndugu yake!!! La kujiuliza ni ndugu yake kweli? Hebu tusubiri Bishop Gwajima atakavyomjibu jpili.
Mtu wa Mungu akiongozwa na Roho wa Hekima na Maarifa; Roho wa Utambuzi na Maono; Roho wa Ishara na Maajabu; Roho wa Nguvu na Uweza anaenda kutoa neno soon. Ole ni wao mamlaka za kuzimu!
 
Sisi watz tumechoka na ujinga wenu hoja ya msingi hapa ni.madawa ya kulevya ni siyo ujinga wenu .
Watu wamekalia ujinga ujinga,ushabiki ushabiki.once utakapoingia kwenye janga la madawa wewe,ama mwanao,nduguyo au yeyote aliyekaribu yako ndo utaelewa.kwa sasa ngoja tukuache uendelee kushabiki hamna namna yakikukutaa utatuletea mrejesho hapa.refer to langa,nando,chidi benz,gwea,rayc,geez mabovu....

Daudi bashite i support you 100%.
Hakuna mtanzania mwingine atakaeweza kama wewe...

Nasema hivyo kwa sababu watanzania hawako tayari wauza sembe waguswe kwa jinsi yeyote
 
Haya maelezo yako yamekuja kipindi kibaya, utumike usitumike,iwe ridhaa yako isiwe yako, iwe vita, uwe urafiki wana dar es salaama tunataka BASHITE ATOE VYETI hizo njia za ujanja ujanja anazozitumia kumaliza hili soo hazimsaidii
 
Undugu wao ukoje?,
Wivu wa maendeleo na utofauti wa imani vimetawala hapo.
Mamlaka husika za Tanzania zitachukua hatua kwa mwanaCCM bila kuzishinikiza?
 
Mdogo wake hana jina? Ngoja tusubirie jpili ya mapigo. Undugu baba zao mashamba yalikuwa jirani.
 
Hii ni mijadala huru mkuu kuitana nyambafuu sio kitu chema.

Majina ya wauza unga alitutajia kwenye simu?
Wewe ni muajiri wake kutaka akupatie vyeti vyake??? Wewe mbona vya kwako hujaviweka hapa hadharani???
 
Hahahahaha

Huyu Jamaa anaitwa Joshua Chiwanga nimesoma naye kwa nimjuavyo mimi wala hana undugu na Gwajima...Labda undugu wa kupewa ili ifanyike Press Conference ya kumtetea Gwajima.....

Hahahaha Joshua naona umekuwa mpunga ndugu yangu....Tukumbukane aisee!
Umenikumbusha STAR TV waliokota mtu wakati wa uchaguzi wakaandika na kutangaza kuwa mtoto wa Kingunge yuko kinyume na uamuzi wa baba yake kuingia CDM siku 3 kabla ya uchaguzi cha ajabu kesho yake familia ilikanusha kwanza Kingunge ana mtoto mmoja na anajulikana.
 
yeye nae atueleze nae yupo mbele ya nani.kama ni ndugu yame akamshauri huko huko kunako undugu.
kazi yetu kwa sasa ni kushughulikia habari za vyeti vya kugushi vya mgushi vyeti.
 
Nilishapita, ila nachungulia tu tena na kuwasalimu


Hahahahaaaaaaaaaaaa

Na vya kwenda kolo.... inajulikana yote yale uongo aaaaagh

Makonda oyeeeee
 
Daudi Mchambuzi, nawe usiwe kasuku kila siku kurukia jambo usilokuwa na uhakika nalo.

Kwanza Bashite ni nani? Kama humjui nyamaza. Kama unamjua na unataka vyeti vyake kuviona, mfuate akuoneshe, ujiridhishe, kisha urudi hapa jamvini kutujuza.

Najua huna ujasiri huo ila kujificha nyuma ya keyboard na kulalama tu.
Hongera wewe ulieko mbele ya Keyboard, au macho yangu maana sioni verified user.
 
Back
Top Bottom